Mke wangu kanibadilikia baada ya ndoa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wangu kanibadilikia baada ya ndoa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Access Denied, Oct 11, 2012.

 1. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Hali zenu wana JF, imenibidi nitumie jukwaa hili ili kuweza kupata ushauri wa busara na hekima. Mimi nimekua na mahusiano na msichana mmoja hivi kwa takribani miaka 6 hivi na hatimaye mwanzoni mwa mwaka tukakubaliana kuingia ktk ndoa. Kimsingi tumeishi vizuri sana kipindi chote cha uchumba wetu potelea mbali matatizo madogo madogo ambayo ni ya kawaida ktk mapenzi, lakini kilichonifanya kuanzisha huu uzi ni kwamba toka nianze kukaa nae mwezi wa 7 amekua na tabia ya kunichagulia marafiki wa kuwasiliana nao kwny simu kitendo ambacho kinanikera sana na tabia hii hakua nayo mwanzo, sms ikiingia anataka awe wa kwanza kusoma hata simu yng ikiita anataka aone nani anapiga na jana nilipigiwa simu na rafiki tu wa kike na yeye alikua nje akifua nguo baada ya kusikia nikiongea kwny simu alikuja dirishani ili kusikiliza mazungumzo yetu na kiukweli yalikua ni mazungumzo ya kawaida ya kutakiana hali cha ajabu yeye akakasirika na kudai kwanini nawasiliana na wasichana nikamwelesha lakini bado, na ikaingia sms ya gd9t tu ya hy hy msichana basi ndo ikawa tabu akaninunia mpaka mda huu hatujaongea nae hata chakula nimekula hotelini. Sijawahi kumcheat hy mwanamke lkn kwake naonekana namcheat daily, nimeongea nae kuhusu hili suala hadi nimechoka. Naomba mnishauri nifanye nini maana nimeishavunja urafiki na watu wengi na nimebadili laini hadi watu wananishangaa lakini kwake hy haitoshi. Nampenda sana lakini huu mwenendo wake umenichosha.
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,284
  Likes Received: 12,995
  Trophy Points: 280
  Upendo hauna wivu. The devil is about to eat you up unajua kitu inaitwa divide and rule hahahah kama tujuavyo ndoa ni takatifu,ukiona mshikamano then ukaanza on matatizo jua shetani ameingia na anataka awatenganishe ili awatumie vizuri
  Muhimu omba sana usijeingia majaribuni

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tayari binti kampata amfurahishaye, jifunze mbinu mpya, acha kuishi kwa mazoea.
   
 4. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  huenda mienendo yako inamfanya asikuamini,jichunguze pia mwonyeshe wampenda na u mwaminifu kwake
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Mpige Mimba ata kuifata simu ataona uvivu..
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  kaka hilo ni kosa kubwa sana. Mimi nimejifunza siwezi kuwa na msichana mwingize ama kuzoeana na demu mwingine zaidi ya msichana wangu tu. thats all. So nakushauri uachane kabisa na wasichana wengine ukiwazoea ama wanakupigia ama nini utaipoteza ndoa. Hapo mke wako hana kosa na yupo so right wewe omba msamaha na focus kwa mke wako tu .
   
 7. The Only Kilo

  The Only Kilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua nini mkuu hapa huyu mwanamke ameshakucheat tayari.....sasa anacho hisi moyoni ni kwamba tabia alizoziona kwa mwanaume waliokula naye utamu anaanza kuhisi na wewe oviazi utakuwa hivyo so anajaribu kukuchunga huku akijipigia picha ya jaaa ake mpya kua inawezekena wote mpo hivyo....ni saikolojia tu lakini inavyonituma japo kwa umakini sana unaweza kuona ukweli ndani yake
   
 8. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Poa mkuu nimekusoma nitajitahidi kubadilika mimi.
   
 9. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Hapo si itakua zaidi maana nasikia wakiwa na mimba ndo huzidisha matatizo!
   
