Mke wangu hanielewi kabisa!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kauli kama hii hutoka vinywani mwa wanaume wengi. Lakini, je, unajua ni kwa kiasi gani kauli hii huwa haina ukweli hata chembe? Huenda hujui kabisa, au inawezekana pia nawe ni mmoja kati ya wale wanaowalalamikia wenza wao kuwa hawawaelewi.

Wanaume mara nyingi sana ndio mashujaa wa kudai kwamba wake zao au wapenzi wao hawawaelewi na hivyo kuwatupia mzigo pale uhusiano unapovunjika. Lakini ukweli ni kwamba wanaume ndio ambao huwa hawawaelewi wanawake kwenye uhusiano.Mara nyingi wanaume wanakuwa tayari wameweka kichwani dhana kwamba wanawake ni tatizo-hawaaminiki, wanasumbua, wana wivu wanapenda kukalia wanaume wakipewa nafasi na mengine ya aina hiyo. Dhana hizo zinakuwa zimejijenga kutokea utotoni katika malezi na katika mazingira anamokulia. Kumbuka mfumo-dume ndiyo unaoongoza duniani.

Kwa hiyo mwanamke anaposema ‘A' mwanaume kutokana na kuwa tayari ameshamhukumu mwanamke, huwa anasikia ‘B' na hivyo hujibu ‘C' na hapo ndipo matatizo ya mawasiliano yanapoanzia. Mwanamke anaweza kujaribu tena kutaka kufikisha ujumbe anaotaka kuufikisha kwa mumewe, lakini safari hii atakuwa na hasira. Mumewe naye atapandisha hasira kwa sababu hajui ni kwa nini aambiwe jambo kwa hasira, na hapo ndipo kisirani kinapoanzia.

Ni wazi wengi wetu tumeshawahi kusikia wanawake wanaolalamika, ‘ndugu yangu mimi sijui nifanyeje, kitu kidogo mtagombana wee hadi unajiona huna maana…..' Lakini miongoni mwetu wanawake wanaweza pia kuwa mashahidi wa hali hii, kwamba, wanapojitahidi kuelezea hisia zao kwa upendo, wanaume wanakuwa wakali bila sababu hadi wanafikia mahali ambapo kila siku kuna malumbano ndani ya nyumba. Haya ni matokeo ya wanaume kushindwa kujua namna ya kuwasliana na wake au wapenzi wao.

Kuna haja ya wanaume kujua kwamba, kuwasikiliza wake zao kwa umakini na kuwaelewa ni sehemu muhimu sana katika kukamilsha uanaume wao. Tatizo la wanaume wengi ni kushindwa kwao kutofautisha kati ya kuwasikiliza wake au wapenzi wao na kuwakubalia. Wanadhani wakiwasikiliza kwa makini itakuwa ni sawa na kuwakubalia, hivyo wanapoona wanaongea jambo ambalo wao hawakubaliani nalo huacha kuwasikiliza, kuwakatisha au kuwaponda kwa njia ya kebehi na dharau. Wanachoshindwa kujua ni kwamba, mara zote wanawake huhitaji kusikiliizwa na siyo kukubaliwa mawazo yao au hisia zao.
 
Wamarekani hawajatoa fungu la kusema naye, wakitoa wanandoa wataelewana tu.
Mara samaki wa kupaka mara chipsi dume zooote wataweza kuziongelea
 
Mtambuzi bana...........kama hakuelewi sio mkeo tena huyo!! angalia vizuri utaona manyoya!

Ha ha ha ha haaaaa..............Memo, ina maana atakuwa ameshaliwa!?...............LOL
 
Wamarekani hawajatoa fungu la kusema naye, wakitoa wanandoa wataelewana tu.
Mara samaki wa kupaka mara chipsi dume zooote wataweza kuziongelea

Kongosho, haki ya Mungu sijakuelewa, naona umetumia misamiati, ngeli, nahau na tamathali................fafanua please...........LOL
 
mtambuzi.......

inawezekana wanaume huwa hamna masikio? au mnachagua cha kusikia? au ndo "mwanamke anaposema ‘A' mwanaume kutokana na kuwa tayari ameshamhukumu mwanamke, huwa anasikia ‘B' na hivyo hujibu ‘C'?"

hii huwa inakera sana
 
Shikamoo baba,
Nashukuru ww km mwanaume umeliona na kulitambua hili,
Hope nia yako ni kupenda mahusiano /ndoa za vijana wako/wababa wenzako zikiwa ktk maelewano,
Haya wakaka/wababa Mzee leo kawaletea nondo hiyo.
 
Inataka kutumia akili sana kuishi maisha ya ndoa. Siku nyingine nashindwa kuelewa what the hell is happening around me! Ila nashukuru moyo wangu umetanuka umekuwa mkubwaa nayabeba yote na kutulia kimya nikiangalia mambo ya maana yaliyo mbele yangu.
 
Ishu siku kusikiliza pekee yake, unasikiliza na kupima ulichoambiwa kama kina tija aul laaa. Huwezi kukubaliana na kila unachoambiwa ndg yangu, utashindwa kuimudu familia yako!
 
If you cant shoot the moon, rest be assured you will never shoot any star, you know why?
Stars are far far away from the earth, at least the moon is within the earth's orbit.
A star is a sun with its complete solar system. Tena some of them are bigger that our sun.

[SIZE=4 said:
"I want to shoot the moon...and even if it happens that I fail, I will land among the stars"[/SIZE].
 
Mchambizi, you have made a point, but, Easier said than done! kwenye ndoa kuna mengi sana.

Have you ever heard of 10 commandments of love?
Do you apply them?
Do they work in your marriage?
 
Ishu siku kusikiliza pekee yake, unasikiliza na kupima ulichoambiwa kama kina tija aul laaa. Huwezi kukubaliana na kila unachoambiwa ndg yangu, utashindwa kuimudu familia yako!

Tatizo huwa wanaume wanapima kabla ya kusikiliza, na hapo ndipo tatizo hutokea........................
 
Inataka kutumia akili sana kuishi maisha ya ndoa. Siku nyingine nashindwa kuelewa what the hell is happening around me! Ila nashukuru moyo wangu umetanuka umekuwa mkubwaa nayabeba yote na kutulia kimya nikiangalia mambo ya maana yaliyo mbele yangu.

Huo ndio uanaume, na siku zote kinachotushinda wanaume wengi ni subira...................... Huo ndio mtihani mkubwa sana kwetu.
 
Back
Top Bottom