Mke wangu hatari kwa uchumi wangu

Mke wangu hatari kwa uchumi wangu

IPTL one

Member
Joined
Jan 9, 2018
Posts
9
Reaction score
4
Habari wana JF,

Nimekuja mbele zenu naombeni ushauri,

Mimi ninamke tumedumu kwenye ndoa miaka minne mpaka sasa bahati mbaya hatujabahatika kupata mtoto wala hata ujauzito kuharibika japo nje ya ndoa ninamtoto na hata mwenzangu analijua hilo.

Lakini maswala ya uzazi na mwenzangu hayajawahi kuninyima raha kwani naamini ipo siku ya itakuwa poa na nimejaribu mara kadhaa kutoka nje ya ndoa kufanya kama self test nakuta niko poa na hata saizi natarajia kupata mtoto mwingine kutoka kwa mchepuko ambao nilikua nao hata kabla ya kuoa maana ulinipenda sana, tukatibuana baada ya mimi kuoa baadae nikauweka sawa tukarudiana pia huo mchepuko wangu ulisha wahi kutoa mimba kabla hata sijaoa kwasababu eti sikuonesha future nao na baada ya kurudiana nao mwaka juzi ulidaka tena ujauzito ambao ulidai ni wangu lakini bahati mbaya ikatoka na sasa ni mjamzito tena na hii tulipanga kabisa wala sio bahati mbaya kwani muda wowote atajifungua.

Pia mbali na huyo mchepuko kuna mwingine mimba ilitoka kwa sababu ya magonjwa ya zinaa ambayo hata mimi yalinipata na nikatibiwa na kuachana nae.

Sasa kinachonikera na kuniudhi zaidi kwa wife mpaka nawaza kuachana nae ni kwamba kwanza wakati namuoa hali ya uchumi ilikua stable kiasi now nimeshuka na mwenzangu ni mtu ambaye anajali sana kwao.

Kuliko hata maisha yetu pamoja na kwamba kwao wazazi wake wote ni waajiriwa na familia yao ni ndogo kuliko ya upande wetu pia kwetu mimi ndio tegemeo na ndio first born sasa napata hofu kuendelea nae afu amekua ni mtu mwenye kupenda kuonesha anauwezo hata kama hali haiko hivyo je nikikua kiuchumi itakuaje?

Naomba ushauri nifanye ili nimuache huyu au nitengeneze sababu ya aina gani itakayofaa?
 
Habari wana JF ;

Nimekuja mbele zenu naombeni ushauri , mm ninamke tumedum kwenye ndoa miaka minne mpaka sasa bahati mbaya hatujabahatika kupata mtoto wala hata ujauzito kuharibika japo nje ya ndoa ninamtoto na hata mwenzangu analijua hilo.

Lkn maswala ya uzazi na mwenzangu hayajawahi kuninyima raha kwani naamini ipo siku yataku poa na nimejaribu mara kadhaa kutoka nje ya ndoa kufanya kama self test nakuta Niko poa na hata saizi natarajia kupata mtoto mwingine kutoka kwa mchepuko ambao nilikua nao hata kabla ya kuoa maana ulinipenda sana tukatibuana beada ya mm kuoa baadae nikauweka sawa tukarudiana pia huo mchepuko wangu ulisha wahi kutoa mimba kabla hata sijaoa kwasababu eti sikuonesha future nao na baada ya kurudiana nao mwaka juzi ulidaka tena ujauzito ambao ulidai ni wangu lkn bahati mbaya ikatoka na sasa ni mjamzito tena na hii tulipanga kabisa wala sio bahati mbaya kwani muda wowote atajifungua

Pia mbali na huyo mchepuko kuna mwingine mimba ilitoka kwa sababu ya magonjwa ya zinaa ambayo hata mm yalinipata na nikatibiwa na kuachana nae

Sasa kinacho nikela na kuniudhi zaidi kwa wife mpaka nawaza kuachana nae nikwamba kwanza wakati namuoa hali ya uchumi ilikua stable kiasi now nimeshuka na mwenzangu ni mtu ambaye anajali sana kwao kuliko hata maisha yetu pamoja na kwamba kwao wazazi wake wote ni waajiliwa na familia yao ni ndogo kuliko ya upande wetu pia kwetu mm ndio tegemeo na ndio first born sasa napata hofu kuendelea nae afu Amekua ni mtu mwenye kupenda kuonesha anauwezo hata kama hali haiko hivyo je nikikua kiuchumi itakuaje?


Naomba ushauri nifanye ili nimuache huyu au nitengeneze sababu ya aina gani itakayo faa ?
Mkuu hyo ndio ndoa,usikate tamaa mwanamke ni mwanafunzi kwetu japo mama zetu ni walimu kwetu.Tambua kwamba unakipimo unahtaji kukivuka hapo usiogope sana.majaribu madogo tu ila japo wanasema "HERI UCHUMBA ULIOVUNJIKA KULIKO NDOA ISIYOKUWA NA UPENDO,FURAHA,NA AMANI" Akil kuchwani kwako. HAKUNA MSHAURI MZURI ZAIDI YA MOYO WAKO NA NAFSI YAKO"
 
Daaah mkuu usiumie na huu mwezi Wa January!!.

Sema nn ,,, Kama athar nikubwa za kiuchumi na zinazoenda kinyume na makubaliano yenu,Huyo si/ni Mke nakinachomuumiza Hana mtoto.

Aiseeee sikushaul umuache ila jaribu kumwelewesha kwa UPENDO SANA.

naumuaminishe kua "Mke Wangu ,kuzaa nimajaaliwa ila Mimi Nakupenda Sanaaaa".... Ujue ukute kinachofanya awe ivo anajihisi atakuja kupoteza Sikh za usoni !!.
 
Mi natabiri kuvunjika kwa ndoa yenu, hata kama wewe utakuwa umeamua muishi tu!
ndoa yenu ina matatizo yanayovunja 90% ya ndoa

1. kutokuwa na uelewano ktk fedha
2. Mke kutopata uzazi
3. mke kudhamini kwao kuliko kwake (popo)
 
Unajua tabia ni Kama ngozi.....hamna Jinsi ya kuirekebisha.....Ila asio na hili Ana lile....so angalia mema yake na mabaya yapi yanazidiana.......wanawake Ndo hawahawa tu.....
 
Piga chini mapema kabisa. Akili yake iko salama kabisa kua kuna cku utamwacha tu kutokana n hilo tatizo lake. Awe tayri kajijenga kwao mapema kisha ww akuache umepigika kipesa n kukosa mtoto nae. Yy atakua ka win kuliko ww mkuu
 
Mi naamini yote hayo yasingekuwa na nguvu, km hasingekuwa na tatzo la uzazi.. Unafikiria, "kwanza hazai, alafu ananikwaza hapa na pale" hayo yote msingi mkubwa wa kutaka kumuacha umetokana na yy kutokukupatia mtoto.. Nadhani unamuona km hasara
 
Mi natabiri kuvunjika kwa ndoa yenu, hata kama wewe utakuwa umeamua muishi tu!
ndoa yenu ina matatizo yanayovunja 90% ya ndoa

1. kutokuwa na uelewano ktk fedha
2. Mke kutopata uzazi
3. mke kudhamini kwao kuliko kwake (popo)

Kitakachovunja ndoa yake ni dhambi ya uzinzi anayoifanya ya kuzaa na michepuko yake. Hizo zingine hazina uzito sana. Hata vitabu vya dini vimekemea uzinzi na ikibainika mmojawapo wa wana ndoa amekosa uaminifu basi talaka yaweza kutolewa.
 
Back
Top Bottom