Mke wangu haachi pesa ya matumizi

Mke wangu haachi pesa ya matumizi

ngulyavyangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2019
Posts
203
Reaction score
266
Ni mwaka wa Pili sasa tupo kwenye ndoa, nimejuananae toka tupo chuo mwaka wa kwanza.
Tuliishi pamoja ghetto hadi tunamaliza chuo, ivo namfamu vizuri Mke wangu na yeye ananifamu vizuri.

Mara baada ya kumaliza chuo nilibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ivi ya wachina, baada ya kufanya kazi kwa miezi kadhaa nikaona bora nimuite Mke wangu tuje tuishi Wote Kwani Wakati huo nilikua nimejitisheleza.
Wakati huo Mke wangu alikua Hana ili wala lile japo alishafanya interview nyingi tu lakini bado hakubahatika kupata kazi, kwa kipindi chote hiko Mimi nafanya kazi nilikua namtia moyo, kipindi chote hiko nafanya kazi hajawai kulala na njaa wala fashion yeyote kumpita.

Baada ya kukaa nyumbani takribani mwaka mzima bila kazi, Nakumbuka 11th mwezi 3 alifanikiwa kupata kazi kwenye taasisi moja ivi, Kwakweli turifurahi Sana hiyo siku, turimshukuru mungu kwa tusimamia na kupata kazi sote,.

Maisha yalienda tukiwa na furaha japo Kuna vitu vilinitatiza, japo Mke wangu anapokea mshaara Mkubwa Mara mbili yangu ila majukumu Yote ya kifamilia nilikua nayatekeleza Mimi, pesa yake sijui alikua anapereka wp Yaani hata gari anayotumia yeye Mimi ndie nilikua namjazia mafuta.

Kisanga kilianza baada ya mkataba wangu na wale wachina Kuisha, mwanzo mambo yalikua mepesi Mke wangu alinishauri na kunitia moyo, alikua anarudi kazini mapema japo kuna kazi nilikua nimeshazifanya km kufua, usafi wa nyumba n. K akirudi yeye kabla hata hajapumzika hunipikia chakula cha Jioni, asubuhi kabla hajaondoka huwa ananiachia kiasi cha pesa ya matumizi,,

Toka ile kazi imeisha yapata miezi minne sasa, nieleweke Sio kwamba kipindi chote hiki nimekaa tu nyumbani, nimehangaika na vyeti ofisi mbalimbali kutafuta kazi, Muda mwingi nipo na laptop yangu nafanya interviews online, kokote nikisikia Kuna nafasi za kazi mm huwa wa kwanza.

Shida kwa Mke zilianza takribani mwezi sasa, kidogo kidogo nikaanza kuona mabdiliko, akawa anachelewa kurudi, akirudi hanipikii anadai amechoka ivo ananipa pesa nikale mghawani na yeye anadai hajisikii kula, ila asubuhi lazma aache ela ya matumizi kwasababu anajua Sina ujanja wa kupata pesa.

Tumeenda ivyo mpaka majuzi Hari imeanza kuwa mbaya, akirudi hapiki wala hanipi pesa ya kwenda kula mghawani, mbaya zaidi asubuhi anaondoka aachi chochote,
Tena Jioni akirudi Hana hata Muda wa kunitazama yeye anaoga na kulala, Hataki hata kujua nimekula nini.

Naandika ivi toka Jana sijala, nyumbani Siwezi kupiga simu kuwaomba pesa kwasababu wanajua Mke wangu anafanya kazi mzuri tu.

Hari yangu mbaya Kwakweli nisaidieni hata kwa mawazo nifanyeje kwa Hari Hii niliyonayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hutu tumwanaume tunyonge twa kulia lia tulitokaga wapi?

Kosa wanalofanyaga wanaume ni kutojua kwamba mwanamke utakavyoanza nae ndivyo atakavyoishi na wewe.

Jifanye mnyonge, atakupanda kichwani the slightest window of opportunity she gets.
 
Unataka ushauri gani ndugu, wa kutafuta kazi au ushauri juu ya mkeo, mathalan awahi kurudi nyumbani, akupikie au akupe pesa walau ukale mgahawani kama hataki kuwahi kurudi nyumbani na kukupikia?
 
Mkuu hapo umekosa pesa ndo uijue tabia ya mkeo,cha msingi ni kupambana ujikwamue.

Kuhusu mkeo utajiongeza mwenyewe nini ufanye.
 
looh, pole sana mkuu! Wanawake hawa hawana ubinadamu kabisa.. ila kwa maelezo yako tayar mke ameshapata dume la kumpumulia, kama hamjapata mtoto tafuta maisha yako.. la sio utaishia kujutia kadiri unavyokuwepo, POLE SANA

ngulyavyangu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo huitaji ushauri ila ukifika wakati utapiga simu nyumbani na ukitumiwa pesa na wazazi wako ndiyo utajua wazazi na mke nani bora
 
Mkuu ke anakuaje na mke??
Siku hizi dunia imebadilika labda Ke kwa Ke wameona maana na utimamu wangu sijawahi kuona Mwanaume Rijali mwenye nguvu za ku2omb-e-a analalamika kutokuachiwa hela ya matumizi na mkewe.

CC Zero IQ
 
Back
Top Bottom