'Mke wangu hajapendeza'

'Mke wangu hajapendeza'

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,094
Reaction score
79,492
Anaandika, Robert Heriel
Mume wa mke mmoja.

"Sijategemea kama huku ndiko tulikofika, ninahasira. Hasira za nini bwana mdogo? Acha! Acheni tuu. Nina hasira hapa, nafikiri polisi na madaktari watapata kazi na mteja hivi punde. Bado nafikiria chakumfanya huyu mpuuzi, mshenzi Sana. Serikali iingilie Kati, kuna watu wana machezo ya kipuuzi, machezo yao uozo, wanafikiri mimi napenda dezo kama wao. Ngoja tuone."

"Embu tulia bwana mdogo ueleze nini tatizo, Nitulie! Wewe ungetulia! Nakuuliza wewe mkeo angeambiwa hajapendeza ungetulia? Nijibu sasa, unanitazama unadhani upo kwenye maonyesho! Nyokonyoko! Nyashinyashi! Unajifanya una hekma kama mwenyekiti wa hitma."

Mimi nimetoka zangu na mke wangu mama Tobi, hao kwa mguu siyo kama wao wenye magari yao. Kwa mguu bila makuu tukafika Kanisani, nilifikiri Dunia tuu ndiyo imebadilika lakini hata kanisani nako nilikuta pamebadilika, sio majengo tuu bali mpaka waumini niliowakuta humo.

Mbona unanitazama sana kama hujui nilipokuwa, unataka kujua nilikuwa wapi miaka yote? Nilikuwa hapo hapo mtaani nikilipita Kanisa kama nyumba ya mtu anayenidai. Mwaka wa kumi huu sijatia miguu hii unayoiona kanisani.

Shida zikanirejesha, kodi nadaiwa, hakuna ambaye pale mtaani kwetu hanidai, nimekuwa mdaiwa sugu ambaye mpaka vituo vya polisi vyote vinanifahamu. Huko kituoni tuu Mkuu wa Kituo naye ananidai. Sasa nimeona nimkimbilie tuu Mungu wangu, nikasema huko nako nikakope tuu hamna namna.

Mimi pekeangu kwenye lile Kanisa ndiyo nilikuwa sinukii mafuta na marashi mazuri. Mimi pekeangu ndiye niliyekuwa nimevaa marapurapu utadhani Budah wa Kipare. Mimi yekeyangu ndiye nywele zangu hazikuwa na rutuba, labda ni kutokana na maisha kunichachafya kama chafya ya mtu aliyekula ngusigii ya Wamasai.

Mimi pekee ndiye niliyekuwa nina biblia ya kisela ambayo imechoka vibaya mno. Mimi pekee! Mimi pekee! Ndiyo ni mimi pekee ambaye hata baadhi ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa nilikuwa namung'unya maneno utadhani nachana nyimbo ya Shaggy.

Sikujali, nikakaa zangu nikiwa na mke wangu kipenzi, mama Tobi, mtoto mzuri aliyeyavagaa kwa kuolewa na Taikon mwanajeshi aliyepoteza ramani na silaha.

Rafiki yangu wa kale aliponiona alifurahi sana. Akatufuata pale mlangoni tukiwa ndiyo tunaingia, akatukaribisha lakini akawa anamtazama sana mke wangu. Ni mpaka niliposoma kidani alichokivaa shingoni kimeandikwa Shemasi, ndipo nilipomsikia akisema, "Shemeji umependeza!"

Maneno hayo yakanifanya nimtazame mke wangu, Mama Tobi. Jamani! Jamani! Nitaua mtu!
Nilimuona mke wangu amefadhaika masikini, iweje aambiwe amependeza ilhali nguo alizozivaa ni mtindo wa zamani, lilikuwa gauni lililofubaa, lililomfanya aonekane amezubaa. Lilikuwa limepauka kama hadithi za Pauka pakawa.

Nywele za mke wangu Jamani! Hiii!hiiii! Acha kulia Taikon, tuliza munkari! Niache tuu nilie, hujui tuu vile ninavyojisikia. Mimi sio wa kumfanya mke wangu aonekane kituko vile. Hata kama ni umasikini lakini sio vile. Nilijiona sio mwanaume muwajibikaji.

Nywele za mke wangu zilikuwa zimepitwa na wakati wake na hazijui hata rangi yake ni gani. Hicho kibanio sasa!
Kauli ya Rafiki Shemasi ilikuwa ni kejeli na kijembe cha mimbarani kilichoamua kunitoa madhabahuni. Kumwambie mke wangu amependeza ilhali kwa uhakika alikuwa hajapendeza ilikuwa unafiki wa kiwango kikubwa ambapo ukiwa nao kwa Shetani unachukua mkopo mzuri tuu.

Kuanzia hapo macho yangu yakaanza kuangalia wanawake waliokuja hapo ibadani. Yalikuwa mashindano ungesema ya "Fashoni(fashion)". Kuna waliovalia magauni ya vitenge vya Kongo, hawa walitembea kwa madoido ya Kikongo.

