Mke wangu kakutana na EX wake tukiwa pamoja, kafurahi hakuna mfano!

Ni kweli maumivu yake si rahisi sana kuyaelezea, na ndio maana pamoja na ushauri wako mzuri kabisa bado atakiwa kuchanganya na akili yake vinginevyo siona kama kuna aina ya ushauri unaoweza kumpa faraja ya haraka. Ni suala la muda tu atulie atafakari na kuchunguza nyendo za mkewe kiasha ajue ni njia ipi sahihi.
kweli kabisa .. ila hizi ndoa ni shida
 
Ni taabu kweli, walioko nje wanatamani kuingia na waliomo wanatafuta watoke vipi, basi ni timbwiliko
 
Hahahahaha unatisha
ndio hivyooo...ujuwe hawa wake zetu wanajisahaugi wakituona tumetulia wanajua tumezeeka na ujanja hatuna...ukichanganya na mitishamba wanayotuwekea kwenye vyakula na maji ya kuoga wanaona wamatuteeeeka wenyewe.

Sasa kumuweka kwenye mstari mnyoofu...unakula deal na wema sepetu, irene uwoya, lulu, aunt ezekiel, wolper na bongo movies woote wa ukweli na wanaojulikana kwa kukamata vidume vya watu...sikuhiyo unamwambia lulu aje akuhugh na kukuchum mbele yake kisha unahamia mezani kwao unawapiga bia mbaya.....lazima kesho umsikie kalazwa ana presha bp, oilcom na puma vyote kwa mpigo...ahahahaha
 
Pembeni kama hayupo ruksa? (anyway joking), wakati mwingine ukute jamaa alivamia kambi kutokana na penzi la mbali na huyo jamaa wakajikuta wanapoteana huku jamaa akaonyesha bidii ya kumdhibiti mrembo mpaka akaoa kumbe demu alikuwa ana feeling za msela (mzee wa ku-hug ila ndo hivyo alikuwa haeleweki na wakawa wamepotezana mwisho wa siku jamaa akaoa)

"That is what I call thinking out of the box"
 
Wakuu nawasalimu.

Nimetatizwa sana na jambo moja. Last Sunday tulienda Mlimani City na wife kwa matembezi ya jioni na kununua mahitaji machache ya ndani. Wakati tumefika mataa ya Mwenge, akampigia girlfriend simu wakutane hapo maana anaishi Survey jirani na hapo. Hivyo tukawa watatu kwenye mizunguko ya humo mall; mimi, wife na girlfriend who is a family friend to us ingawa mimi sina mazoea nae kiiivile.

Mwisho tukakaa nje tukawa tunakunywa pombe zetu taratibu. Kwenye saa mbili kasoro usiku akajitokeza jamaa mmoja, baada ya kutuona akaja kutusalimia, ambapo wife aliinuka kwa shangwe kubwa kumlaki kwa hugs na zile kiss za mashavuni wanaopiganaga wale wanaojifanya wazungu.

Wife akanitambulisha kuwa "he is a longtime friend". Lile jitu likazungusha round ya vinywaji, na pia likaniomba liende limtambulishe wife kwenye meza yao nikakubali ingawa moyoni nilikua nimefura kwa hasira, sema sikutaka kuonesha, bahati mbaya zaidi meza ya hilo jitu ilijaa wanaume pekee.

Tukabaki wawili wakati wife anaongea na meza ile, yule girlfriend akasema "shemeji naomba namba yako hapa mjini huwezi kujua ya kesho na keshokutwa", nami nikajibu ni kweli kabisa, tukabadilishana namba.

Monday yule binti akanipigia simu nikiwa kazini akaniambia shemeji kuna jambo nataka kukuambia ila usinitaje, nikajibu poa, akasema, "Yule jamaa wa jana ni ex wa mkeo. Walikua wapenzi kwa miaka yote mitatu chuoni wakiishi chumba kimoja nje ya chuo kama mke na Mume".

Na kwamba kwa kipindi chote cha hiyo 3 yrs alitoa kama mimba 2 hivi za huyo mshikaji, pia uhusiano wao ulienda hadi mtaani after university life. Walikuja kuachana kila mtu alipopata kazi yule ndugu akapelekwa Bukoba. Since then hawajawahi kuonana hadi hiyo jumapili pale Mlimani City, na kwamba lile jitu limerudishwa hapa Dar na halijaoa bado ila lina mapene sana.

Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yy ndie source ya hiyo habari. Huyu binti ni rafiki wa wife tangu chuo ila bahati mbaya ndoa yake ilipata shida kidogo na kushindikana kutokana na uzinzi wa mwanaume

Ndugu wana JF, niliporudi home jioni ya monday nikaamua kulianzisha, ambapo wife alidai hakuona busara kunitambulisha kwamba yule bwana alikua ex wake.

Nikamuuliza ilikuaje ukafurahi na kushangilia kiasi kile na kushindwa kuficha kabisa hisia zako? Akabaki anajiuma uma tu na kushindwa kujibu.

Kiukweli sijaridhika na majibu yale na bado nina hasira. Nimekaa kimya bila kumuongelesha chochote wala kumsemesha kwa salaam wakati nikitafakari hatua ya kuchukua.

Nimekuja kwenu kwa msaada zaidi..

ndo matatizo ya kuoa mwanamke aliyebikiriwa na wahuni huko nje
 
Mmmmh kazi kwelkwel... Imagine wangekutana wawili peke yao ingekuwaaje... Si haba angerudi home baada ya wiki
 
Back
Top Bottom