Mke wangu anajihusisha na mambo ya ushirikina! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wangu anajihusisha na mambo ya ushirikina!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtego wa Noti, Dec 28, 2011.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Wahenga wanasema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni....!!!

  Rafiki yangu wa karibu sana jana kidogo agongwe na magari baada ya kumfuatilia mke wake kwa umakini zaidi na kugundua kuwa mkewe anahusudu sana na anashiriki katika mambo ya kishirikina. Kwa sababu mke wake huyo anafahamu kuwa mumewe hapendi haya mambo ya kishirikina, basi ilibidi ayafanye kwa tahadhari sana ili kuhakikisha kuwa mume wake hafahamu kinachoendelea.

  Mumewe alikuwa anahisi kuwa mkewe anashiriki ktk mambo hayo. Mambo yalikuja kuharibika pale mumewe alipomtegea vitu vya kunasa sauti katika maeneo ya nyumbani na maeneo ambayo mkewe anafanyia kazi zake na kushitushwa na mawasiliano ya kulipana pesa baina yake na mganga wake huyo.
  Baada ya mumewe kugundua hivyo na kupata ushahidi wa sauti, mkewe alijitetea kuwa anajilinda mwenyewe na anashughulikia afya yake na kuwa eti hana mpango wa kumdhuru yeye.

  Anasema mkewe baada ya kuona ishu imevuja kaomba msamaha na kuahidi kuwa hatafanya tena upuuzi huo. Mume anasema haamini maneno hayo, anadai labda mkewe anasema hivyo ili kujipanga zaidi na kuhakikisha kuwa nyendo zake hazivuji tena.
  Sasa jana rafiki yangu huyo kaja povu likiwa linamtoka akisema kesha mzaba mkewe vibao kadhaa na anafikiria kuachana naye. Kaniomba ushauri afanye nini maana keshachanganyikiwa baada ya kugundua kuwa mkewe amekuwa akifanya mambo hayo behind the door!
  Kaja kuniomba ushauri na mimi nikaona sio vibaya nikaliweka hapa jamvini ili watu waweze kunisaidia kumshauri rafiki yangu katika kipindi hiki kigumu!
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Mh pole yake.
  Ampleleke kwenye maombi.
   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  yaani ndani ya nyumba anasema amani haipo tena baada ya kugundua hizio takataka...maombi ni jambo jema sana ila sijui kama atakubali.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Si achunguze kwanza ajue mkewe anaenda kwa mganga kwa ajili ya nini! Kama ni maradhi yake mwenyewe amweleweshe tu kuwa hospital yanatibika: kama anahofia kibarua, amueleweshe tu kuwa hard working na ufanisi vinalipa, kama ni mapenzi basi amuhakikishie kwa vitendo kuwa anampenda bila msaada wa ndumba.
  Kifupi amweleweshe tu mkewe kuwa mganga wake anamlia pesa za bure, uwezo wa kila akitakacho uko mikononi mwake.
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana maana umeongea kitu cha msingi mno!....inavyoonekana mkewe huenda kwenye hayo mambo kwa ajili ya afya yake...actually it is a wastage of money and uaminifu kwa mumewe...
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Kwa nini mnapenda kutumia neno rafiki yangu, badala ya ninyi wenyewe? hao rafiki zenu ni kwa nini msiwashauri wawe member wa JF? nahisi udanganyifu mtupu kuwatumia third part kwa karibu kila thread.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  ukimkaribisha shetani ndani ya nyumba hutakaa uijue amani.
  Piga chini fasta, atakuja kuombwa hata sadaka ya mtoto au mumewe.
  Si mke huyo!!!
   
 8. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  unalosema ni kweli kabisa. siwezi kuacha kutumia third part kama ishu inamhusu third part, ingekuwa inanihusu nisingehangaika kuweka third part...hii ni kwa sababu humu jf hatutumii majina halisi kwa hiyo hata kama nikisema ni ishu yangu huwezi kunfahamu/kunitambua.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Superstitious goat.