Wapo waliovalia vitenge vya Java, hawa nao walikuwa na miondoko yao. Na wapo waliovalia vitenge vya Polista hao nao walitembea na kuweka mapozi ya kipolistapolista. Nikaona wanawake wengine wakiwa wamevaa Kimalkia Elizabeth, hawa walivaa sketi fupi za vitambaa zilizowachora maumbo yao vyema kabisa.

Wapo niliowapongeza kimoyo moyo kwa uzuri wa shepu zao, na wapo nilijikuta nikisonya nilipoona vigimbi na miguu iliyokomaa. Wapi huko, nipo Kanisani na yote yanatokea huko. Ndipo dunia ilipofikia?

Hazikuwa nywele zao kichwani, wengine waliweka weaving, wengine walisuka rasta, wengine na wengine walivaa malemba makubwa ungedhani ni Wanaijeria. Sikumuona aliyekuwa kama mke wangu, nafikiri yeye pekee ndio alikuwa hajapendeza.

Kwa upande wa wanaume niliwaona wakiwa wananyuso zilizokunjamana, wachache sana walikuwa wanasiha njema. Ila wengi wa wanaume walikuwa wamechoka ingawaje mavazi yao yalikuwa mazuri na nadhifu.

Nikazama ndani nikiwa na mke wangu. Ingawaje waumini walikuwa wametazama mbele ilipomimbari lakini niliona ni kana kwamba wanamacho kwenye visogo vyao. Niliona kanakwamba Kanisa zima linatutizama.
Tukaketi. Nikashusha pumzi mimi na mke wangu mama Tobi, huku katoto ketu kakishangaa ungedhani kameingia peponi.

Ukiwa haujapendeza hata ungebanwa na mkojo hautamani kutoka nje kwa kuogopa kuangaliwa na watu.
Utajikaza na kujikaza, lakini ukiona uvumilivu umekusaliti/umekushinda basi utavizia wakati wa maombi watu wakiwa wamefumba macho ndipo utoke kinyemela na hapo kuna uwezekano usirudi tena.

Wakati huo waliovaa vizuri wakapendeza wakipita pita na kujiundia visafari ili watu waone. Doooh! Ni kweli mke wangu alikuwa hajapendeza, na hii moyoni ikaniambia kuwa moja ya sababu za watu wa zama hizi kushindwa kwenda kanisani ni pamoja na hali duni za maisha na uhaba na nguo kwa waumini.

Nikajua kwa nini wanaume wengi hatupendi kanisani tukiwa familia. Hivi unaendaje kanisani mkeo na watoto hawajapendeza? Unaendaje kanisani michango inatajwa hutoi hata shilingi moja?

Basi nikamwambia mwanangu Tobi, maneno haya, "Mwanangu siku ukiwa mkubwa, ukaoa fanya kazi kwa nguvu zote, kusanya mali na pesa kadiri uwezavyo ili uweze kumtunza mkeo na watoto. Vinginevyo ukishindwa hata Mungu hautamuabudu. Utajiona unahatia, hutimizi wajibu na majukumu yako kama baba"

Nikiwa namalizia na hasira zangu, vijana tafuteni pesa, angalau muwe nazo kiasi. vinginevyo Mungu hamtamuabudu. Taikon yamenikuta.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
"MKE WANGU HAJAPENDEZA"

Anaandika, Robert Heriel
Mume wa Mke mmoja,

Sijategemea Kama huku ndiko tulikofika. Ninahasira, hasira za nini Bwana mdogo? Acha! Acheni tuu. Nina hasira hapa, nafikiri polisi na madaktari watapata kazi na mteja hivi punde.
Bado nafikiria chakumfanya huyu mpuuzi, mshenzi Sana.
Serikali iingilie Kati, kuna watu Wana machezo ya kipuuzi, machezo Yao uozo, wanafikiri Mimi napenda dezo Kama wao. Ngoja tuone.

Embu tulia Bwana mdogo ueleze nini tatizo,
Nitulie! Wewe ungetulia! Nakuuliza wewe Mkeo angeambiwa hajapendeza ungetulia? Nijibu sasa, unanitazama unadhani upo kwenye maonyesho! Nyokonyoko! Nyashinyashi! Unajifanya una hekma kama mwenyekiti wa Hitma.

Mimi nimetoka zangu na Mke wangu mama Tobi, hao Kwa mguu sio kama wao wenye magari Yao. Kwa mguu bila makuu tukafika Kanisani, nilifikiri Dunia tuu ndio imebadilika lakini hata kanisani nako nilikuta pamebadilika, sio majengo tuu Bali mpaka Waumini niliowakuta humo.

Mbona unanitazama Sana kama hujui nilipokuwa, unataka kujua nilikuwa wapi miaka yote,
Nilikuwa hapohapo mtaani nikilipita Kanisa Kama nyumba ya Mtu anayenidai. mwaka wa kumi huu sijatia miguu hiii unayoiona kanisani.

Shida zikanirejesha, Kodi nadaiwa, hakuna ambaye pale mtaani kwetu hanidai, nimekuwa mdaiwa sugu ambaye mpaka vituo vya polisi vyote vinanifahamu. Huko kituoni tuu Mkuu wa kituio

Taikon kulikoni hauoni jikoni hakusomi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom