MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,588
naogopa ku mwambia umwache yasije nitokea yaliyonikuta huko nyuma. mwaka juzi mdogo wangu alioa mke kutoka mikoani, sasa alipomuowa yule mke akawa na vitimbi vya ajabu ajabu na mara anadai huyo mme siyo chaguo lake, ndani pakawa hapakaliki na mimi mwenyewe nikaona kweli ndani hakuna maelewano. siku moja mdogo wangu akawapigia wazazi wa yule mke wake akawaelezea kila kitu. wale wazazi walipompigia mtoto wao (mke wa dogo), mwanao akawajibu hivi...kwani baba we ndio umeolewa huku? msinilazimishe kuishi na mtu ambaye mm simtaki. hapo na mm nilikuwa naskia na naona hiyo movie...hapohapo nikachukua uamuzi wa kumshauri dogo amuache. sikujua kuwa dogo alikuwa anaomba ushauri wa kumfukuza mke wake ili hali bado anampenda, wakienda kitandani wanabembelezana. baade dogo kanambia..aah, nimeamua nimsamehe amesema atajirekebisha, ngoja tuone itakuwaje hapo baadae.
then wakaanza kuishi wote na mimi niliyetoa ushauri wa kuachana nikaanza kuona aibu. pamoja na kuwa wanaishi lakini wanaishi maisha ya bora liende..mwanamke ni mchungu kama pilipili, namuonea sana huruma dogo maana ile siyo ndoa ni ndoano.
ndio maana nasema msimshauri amwache huenda anampenda sana na nyie atawashangaa kwa ushauri wenu maamuzi ya mwisho anayo yeye...maana ndiye anayefinywa...
katikaa vitu vigumu ni kuowaa mke au mume aliachikaa...wengi wanaachikaa kwa visirani huyo wako chunguza aliachika kwa kitu gani...je kweli alipewa talaka au ndo alichomoka tu akakupata ukavuta ndani sasaa hivi unaliaa.pole sanaaa...ila sio ndoa hiyo ndoano
Achana naye huyo,atakuua bure!mwenzio nilishaweka nadhiri ya kutokuoa aliyeachika ama aliyekwishazaa!
Pole sana,hongera yataka moyo kuoa mwanamke aliyeisha achika kwa mumewe kwanza.......
Nakushauri tulia na jipange vizuri kukabiliana naye.....huo ni mwanzo tu,kama alimuacha wa kwanza akakupata wewe then anajua aweza mpata/kama si anaye mwingine.......
Muombe Mungu akulinde na aondoke salama,huna mke,una mwanamke unayeishi nae chini ya dari moja.......let her go....forgive....move on!!!!
Na kama yuko kwa dada yake na dada yake haoni tatizo,then hata ndugu zake hawana busara au labda hawakutaki......kama unampenda sana mpe muda uone,mshirikishe Mungu na wazazi na ndugu zako pia,watakushauri.
nimeoa mwanamke aliyeisha olewa zamani na akaachika, maelewano na masikilizano ndani ya nyumba mwanzo yalikuwa mazuri, ukorofi ukaanza ghafla, akashika mimba akaenda itoa kisha akadai imetoka yenyewe, safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na vitu vyake alivyokuja navyo kwangu akawa anahamisha kidogo kidogo kila nnapokuwa sipo.
Nilipomuuliza akadai yeye kuna mtu amemuazima pesa na ili akasome ndio kaamua na yeye amuazime vitu vyake kisha akimaliza kusoma ataenda kuvigomboa, nikamuuliza mbona mimi hukunishirikisha ktk hilo japo vitu ni vyako, basi kuanzia hapo ni makeke tu na hivi huyo hakufai achana nae kama aliishaachika na hakujifunza sasa wewe unaendelea nae wanini na katoa mimba yako hakuna upendo hapo tafuta mwingine au unampenda bado maana masuala ya mapenzi huwa ni magumu sana tunaweza kukushauri na bado tukashangaa umekiuka ushauri wetu!niongeapo yuko kwa dada yake yapata wiki na zaidi hakuna ugomvi zaidi ya hilo suala, jana ananiambia uko kimya hali ya kuwa unajua nahitaji kwenda kusoma huku sina hela nikueleweje, NIMEMWAMBIA KAMA UNAJUA MIMI NI MUMEO NAWAJIBIKA KWA HILO NI VIPI UKAE KWA DADA YAKO ...?
NIMEKATA MAWASILIANO NA YEYE KAKAA KIMYA ..........
nimeoa mwanamke aliyeisha olewa zamani na akaachika, maelewano na masikilizano ndani ya nyumba mwanzo yalikuwa mazuri, ukorofi ukaanza ghafla, akashika mimba akaenda itoa kisha akadai imetoka yenyewe, safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na vitu vyake alivyokuja navyo kwangu akawa anahamisha kidogo kidogo kila nnapokuwa sipo.
Nilipomuuliza akadai yeye kuna mtu amemuazima pesa na ili akasome ndio kaamua na yeye amuazime vitu vyake kisha akimaliza kusoma ataenda kuvigomboa, nikamuuliza mbona mimi hukunishirikisha ktk hilo japo vitu ni vyako, basi kuanzia hapo ni makeke tu na hivi niongeapo yuko kwa dada yake yapata wiki na zaidi hakuna ugomvi zaidi ya hilo suala, jana ananiambia uko kimya hali ya kuwa unajua nahitaji kwenda kusoma huku sina hela nikueleweje, NIMEMWAMBIA KAMA UNAJUA MIMI NI MUMEO NAWAJIBIKA KWA HILO NI VIPI UKAE KWA DADA YAKO ...?
NIMEKATA MAWASILIANO NA YEYE KAKAA KIMYA ..........