 10. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Mimi USHAURI WANGU NAUTOA FRM EXPERIANCE!!!!!! My Broo nae kabla ya kuoa alikua SWEETIE wa mademu kibao, na hata kuchangia harusi walichanga kinomaaa! Sasa baada ya kuoa si ndio IKAWA KASHESHE!!! Bi dada kila simu ikiita ANAVIMBA KAMA KOBRAAAA! Tukamshauri awe Dk 3 Mbele!!!! Sasa wale SWEETIE umewaambia unaoa nao hawana tabu na mtu, na wamekuchangia, huwezi KUKATA MAWASILIANO GHAFLA!!! Na wengine ni wateja wazuri coz anafanya BUSINESS TOKA CHINA!!!! SULUHISHO TULILOFIKIA NI KUWA NA SIMU MBILI, TENA KAMUONESHA MKEWE, MOJA YA BUSINESS, INALALA KWENYE GARI, NYINGINE YA PERSONAL NDO ANAINGIA NAYO MATRIMONIAL ROOM! LOLEST! Tena Bi Dada alipigwa biti kuwa ASIIZOEE ZOEE ILE SIMU YA BUSINESS KABISA, HIYO PERSONAL AKITAKA ASHINDE NAYO, AKAAMBIWA KAMA ANATAKA WALE MAWE HUMO NDANI ACHEZEE BUSINESS CONECTIONS AND NETWORKS!!! Hahahaaaaaa! Simu anaitaka kuikagua, Kula mawe haweziii, ALISONYAJE KIMYA KIMYA!!! Sasa na wewe UMEWEKEE MKEO MIPAKA!!!! LOL! (Mimi sikuombi kukagua, NAKULIA TIMING TU! IKIINGIA KWENYE 18 ZANGU, NAMBA TATA ZOTE NAZIKOPI, WALA SIKUULIZI, NAZITAFUTIA LINE YA MAGUMASHI!!! UTAISOMA KIMYA! KIMYA! KILA NAYEMSHUKU ATALIJUA JIJI KUWASILIANA NA WEWE! LOLEST!!!)
   
 11. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Acha kuzoeana na wasichana wengine, hata kama mlikua na mazoea before ndoa sasa hivi tengeneza mipaka ya maana.Mfano mzuri ni mimi mwenyewe,nilivooa kuna wasichana tumesoma nao na bahati mbaya mimi tokea naanza shule nimesoma shule za mchanganyiko yaani co-education na pia wengine tunafanya nao kazi. Lakini baada ya kumweka mama watoto ndani simu zisizo za lazima nilishaambia sitaki unless ni mchana au ni wakati ambao najua kuwa mke wangu yupo mbali na mimi.

  Nafanya hivo sio kusema kuwa namcheat mke wangu, la hasha nafanya hivo kwa kuwa sitaki mke wangu awe na chembe ya doubt na mimi.Pia kuna wasichana wengine ni marafiki zangu na wamenisaidia to the certain point to reach here am kwa hiyo si mbaya kuwatambulisha kwa mke wako na once unapopokea simu ya hao wasichana mke wako anakuwa huru kidogo lakini sio njia ya kila muda kuwasiliana na hao wasichana na pia wasiwe wengi kama uyoga maybe wawili watatu bt wasizidi.Ni mbaya sana mke wako kuanza kukuhisi kuwa unamcheat please just be open with her na kama unaona hapendi hayo mawasiliano just cut it off completely maana bwana mama watoto ni mama watoto tu
   
 12. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  aaaah Lara1 umetishaa...ila shughuli utapokutana na shankupe wa m/nyamala au tandale kwa tumbo,nakwambia shilingi itakugeuka utajuta kumchokonoa..
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kuna ukweli kuhusu uaminifu wako kwake. Lakini mwangalie kama ana ujauzito, kama anao basi wala usihangaike we kuwa mpole tu manake dada zetu wakipata ujauzito psychologically wanakuwa hawajiamini na hii hupelekea matatizo madogomadogo katika ndoa. Kuwa mpole mkuu!!!
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mambo ya good night toka kwa mdada mwingine yanatoka wapi?ingekua ni mkeo katumiwa g9t na mwanamume mwingine ungejiskiaje??? Acha mazoea yasiyo na mipaka na vibinti vingine na ndoa yako itadumu
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  gudnite nawe za nini?
   
