Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Kwel hapo umezingua hatakama una muhudumia utakiwi kumuita jina la lako baadae italeta mtafaruku kwa mtoto ,
Sema hongera kwa kumhudumia ila watoto kama hao uwa wanakaa kwa bibi zao mama zao wakiolewa ili wasiharibu ndoa .
 
Jacklyn na Theodore walikuwa ni wapenzi wa muda mrefu,

Baada ya kumaliza masomo Yao walifunga ndoa na kumzaa mtoto aitwaye Jeffrey

Kutokana na ugumu wa maisha hasa baada ya Jeffren Kuzaliwa, miezi 18 baadaye Theodore alikimbia familia na kumuacha Jacklyn akiwa katika Hali ngumu kimaisha

Mungu hamtupi mja wake, Japo Jacklyn alikuwa tayari ana mtoto, Mzee baba Miguel Besos (Mike Bezoz) alimpenda Jacklyn na kuamua kumuoa kisheria

Baada ya Kumuoa tu, Jambo la msingi ambalo alilifanya ni kumuasili yule mtoto Jeffren kutoka kuwa Jeffren T. Jorgensen na kuwa Jeffren M. Bezoz

Huyu ndio Jeffren Bezoz maarufu kama Jeff Bezoz

Tajiri namba 2 duniani ambaye alilelewa na baba wa Kambo, na baba wa kambo alimpatia mahitaji yote muhimu kama mwanae wa kumzaa

Kwa kifupi tu ni kwamba Mzee Sasahivi anakula pensen ya mwanae tu

Naami mleta mda nada utakuwa umepata kitu

Kwa upande wangu hujakosea, umefanya maamuzi sahihi,

Hongera Sana.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Wewe na singo maza wako wote mmekosea.

Tukianza na wewe ni kweli unahudumia mtoto, ila hukupaswa kubadilisha ubini bila kukaa na mwenzio mkakubaliana. ULIKOSEA KUFANYA MAAMUZI PEKE YAKO.

Tuje kwa singo maza wako, HAJIHESHIMU NA HAKUHESHIMU, ni kweli ulimkwaza na kumkosea ila ilitakiwa akwambie bila kutumia maneno makali kama "zaa wa kwako"

Kumuacha inawezekana ni sahihi au sio sahihi, hayo majibu yake yanatia mashaka.

Kusomesha mtoto na kufanya kila kitu, FANYA KAMA UNAMLEA YATIMA NA USITARAJIE LOLOTE, UKISHINDWA KUFANYA HIVYO NI BORA UACHE KABISA MAANA UTAUMIA ZAIDI YA HAPO.

Ni mimi singo maza mstaafu.
kweli kabisa usemayo
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.

Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.

Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80, sms 30
Zaa wakwako umpe uo ubini wako simple tu
 
Hakuna kitu kinakera kama unajipinda na hali hii ilivyo ngumu kumlipia school fees na matunzo mengine mtoto wa single mother kwa sababu uko na mama yake kwenye mahusiano then midaftari yote imeandikwa majina ya mwanaume mwingine ambaye yuko bussy na mambo yake uko. Then mbaya zaidi mtoto awe anamfanana baba yake ndo inakera zaidi. Yaani ukimuona mtoto unamuona mme mwenzako in full effect
Ha ha ha
 
Sasa mkuu shida ni moja nataka kumpiga chini huyu mwanamke ila kila nikimuangalia huyu mtoto roho inaniuma sana sababu huyu mtoto nimemlea tangu akiwa na mwaka mmoja (1) na anajua kabisa mimi ndio baba yake mzazi.
Mama yake ni kichwa panzi katika kipindi chote iko cha miaka 4 hataki kuzaa mpaka nimuoe.
Dogo upstairs yupo vizuri sana Naona nikimpiga chini mama yake huyu dogo ataharibikiwa sana
Zaa wakwako bana
 
Hivi single maza huwa anajielewa?
Maana mi mpaka leo nimedate nao wa 5 sikuona "Kujielewa?"

Huyo ajaachana na baby daddy wake ndio maana.

