Mke wangu kakutana na EX wake tukiwa pamoja, kafurahi hakuna mfano!

Aisee mnatutisha.
Ndio maana wengine tunasitasita kuoa.
Hiyo scenario ni rahisi kuijadili ila usiombe ikutokee.
Yaani mimi hata sijui ningechukua hatua gani ila ninachojua huyo mke ana dharau hata kama huyo rafiki yake amem-snitch kwa maslahi binafsi
 
Kijana, huna haja ya kuwa na hasira wala kutomsemesha mkeo.

Kama tatizo kwako ni taarifa ya yeye kutoa mimba mbili akiwa chuoni hiyo inaonyesha tu aina ya mwanamke uliyemuoa, japo anaweza kuwa amebadilika na kuwa mke mwema. Je ulimuuliza kuhusu taarifa hizo za kutoa mimba mbili? Kama ni kweli hiyo inaathiri ndoa yako?

Au kama hasira zinakuja kwa kuwa jamaa ana hela kukuzidi hiyo inategemea na aina ya mke uliyenaye je anatamani hela zisizo zake?!

Kwa sasa tulia na ufanye mambo yako kwa busara. Unapo ''panic'' na kununa unaonyesha mambo mawili tu kwa mkeo;

1. Hujiamini, yaani fanya yote mbele ya mkeo ila sio kuonyesha kutojiamini tena kwa sababu ya mwanaume mwingine. Wanawake ni wazui sana kwenye kukupima na kukuona namna unavyo ''hemukwa'' kwa vitu kama hivyo.

2. Unaogopa kuwa jamaa atamchukua; hapa ndio unaharibu kabisa, yaani hata kama hakuwa na wazo la kurudiana naye basi unaandaa njia kwa wao kufufua upya mahusiano yao.

Jambo la kuzingatia ni kuangalia nyendo za mkeo kwa ukaribu zaidi bila ya kuonyesha wasiwasi wala papara.

Kwa huyo rafiki wa mkeo aliyekupa taarifa, je ulimuuliza lengo la taarifa zake?!

Kuhusu mkeo kuficha hisia na kuonyesha malavidavi mbele yako hilo ni swala lingine, katika hali ya kawaida mwanamke anayejielewa na kuthamini ndoa yake ilipasa awe na kiasi katika hilo.
 
Pole , ila tangu ulipoaa na kukuta watu weshapita kuwa mpole wewe jali kama anakujali na kukupenda!!
je ushwahi muuliza walitingisha nyavu wangapi hapo? na wako wapi?

UKWELI: Kama waliachana bila ugomvi wewe jua jamaa litamla tu!! no way out!! na ushahidi upo, kama waliachana kwa ugomvi hizo bashsha zisingekuwepo. jifanye hujui tafuta vielelzo vikikamilika basi ni adultery case na - mwisho ni kuachana !!
 
'' shemeji naomba namba zako maana hapa mjini hwezi jua kuna kesho na kesho kutwa''................huu mstari umebeba ujumbe mzito sana na nimemwelewa huyo sasa na nimefurahi sana kuuona mstari huo..
 
Yani huyo anatakiwa kijiti cha kalio, af kwanini aombe wakati shoga ake hayupo mashoga wengine wathenge mxyuuuu

shemeji naomba namba yako maana hapa mjini huwezi kujua kuna kesho na keshokutwa...hapo ndo ujumbe wa huyo dada ulipo kwa huyu jamaa....
 
nina miaka 33 na watoto wawili niliozaa na wanawake tofauti. sina mpango wa kuoa kwa sasa,naendelea kutafuta pesa kwa ajili ya wanangu na mimi mwenyewe. hii midemu iliyograduate huwa imegraduate kuanzia virgin,michepuko hadi utoaji wa mimba afu bado ikiolewa ni mizinzi na viburi juu. me nimeizalisha afu nimepiga chini yote. watoto ndo mpango,ni heri nisaidie ndugu zangu tu. sometimes huwa tunalaumu sana islamic fundamentalists ideology ya kuwatreat hawa wanawake lakini wapo ok,yakae home,yazae,yalee,yapike,yafanye usafi wa nyumba n.k.
 
ahahahhahaha...mie ningekuwa wewe...ningeuagiza mchepuko wangu uje mliman city nikiwa na wife halafu nauambia tukikaa ukituona uje utusalimie na tutahughiana vibaya sana kisha utanikaribisha mezani kwao na warembo wenzake...lazima nikirudi nikute ushafika home na umenuna mbaya.....MWAGA MBOGA NIMWAGE UGALI UKILETA VYOKO NAMWAGIA MAJI MKAA ULIOPIKIA CHAKULA.
 
