Mke wangu bado anawasiliana na Ex wake

Mke wangu bado anawasiliana na Ex wake

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,293
Reaction score
4,969
MOYO WANGU UNAUNGUA, SINA RAHA TENA!

Nimeoa mwanamke ambaye nimeishi naye miaka mitano hadi sasa. Wakati tunaingia katika mahusiano nilimkuta tayari ana mtoto ambaye alizalishwa na mwanaume mwingine na akamkimbia.

Kwa kuwa nilimpenda sana naye akanipenda sikuona mtoto kama kikwazo katika mahusiano yetu. Niliendelea kumpenda yeye pamoja na mtoto wake na kuwatunza wote vizuri.

Maisha yetu yalikuwa ya furaha sana, lakini miaka miwili iliyopita niligundua kumbe bado anawasiliana na mwanaume ambaye alimzalisha akamkimbia.

Nilimkanya, akaniambia hakuna chochote zaidi ya kutaka kujua hali ya mwanaye. Siku moja wakati nachungulia simu yake niliona kuna ujumbe kutoka kwa huyo mzazi mwenzie ambaye anamsifia kuwa sasa hivi amekuwa mtamu na anajua kukatika mauno.

Moyo ulinienda kasi sana, kwa ujasiri niliamua kumuuliza ambapo alikubali kuwa ni kweli amefanya naye mapenzi ila nimsamehe hatarudia tena.

Kuanzia hapo, nimekuwa sina raha katika ndoa yangu, moyo wangu unaungua kwa sababu mara kadhaa naendelea kuona wakiwasiliana.

Naomba ushauri wako, nifanyeje? Nitasoma comment zote kwani nahitaji kuokoa moyo wangu

Au nikanyage tu maisha yaendelee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe wasiliana na Ma X girlfriends. wako kama unadhani itakupa amani.

Lakini pia, amua kupuuza upumbavu wake, usiuweke akilini, jiepushe kushishika simu ya mkeo, utagundua Kuna Bodaboda anamfumua Malinda.

Simu ya mke ni kifo iepuke na kuigopa kama ukoma, as long as hafanyi mbele yako, anakuhishimu, anakutunza na kukutumikia.
 
Kama miaka yako ni chini ya 35 nyanyuka hapo aidha uwe bachela milele au ukaanze maisha mapya na mwanamke mwingine iwapo utahitaji familia. Mkeo uondoke kwa kuagana nae uzuri tuu na umwambie sababu ya kuondoka na usimamie msimamo wako hata akubembelezeje. Kama mna mtoto engrossed kutunza mwanao aidha atabaki nae yeye au utamlea wewe.

Kama miaka yako ni zaidi ya 40 huyo ni mkeo, mpotezee kanunue shamba mahali nje ya mnapoishi kila weekend aidha uwe unaenda nae shamba muwekee ratiba niwe bize na kujiandaa kustaafu halafu mdai K kila siku hata kama umechoka kula viagra ili hata akienda huko ale mabaki.

Acha ninywe red bull usingizi ukate maana sio Kwa mdondo huu nilionao... Bata tamu usingizi nao huu hapa...

Granny Matata.
 
Haiwezi kuwa sawa Ukiona mwanamke unamakataza asiwasiliane na mwanaume flani lakini hakusikiii jua Huyo mwanaume is far better than u ndo maana mwanamke haogopi kuwa utamuachaa wala nini..!!
pole sana kiongozi najua mzigo ulionao moyoni
Kwa wale ambao hawajui jinsi mapenzi yanauma watakubeza

Ila nalo litapita tuu kila kitu kitakua Sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama miaka yako ni chini ya 35 nyanyuka hapo aidha uwe bachela milele au ukaanze maisha mapya na mwanamke mwingine iwapo utahitaji familia. Mkeo uondoke kwa kuagana nae uzuri tuu na umwambie sababu ya kuondoka na usimamie msimamo wako hata akubembelezeje. Kama mna mtoto engrossed kutunza mwanao aidha atabaki nae yeye au utamlea wewe.

Kama miaka yako ni zaidi ya 40 huyo ni mkeo, mpotezee kanunue shamba mahali nje ya mnapoishi kila weekend aidha uwe unaenda nae shamba muwekee ratiba niwe bize na kujiandaa kustaafu halafu mdai K kila siku hata kama umechoka kula viagra ili hata akienda huko ale mabaki.

Acha ninywe red bull usingizi ukate maana sio Kwa mdondo huu nilionao... Bata tamu usingizi nao huu hapa...

Granny Matata.
Bravo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom