Watu wengine huwa wanapenda kuleta challenge kwenye kila suala wala udishangae.Mkuu sio mbaya nikileta hapa na kipata ishauri kwani hakuna anayenijua mm wala mke wangu sasa nashangaa wanaosema namdharilisha mke wangu wakati hakuna anaye nijua mm wala mke wangu wala familia yangu...
Lakini kwa uelewa wangu wanawake wengi siku hamu yao ya tendo la ndoa inaathiriwa na vitu vingi, mfano baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinapunguza hamu ya tendo la ndoa. Sababu nyingine ni ile ya ujauzito, baadhi ya wanawake huwa na tabia za ajabu kama vile kumpenda sana mumewe au mtu fulani, au kumchukia sana mumewe au mtu fulani, si kwa kupenda lkn inatokea tu na hali hiyo inakuwa nje ya uwezo wao.
Ile sababu ya kuwa labda kapata dume jingine siwezi kusema ni kweli au sio kweli. Maana yote yanawezekana. Wanawake wazinzi wapo na wanaume wazinzi wapo pia (hivyo chunguza kama ni kweli utagundua tu).
Lkn kukunyima tendo la ndoa si lazima awe kapata mwamamume mwingine inaweza kutokea kwa sababu nyingi baadhi kama nilivyoeleza hapo juu.
Lkn ilitakiwa akueleze kabla ya kukunyima, atoe sababu ya msingi kwa nini akunyime? Isiwe sababu ya kujua yeye tu!!!!! Hapo lazima hata mimi nitaona sio kitu cha kawaida.
Kuleta uzi huu humu sio kosa, maana wengine wanadhani wanajua kila kitu, lkn kutafuta ushauri ni busara zaidi kuliko kujifanya hauhitaji ushauri halafu ukafanya maamuzi mabaya peke yako.