Mkuu, unajua kuwa hata mamako aliyekuleta hapa duniani naye ni mmojawapo wa "yakae, yazae, yalee, yapike, yafanye usafi wa nyumba"? Wanawake hasa wa siku hizi wana matatizo yao lakini hata sisi wanaume mambo ni yale yale. Kuwadharau na kuwadogosha namna hii wala siyo dili unless kama uko sexist.
 
"Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yy ndie source ya hiyo habari"

Huu ni umbea sasa.. yeye shemeji yako yanamuhusu nini?Ukifanya mchezo mtaachana kisa umbea wa shemejio yake yamemshinda anaanza kukufukunyua na nyie yakushinde shoga wake naye awe ameachika...

Think big mwanaume acha kufuatilia umbea babue.. kama mkeo hajawahi kukucheat ya nyuma yanakuhusu nini? we umefanya mafinyo finyo mangapi kabla ujakutana na mkeo... ACHA KUFUATILIA HABARI ZA UMBEA NDOA ITAKUSHINDA LOH....

Pole sana ndugu najua hisia zako yeyote anaweza kuwa nazo iwe na mke au mume..., tena ingekuwa mbaya zaidi kama ingekuwa ni wewe umekutana na EX wako, mkeo angelianzisha papo hapo ila wanaume tumeumbwa na subira ya kiwango cha kuridhisha..

Ushauri huu wa miss chagga ni mzuri ila yote kwa yote Akili ya kuambiwa changanya na yako...
 
Last edited by a moderator:
ahahahhahaha...mie ningekuwa wewe...ningeuagiza mchepuko wangu uje mliman city nikiwa na wife halafu nauambia tukikaa ukituona uje utusalimie na tutahughiana vibaya sana kisha utanikaribisha mezani kwao na warembo wenzake...lazima nikirudi nikute ushafika home na umenuna mbaya.....MWAGA MBOGA NIMWAGE UGALI UKILETA VYOKO NAMWAGIA MAJI MKAA ULIOPIKIA CHAKULA.

Sio lazima awe michepuko wako, unaweza kula deal tu na warembo wa dar, ukapiga offers huku ukamtikisa kidogo wife, dah umenipa kaujanja

Ha haa
 
Pole sana ndugu najua hisia zako yeyote anaweza kuwa nazo iwe na mke au mume..., tena ingekuwa mbaya zaidi kama ingekuwa ni wewe umekutana na EX wako, mkeo angelianzisha papo hapo ila wanaume tumeumbwa na subira ya kiwango cha kuridhisha..

Ushauri huu wa miss chagga ni mzuri ila yote kwa yote Akili ya kuambiwa changanya na yako...
iala inauma
 
sio lazima awe michepuko wako, unaweza kula deal tu na warembo wa dar, ukapiga offers huku ukamtikisa kidogo wife, dah umenipa kaujanja

ha haa

ndio hivyooo...ujuwe hawa wake zetu wanajisahaugi wakituona tumetulia wanajua tumezeeka na ujanja hatuna...ukichanganya na mitishamba wanayotuwekea kwenye vyakula na maji ya kuoga wanaona wamatuteeeeka wenyewe.

Sasa kumuweka kwenye mstari mnyoofu...unakula deal na wema sepetu, irene uwoya, lulu, aunt ezekiel, wolper na bongo movies woote wa ukweli na wanaojulikana kwa kukamata vidume vya watu...sikuhiyo unamwambia lulu aje akuhugh na kukuchum mbele yake kisha unahamia mezani kwao unawapiga bia mbaya.....lazima kesho umsikie kalazwa ana presha bp, oilcom na puma vyote kwa mpigo...ahahahaha
 
'' shemeji naomba namba zako maana hapa mjini hwezi jua kuna kesho na kesho kutwa''................huu mstari umebeba ujumbe mzito sana na nimemwelewa huyo sasa na nimefurahi sana kuuona mstari huo..

Anataka LOSE LOSE situation... wakose wote...
dah wanawake bana
 
iala inauma

Ni kweli maumivu yake si rahisi sana kuyaelezea, na ndio maana pamoja na ushauri wako mzuri kabisa bado atakiwa kuchanganya na akili yake vinginevyo siona kama kuna aina ya ushauri unaoweza kumpa faraja ya haraka. Ni suala la muda tu atulie atafakari na kuchunguza nyendo za mkewe kiasha ajue ni njia ipi sahihi.
 
Back
Top Bottom