  With wives like these, who needs marriage?
   
 10. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Sio lazima aombewe kwingine, kama ana imani juu ya maombi mwambie amwombee yeye mwenyewe.
   
 11. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Halafu kajichanganya kichwa kinasema ''mke wangu'' stori- mke wa rafiki yangu...........kwa vile hujiamni huwezi kusema hili ni tatizo langu- huenda mkeo anaenda kwa waganga kutafuta dawa ya kukufanya ujiamini zaidi................
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kumpiga chini sio suluhisho maana anaweza kumpiga chini huyo baadaye akapata mke mwenye matatizo kuliko hayo. Kwahiyo mwambie ayamalize kwa busara.
   
 13. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  naungana na wewe kwa huo ushauri, hata mm nilimwambia ivoivo....asante kwa kukazia uzi
   
 14. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  sijajichanganya mkuu...ila nimesahau kuweka alam za funga na fungua semi kuonesha kuwa kaongea hayo maneno mtu mwigine/yaani naandika kwa niaba!!!
   
 15. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Wala usiache Mwanamke Mchawi aishi..................................kwahiyo mhurumie kwa kumuachia uhai wake ila mpige chini (achana naye).............uchawi ni roho hawezi kuacha kwa kusemwa au maonyo, watu wengi wanapenda kuacha uchawi, lakini shughuli namna ya kutoa hizo roho. Kama unampenda na hutaki kumuacha mpeleke kanisani afanyiwe maombi ya kuondoa roho chafu, mikataba, na uchawi na pia aonyeshe vitu vyote alivyowahi kupewa na mganga na sehemu alizowahi kuviweka ili navyo viombewe na kuchomwa moto.........
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi nachanganya mambo hapa! Mtoa mada umezungumzia ushirikina lakini hujawa muwazi zaidi huyo mmama anakwenda kwa mganga wa aina gani? Anakwenda kuloga au kuaguliwa? Maana nadhani kuna waganga wa uchawi na wale wa jadi (dawa za asili) which is which now?
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huyo mwanamke ni hatari kuliko AK47!!

  Ingawa siamini mambo ya uchawi, ila mtu yeyote anayeyaamini si rahisi kubadilika...

  Inabidi hapa muhusika aangalie possible solutions zote ana achague iliyo rahisi kwake...Ambazo ni ama kuungana na mke wake na wote wakawa wanga, kukubali kuishi na mchawi na kila mtu akaendelea na mambo yake au kupeana uhuru ili kila mmoja aendelee kuabudu Mungu/Miungu wake......Sijui kama naweza kupata alternative nyingine!

  Babu DC!
   
 18. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Je huyo rafiki yako anaamini uchawi unadhuru bila mungu? Kama anaamini basi hana makosa mke wake....kama rafiki yako haamini uchawi basi huyo mwanamke ana makosa...swali moja tu wewe ni muislam au mkristo-mana kitabu cha kiislamu kinasema uchawi upo lakini wanao amini uchawi wamekufuru-na mwenye kukufuru basi hajamuogopa mungu kwa hio hawezi kumuogopa mme wake.

  Hapo ni talaka naziona kwa mbali....:lol:
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna mambo! Mie ni Dadaake mke wangu, binti wa miaka thelathini na kidogo lakini habari zake si nzuri! Jana kanisimulia mambo ambayo sikupaswa hata kuyasikia na sikuamini kuwa ni mshirikina kiasi hicho! Kwa bahati mbaya sitaweza kueleza story yenyewe kwa sasa ila niliishia kuamini tu kuwa MAOMBI yana nguvu hata kama unasali kwa mazoea tu! maana ali-confess mbele yangu kuwa wamenishindwa!! so hata hili nalo laweza kuwa kweli, ntaanzisha thread nikiwa na computer nielezee kwa mtindo wa "rafiki yangu"
   
 20. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mtu habadiliki tabia fasta hivyo....ataendelea kuwa witchdoctor tu.....tahadhari,chukua hatua
   
Loading...