Mke wangu hatoi maziwa ya kutosha kwa kichanga chetu cha siku nne

kvelia

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
246
44
Wataalam na wenye uzoefu wa malezi ya watoto wadogo kuanzia siku sifuri na kuendelea. Mwanangu wa kwanza ana siku nne kwa sasa, Imenilazimu kutumia lactogen (1) ili kuongeza kiwango cha maziwa anachokihitaji mtoto. Natambua umuhimu wa maziwa ya mamake lakini bila kufanya hivyo hali ingekuwa mbaya. NAOMBENI MSAADA NIFANYEJE ILI MKE WANGU APATE MAZIWA YA KUTOSHA. NITASHIKURU SANA WAKUU.
 
Wataalam na wenye uzoefu wa malezi ya watoto wadogo kuanzia siku sifuri na kuendelea. Mwanangu wa kwanza ana siku nne kwa sasa, Imenilazimu kutumia lactogen (1) ili kuongeza kiwango cha maziwa anachokihitaji mtoto. Natambua umuhimu wa maziwa ya mamake lakini bila kufanya hivyo hali ingekuwa mbaya. NAOMBENI MSAADA NIFANYEJE ILI MKE WANGU APATE MAZIWA YA KUTOSHA. NITASHIKURU SANA WAKUU.

atumie uji wenye pilipili manga, pia kama unaweza pata pweza atumie ile supu yake tu ilimsaidia wife sana.
 
Hongera kwa kichanga mkuu! Kinaitwa nani vile? Nadhani ushauri umeupata, pia jitahidi mama ale vizuri sana siku za mwanzo huwa maziwa yanasumbua sumbua.
 
apewe uji wa pilipili manga anywe kwa wing japo mara 3 kwa cku na uwe wa moto , ni vyema akatumia bakuri kubwa mathalan ambalo linaweza kuunga vikombe 4 na kuendelea. supu aweke nyanya chungu, pia wakati wa kukandwa mkandaji asisahau kukanda kifua, mabega na kwapa. . . hmgera kwa kichanga
 
Aloweke mchele ( Kama kilo 1) kwenye lita 2 za maji safi na salama kwa muda wa nusu saa hivi kisha ayachuje vizuri na kunywa hayo maji yote ndani ya masaa 10 hivi akisindikizia na matole ( nyanya chungu) ambazo hazijapikwa kama 3 au 4 hivi. Hata kama ana mapacha 3 huyo mzazi atakuwa na maziwa ya kutosha kabisaa!!


Angalizo : Mzazi mwenye tatizo la kisukari hashauriwi kutumia tiba mbadala hii!
 
yanyonye wewe kuya activate...maziwa yapo yanangoja tu kuwa activated..wala sio issue ya medical hiyo ni software tu inahitaji activation
 
Jamani nashukuruni sana, ngoja nikafanye hivyo sasa. KICHANGA CHANGU (cha kiume) KINAITWA HERO (KILIZALIWA SIKU YA MASHUJAA). Kigogo kaniacha hoi japo ni kweli....... asanteni sana...
 
yanyonye wewe kuya activate...maziwa yapo yanangoja tu kuwa activated..wala sio issue ya medical hiyo ni software tu inahitaji activation
Mkuu Kigogo hii ndio dawa pekee!.

Mkuu Kivelia, mimi ni baba wa watoto 6 hivyo ushauri nitakao kupa ni from experiance na sio theory!.

1. Kwanza hongera kupata mtoto!.

2. Usihofu sana ukidhani ni tatizo kubwa sana, ni kawaida kwa baadhi ya wamama kushindwa kutoa maziwa mara tuu baada ya uzazi, au kutoa maziwa kidogo kuliko mahitaji ya mtoto kwa sababu mbalimbali up to seven days!. Kutokana na ugeni wa uzazi kwa kuzinga huyo ndiye mtoto wenu wa kwanza, s/he would have survived on water!, umeharakisha kukimbilia Lactogen 1!.

3. Miongoni mwa sababu za kuchelewa kutoa maziwa ya kutosha!.
Maziwa yanatengenezwa na tezi za Mamary glands, ili ziweze kutengeza maziwa kuna vimeng'enyo vya estrogen na progestrogen ambazo ziko resiponsible kuandaa mamary glands kuanza milk production kuanzia miezi 3 baada ya ujauzito. Ili Mamary glands zifanye kazi husika, zinahitaji kuwa activated by ceresing from time to time!, unaonyesha wewe kwenye "foreplay" ulikuwa unayaogopa kuyatomasa tomasa, matokeo ni glands ziko slowa kwenye production!. Dawa ya hapa ni activation, kwa kuyakamua kwa mikono na kuongeza production catalysts mbalimbali, moja wapo maarufu ni uji wa pilipili manga, mtori wa moto na kwa Wachagga kisusio!.

4. Maumbile tuu ya maziwa, kuna wanawake wameumbwa na maziwa yenye maumbile madogo ambayo hata yatengeneze full production, hayatoshi kukashibisha kachanga, na hapa supplement ni lazima!.

5. Mtoto amezaliwa pre-mature au slow learner hivyo hana uwezo kwa ku suck inavyopaswa, wife wako anatengeneza maziwa ya kutosha, ila uwezo wa kichanga ku suck na kuactivate full production, ni mdogo, in this case, itabidi mnunue artificial sucker, kuyakamua muaziwa ya mama na kumnywesha mtoto mtoto atakapo develop uwezo wake wa ku suck mwenyewe!.

6. Stress na emotions state ya mama, inaweza kumfanya restless akashindwa kutengeneza maziwa ya kutosha, hapa dawa ni upendo tuu na assurance1.
 
Back
Top Bottom