Habari za weekend wanajamvi,
Nimepangiwa kusimamia kazi fulani njiani Arusha kwa muda wa miezi 10. Ili kupunguza gharama nimeona ni vyema nikapanga nyumba badala ya kuishi hotelini. Nimemwambia mke wangu kuwa nafikiria kutafuta msichana wa kazi kwa kuja mchana na kuondoka jioni. Kazi zake zitakuwa ni kupika na usafi.
Mke wangu hajahafiki kwa madai kuwa wasichana wengi wako desperate kupata wanaume na hasa ndoa hivyo nitakuwa nahatarisha ndoa yetu. Anadai mabinti wanaweza kufanya chochote na hasa kwenye chakula nikaja kujuta.Anadai nijipikilishe na kama siwezi nile hotelini. Kuhusu usafi wa ndani na kufua anadai nifanye tu mwenyewe.
Jambo ambalo naona ni gumu sana. Nimemwambia naweza kumtumia mchungaji wetu ambaye amehamia Arusha miezi kadhaa iliyopita anitafutie msichana anayejiheshimu ndani ya kanisa lakini bado hataki.
Mke wangu ana hoja au ni fear of the unknown?
Ushauri wenu wanajamvi