Mi Kuna mmoja kila siku "Nakupenda" ila asichojua ni kwamba najua "anaendelea kuchat na ukaribu na baby daddy wake"

#YNWA
We ulitaka wasichart kwa sababu zipi labda,,? Kwasababu yako? We ulijaza nini tumboni mwake cha kumpa jeuri ya kujiita mwanamke au mama,kaa kwa kutulia hivyo hivyo...familia ni baba,mama,watoto so we ni mvamizi
 
Sasa mkuu shida ni moja nataka kumpiga chini huyu mwanamke ila kila nikimuangalia huyu mtoto roho inaniuma sana sababu huyu mtoto nimemlea tangu akiwa na mwaka mmoja (1) na anajua kabisa mimi ndio baba yake mzazi.
Mama yake ni kichwa panzi katika kipindi chote iko cha miaka 4 hataki kuzaa mpaka nimuoe.
Dogo upstairs yupo vizuri sana Naona nikimpiga chini mama yake huyu dogo ataharibikiwa sana
Wewe hata ungelea mimba na utumbo wake,huwezi kua baba mzazi wa huyo chali....ondoa hilo tatizo kwenye himaya yako mkuu
 
Hapana
Mtoa mada ameshaleta mrejesho hapa,tafuta juu huko!
Kasema alimpiga chini lkn alikuwa tayari ana mimba yake, Kwa ss analea tu hiyo mimba yake
Sasa wake nae apewe ubini wa huko atakakoolewa mama yake , aone kama ni rahisi!
 
Una bahati sana umempata mwanamke mwenye akili. Sheria ya Mtoto Sura 13 tafsiri rasmi ya mwaka 2014 Ibara ya 6 (1-2) inasema hivi:
" Haki ya jina na utaifa 6.-(1) Mtoto atakuwa na haki ya jina, utaifa na kuwafahamu wazazi wake wa kumzaa na ndugu wengine wa familia tandaa.(2) Mtu hatamyima mtoto haki yake ya jina, utaifa na kufahamu wazazi wake wa kumzaa na ndugu zake wengine kwa kuzingatia masharti ya sheria nyingine".

Ulichotaka kufanya wewe ni kosa Kisheria. Mtoto anapaswa kuitwa kwa ubini wa wazazio wake halisi wa kibaolojia. Kwa huyo mtoto wewe ni mlezi tu. Hivyo, huna sababu ya makasiriko, mpende mke wako, Zaa naye mtoto atakayeitwa kwa ubini wako. Kwa huyo mtoto wewe unabaki kama mlezi tu.
 
Alikuwa sahihi, mtoto sio wako, baba yake yupo hata kama hayupo nae ila haibadilishi kuwa mtoto ni wa kwake.

Wewe utajisikiaje ukija kuambiwa kuwa hayo majina uliyo nayo si ya kwako kwa asili yaani yupo baba yako mzazi ambaye ni ubini mwingine kabisa?

Nadhani ifike wakati tujue kutenganisha hisia na uhalisia.

Mpe mtoto jina la baba yake. Muache mama yake amlee hadi miaka saba then baba mtu aitwe mzungumze namna atakuja kuchukua mtoto wake akalee mwenyewe kwasababu mtoto akifikisha umri wa kuanzia miaka saba kuendelea anaweza kuishi na baba yake mbali na mama yake bila shida kwa sharti tu huyu baba mzazi awe na uwezo wa kumudu malezi ya mtoto na awe na mwanamke wa kusaidizana nae.
 
Ndo kashamuacha!
Uzuri kamuacha na mimba, sasa ngoja asikie mwanae kaitwa jina la baba mlezi

Yani watu wengine bana!
 
Alikuwa sahihi, mtoto sio wako, baba yake yupo hata kama hayupo nae ila haibadilishi kuwa mtoto ni wa kwake.

Wewe utajisikiaje ukija kuambiwa kuwa hayo majina uliyo nayo si ya kwako kwa asili yaani yupo baba yako mzazi ambaye ni ubini mwingine kabisa?

Nadhani ifike wakati tujue kutenganisha hisia na uhalisia.

Mpe mtoto jina la baba yake. Muache mama yake amlee hadi miaka saba then baba mtu aitwe mzungumze namna atakuja kuchukua mtoto wake akalee mwenyewe kwasababu mtoto akifikisha umri wa kuanzia miaka saba kuendelea anaweza kuishi na baba yake mbali na mama yake bila shida kwa sharti tu huyu baba mzazi awe na uwezo wa kumudu malezi ya mtoto na awe na mwanamke wa kusaidizana nae.
Alishaleta mrejesho kamuacha!
 
Kama hyo mtoto amebatizwa cheti chake cha ubatizo kina jina halisi la baba wa mtoto hvyo mtoto sio wako!!!!
 
Back
Top Bottom