'parapanda italia parapanda...parapanda italia parapanda...hiyo parapanda.....'
Ndugu angalia usije imbiwa huo wimbo aisee! Huyo hakupendi kama angekupenda angekulinda. Angekwambia ukweli kabla hamjaoana.
Ila Mungu ni mwema...amekulinda kwa muda wote huo. Sasa vile umejua basi huenda ulinzi wa Mungu kwako ukakoma maana sasa Mungu atakuacha uamue mwenyewe...kujiponya au kufa!
Unaweza kujilala kitandani ukazinduka kumbe umemlalia nyoka. Ni Mungu amekuponya! Sasa ukiamua kuendelea kulala na nyoka wakati tayari umemuona eti Mungu ataendelea kukulinda...pole,...utakuwa unamjaribu Mungu!