Mkuu, natanguliza plole na samahani kwa mawazo yangu.
Kwanza kabisa, mtu akikwambia sikutaki, muelewe.Si ni mtu mzima? Hata ukibembeleza sawa atakaa lakini wazo lake halitoki kichwani.
Pili, amini usiamini hata wewe umechangia hali hiyo. Ni vigumu mwanamke umletee mwenzie.Atanyamaza lakini moyoni atakuwa anaumia.Af pia, umesema mmepata watoto wawili! Mbona wengine hata mmoja hawapati na wanakaa! Hii inaonyesha wewe umemtafuta mke wa kukuzalia tu hana umhimu mwingine katika maisha yako! Mwanamke ukimdhalilisha ni kweli utajuta kuzaliwa! Haya ni mambo ambayo mlitakiwa muwekane sawa. Ila kiukweli utambue hata kama dini inaruhusu wanawake wote duniani hawezi kulidhia uongeze mke mwingine. Je, ingelikuwa wewe ndo huzai, akasema akatafute mwanaume mwingine muwe wawili ungefanyaje! Wanaume tukumbuke kwamba maumivu yetu yako sawa na ya wenzetu