Ebu wadau naombeni ushauri wenu. Nina mke na watoto wawili. Mke wangu ana changamoto moja hataki kupika na pia hajali watoto. Yaani tunaweza kukaa siku mbili tatu tunakula mikate na chai tu. Na yeye ni mama wa nyumbani sio kwamba ana shughuli kivile za kumkwamisha yeye kupika HAPANA.
Nikimwambia kwanini hapiki anadai sijaenda sokoni kununua vitu (asa nawaza si yeye ni jukumu lake kwenda sokoni) maana pesa za biashara tunazofanya ni yeye anashika kwahiyo sio kwamba haendi kwasababu hana pesa.
Kuhusu watoto ndio kabisa hawalishi wala hawaogeshi, na watoto ni wadogo chini ya miaka 5. Yaani watoto wasipojipambania wenyewe kula ndio basi hawali.
Kuna saa nakasirika kinoma lakini nakosa namna. NIFANYEJE
Ana umri gani huyo mkeo? kama ni kizazi cha instagramu na fecebook kazi unayo hapo ni wewe mume kuwa mbogo tu na sometime akiwa haelewai kwa kauli zako inabidi na makofi yahusike kidogo maana huyo inaonekana hana hofu na wewe kwa sababu anjua humgombezi, Kung’uta huyo akili imkae sawa
Yani wewe unafanyabiashara halafu hela anashika yeye, huna akili.
Tatizo lipo hapo, tunza pesa mwenyewe, mwenzako anakula chips zege deile huyo, ukirudi wewe ndio anakuektia na chai na mikate. Huu ni uzoba wa kujitakia.
Watoto wana DNA kubwa ya kwako kuliko ya mama ingawa wao ni wa mama. I mean baba tuna transfer genes zetu kwa vizazi vijavyo ila owner wa watoto ni mama.
Jambo la pili, mwanaume ukitaka uishi maisha mazuri uzeeni hakikisha una watoto wengi wa kike, hao hawatakuacha.
Sikuhizi kuna baadhi ya wanawake asilimia kubwa wamekuwa hovyo hawajali familia wala malezi na Wana act ka ma slay queen Bora mtu ka hujali watoto usizae tu.