 16. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mkeo hana kosa lolote, maandiko ya dini yanaonya dhidi ya kuikaribia zinaa(cm zinachangia), hivyo mkeo anafanya kazi ya kukulinda ili kesho usije na kisingizio cha shetani alinipitia.
  Punguza/sitsha mawasiliano yote yasiyo na msingi na hao wasichana na ndoa yako itakuwa na amani.
   
 17. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Wewe kwani NAMTUKANA UNADHANI!!! Nampa tu live, kuwa amegonga ikulu, sasa kama anayaweza AENDELEE KUNYEA KAMBI YANGU, Namtisha kama namba yake nimeipata hata yeye siku si nyingi NAMTAITISHA KWENYE 18 ZANGU!!! Alafu atajua kama maharage ni mboga au kiungo cha makande.!!! Akimuuliza mzinifu mwenzie, ANAKATAA KATA KATA KUHUSIKA NA UTOAJI NAMBA,( SI SIJAMUULIZA!!!!) TENA ANAMUHISI BI DADA KICHECHE COZ KAMA SI YEYE BASI KUNA BWANA MWENGINE demu wake ndo kalikoroga!!! ANAJUTAJE KUNICHEAT!!!! MIMI KIMYAAA! WANAUANA WENYEWE TU!!!! Hahahaaaaa! (HII INAITWA TAKING CARE OF THE PROBLEM FROM THE INSIDE!!!!)
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Taasisi mbili mhimu zilianzishwa ndani ya wiki ya kwanza amnazo ni ndoa na sabato, lakini zote shetani ameshavuruga. Sasa angala sana ndoa yako huyu muongo na mwovu(shetani) asije akavuruga ndoa yako. Ila kuna kitu amacho nimesajaribu kukichunguza, kwenye mahusiano anayemshutumu mwenzake kuwa anatoka nje mara nyingi ndiye anayefanya hivyo.
  Haialishi uthamni wa kiti ambacho shetani amekupatia hapa duniani, mwisho wake ni maafa.
   
 19. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Kuna tabia vijana huwa tunashindwa kuzielewa na mipaka yake hasa baada ya kuingia kwenye mahusiano rasmi(NDOA),wewe umeoa halafu bado ungependa kuendelea kuwa na maisha yaleyale ya kabla ya kuoa,Ushauri ni kwamba kuna mambo you need to udjust yourself kusogea kwa mwenzi nae pia,Unapokuwa umeoa kuna aina ya marafiki is obviously huwa wanaondoka,i mean si kuacha nao kimahusiano but urafiki wenu unakuwa na mipaka na kama ni wanawake usiruhusu wakuchukulie kama bado uko alone,kila mtu akioa ama kuolewa huamini kuwa mwenzi wake ni HIMAYA yake hivyo hatopenda kuingiliwa na yeyote na kwa namna yoyote ile.So bro jitambue sehem gani unakosea na ufanye marekebisho mapema ndoa yako haijamaliza mwaka ni hatari kuacha hali hiyo kuendelea.Kaa chini na mwenzio na kujadili kwa kina na mapana yake pasi na kuhusisha hisia busara na hekima vitawale mazungumzo yenu na hakika njia hiyo itawafanya muendelee kuheshimiana na kujenga upendo wenu pasipo kutiliana mashaka.Mwenyezi Mungu awatangulie katika kupata suluhu la Mahusiano haya muhimu.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Inawezekana comment yako ni nzuri sana, ila una mwandiko mbaya sana, sisomagi miye miandiko mibovu kama hii.

  Unapokuwa JF moja ya faida unazozipata ni kujifunza namna ya kuandika kwa kutenganisha paragraph. chukua hii, utaki unaacha.
   
Loading...