Mke wangu ananidai talaka ama ni wivu tu?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
613
313
Niko na mke wangu zaidi ya mika 10 sasa na tumebahatika kupata watoto 2.
Kutokanana na kua mke huyo anatatizo kidogo la uzazi wake ni wa mbali tukashauriana niengeze mke wa 2 hasa kwa vile dini inaniruhusu na kipato kinakizi japo sio sana kivile alikua akiniuliza kila siku nitaongeza lini mke wa 2 ila nikimuambia bado sijakua tayari siku zikasogea na kwa kua nilijua kua ataumia basi niliamua kuoa mke wa pili kisiri bila ya yeye kujua.

Baada ya kujua nimeowa alizua vurugu sana na kusema kua sikumtendea haki nilitakiwa kumjengea kwanza ndio nioe nikamuuliza nikujengee wapi akanionyesha nikaamua kumjengea nyumba ya vyumba 4 ili tukae nimeijenga kwa miezi miwili na nimeshaiezeka bado tuu kutia plaster na mengineyo.

Katika kipindi hichi cha Ramadhani walikua wakiftari pamoja maaana wote niliwaamuru wawe wanaftari kwa mkwe wao ili kujenga ukaribu wao na wakwe na mawifi zao kwa kua mke mkubwa alikua mwenyeji sana nyumbani na mwenzake alikua na miezi miwili tuuu basi matumizi yote nikawa nampa mke mkubwa na mdogo alikubali nifanye hivyo wakawa wanapika pamoja na kuzungumza na mengineyo.

Tatizo kua lililokuwepo kumbe mke mkubwa hatumii pale nyumbani kwa kisingizio mie siujamuachia pesa za matumizi kwa kua nimejenga na kuowa mke wa 2 inafikia wakati anapika wali tuuu bila ya mboga ama mchuzi wakati nilikua nimemuachia pesa ya kutosha kwa siku hio basi vurugu linazidi ikiwa siku hio silali kwake mara anajitia kuumwa maneno machafu kununa bila sababu ila siku ikiwa zamu yake hata mapishi hua mazuri.

Hukaaa na mke mwenziwe akajifanya kama dada yake akamchuma kua pengine nimempatia nini ama nimepanga nini na skukuu akimuambia pale hujifanya yuko sawa ila akija kwangu basi niko na msala akiniona nimempakia mke mdogo kwenye gari ama pikipiki hununa na hata kama hana safari naye huanzisha na ukisema huendi basi gumzo lake utajuta kuzaliwa.

Sasa kwa hali hii mi naona kma anadai talaka kiupande mwengine wivu ni sehemu ya maisha ya ndoa ila ukipitiliza unakera sana jambo limeshapita na nimemlipa kwa kumnunulia vitu vingi kabla ya kuowa ili mikiowa astahamili ila baada ya raha imekua karaha nisaidie mawazo wadau wenye hekima na suala hili la mathna.
 
Wake wawili inataka sana busara kuishi nao,
Nionavyo mimi bora uwatenganishe lakini kila mmoja umtimizie mahitaji yake kiasi itaepusha mizozo isiyo lazima.....pole sana mkuu ndio ukubwa huo.
 
@jembapoli unajua wako pamoja kwa huu mwezi mtukufu tuuu ila kila mtu yuko na nyumba yake na mahitaji yake
 
Nasikia Babu Tale yule Manager wa Tip Top Connection naye anaongeza mke wa pili, tena mke wa kwanza katoa ruhusa bila shida.

Unaweza kumcheki akupe mbinu, maana kujifunza kwa wengine ni muhimu sana.
 
kuliko kuwa na mke mwenza bora niendelee kuruka magoma mtaani aisee.
 
Kuliko kuwa Mke mwenza afadhali kuwa mjane, kweli wahenga hawakukosea
 
Mie nakushauri ule mke wa tatu. Hii itatatua shida zote manake hawezi kuwa na wivu na wanawake wawili kwa mpigo.
Ramadhan Kareem baba.
 
Mi nimeipenda hii lugha na uandishi uliotumika hapa. Ukisoma unaona ustaarabu na busara flani hivi.

Mengine yamenizidi. Nikutakie tu kila la kheri.
 
Nenda kwa kiongozi wako wa kiroho kuomba ushauri zaidi namna ya kuishi na wake 2 unaweza pata mwanga zaidi
 
Binadamu ana roho mbaya ndomana akifa ananuka mnoooo.

Sasa wivu wa nin kwa mwenzake?
 
Subirini Ramadhan ipite uone kama ataendelea na tabia Hiyo mana kwa sasa si wanapika mji mmoja na muda mwingi wanakua pamoja..akiendelea itabidi ukae na kiongozi wa dini apate somo mana ana husuda na wivu ndo vinavyomsumbua
 
Back
Top Bottom