Access Denied
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 655
- 211
Hali zenu wana JF, imenibidi nitumie jukwaa hili ili kuweza kupata ushauri wa busara na hekima. Mimi nimekua na mahusiano na msichana mmoja hivi kwa takribani miaka 6 hivi na hatimaye mwanzoni mwa mwaka tukakubaliana kuingia ktk ndoa. Kimsingi tumeishi vizuri sana kipindi chote cha uchumba wetu potelea mbali matatizo madogo madogo ambayo ni ya kawaida ktk mapenzi, lakini kilichonifanya kuanzisha huu uzi ni kwamba toka nianze kukaa nae mwezi wa 7 amekua na tabia ya kunichagulia marafiki wa kuwasiliana nao kwny simu kitendo ambacho kinanikera sana na tabia hii hakua nayo mwanzo, sms ikiingia anataka awe wa kwanza kusoma hata simu yng ikiita anataka aone nani anapiga na jana nilipigiwa simu na rafiki tu wa kike na yeye alikua nje akifua nguo baada ya kusikia nikiongea kwny simu alikuja dirishani ili kusikiliza mazungumzo yetu na kiukweli yalikua ni mazungumzo ya kawaida ya kutakiana hali cha ajabu yeye akakasirika na kudai kwanini nawasiliana na wasichana nikamwelesha lakini bado, na ikaingia sms ya gd9t tu ya hy hy msichana basi ndo ikawa tabu akaninunia mpaka mda huu hatujaongea nae hata chakula nimekula hotelini. Sijawahi kumcheat hy mwanamke lkn kwake naonekana namcheat daily, nimeongea nae kuhusu hili suala hadi nimechoka. Naomba mnishauri nifanye nini maana nimeishavunja urafiki na watu wengi na nimebadili laini hadi watu wananishangaa lakini kwake hy haitoshi. Nampenda sana lakini huu mwenendo wake umenichosha.