Mke wangu amekiri kunisaliti

Mke wangu amekiri kunisaliti

hizi stori za kusomesha then kuja kugongewa mbona zimekuwa nyingi?
 
du, aisee pole sana, nashindwa hata kukushauri nikushauri vipi. mwombe Mungu akupe njia ila kibinadamu ni ngumu sana.
 
Unamsomeshe mwanamke wa nini, yeye bada mbichi kakutana na masharo chuoni wamegaragaza mbaya mpaka anakuletea magono! Hapo bado ngoma tu, ukitaka usalama aache chuo afate kazi moja ya ndoa basi.
 
Kosea mengine yote, omba sana usikosee kuoa!!

Ulikuwa na nia njema but ye mwenyewe kajiharibia!! Alifuata mkumbo wa kampani za vyuoni, kama utataka aendelee kujiendeleza mpeleke katika vyuo vinavyotoa elimu kwa njia ambayo itamfanya awe nyumbani!! Mfano distance learning au evening, msamehe then mfuatilie kwa ukaribu!! Pengine kampani za chuo zilimpeleka vibaya

Kosa si kutenda kosa bali kurudia kosa!!
 
Pole sana najua kusamehe si kitu rahisi lakini jitahidi Mungu akusaidie hasa ukitilia maanani mna mtoto. Kusamehe unaweza ila hutasahau.
 
Msimpoteze, ye kashaoa, majukumu yote kuhusu mkewe ni yake na kwa pamoja wanaweza kushauriana ila tu wanwake wapo tofauti,..ndugu,pole kwa maumivu ya moyo..kwani kazi anaenda mbali?hapa inabidi kupanda mzizi wa uaminifu tena,kwa ninavyoona, cause msipofanya hivyo mtaanza kugombana soon..pole
 
Mkeo ameruka stage. Ulimuoa akiwa mdogo yale maisha ya kutoka kidato cha nne mpaka chuo kayaruka ameyapata akiwa kwamume hivyo uwezekano wa kuyarudia ni mkubwa. Na hapo ni hatari maana anakuwa ndoani.
 
Pole sana mkuu. Inauma sana pale wewe unapojilinda na kumlinda mwenzio lakini yeye akaenda kufanya kinyume chake.

Jipe mda utapoa na kusahau, kwa kuwa natumai mkeo kama ni mwelewa amejua kwamba amekukosea na ana deni kwako.
 
Pole sana mtoa mada,,muombe Mungu ndio muweza wa yote
 
Huyo bado anakula ujana kaolewa bado mdogo sana na hawezi kuacha kuchepuka. Na aliolewa na we we baada ya kuwa hana options. Hakupendi huyo anakutumia tu na lazma aje akuache.
Pole sana the more anavosoma ndo mapenzi yatakavozidi kuisha.
 
Kosea mengine yote, omba sana usikosee kuoa!!

Ulikuwa na nia njema but ye mwenyewe kajiharibia!! Alifuata mkumbo wa kampani za vyuoni, kama utataka aendelee kujiendeleza mpeleke katika vyuo vinavyotoa elimu kwa njia ambayo itamfanya awe nyumbani!! Mfano distance learning au evening, msamehe then mfuatilie kwa ukaribu!! Pengine kampani za chuo zilimpeleka vibaya

Kosa si kutenda kosa bali kurudia kosa!!
Asante
 
"Akakiri alichepuka nae mara tatu"
Shenzy type yaani mimi wakati anamaliza kusema hiyo nilichepuka atajikuta virago vyake vipo nje vinagaragara...vijana tunaoowa miaka hii tuwe makini ndugu'zanguni wanawake(sio wote)wengi wamekuwa na tamaa za kijinga we mtu umeacha mme nyumbani unaenda mvulia mwingine ch*pi hata hujiulizi,imefikia mpaka kuleta magonjwa nyumbani kwa mmeo inaonyesha ni jinsi gani alivyo hopeless hata msimamo kwamba mchepuko uvae condom hana!!!!!shit me nitaondoka na shingo yaani nimetulia mwanamke aniletee gono ndani,labda aongee lugha ya malaika ndo nitamwelewa.
 
Huyo bado anakula ujana kaolewa bado mdogo sana na hawezi kuacha kuchepuka. Na aliolewa na we we baada ya kuwa hana options. Hakupendi huyo anakutumia tu na lazma aje akuache.
Pole sana the more anavosoma ndo mapenzi yatakavozidi kuisha.

Ukweli unaouma lazima usemwe.....

Namwonea huruma mme wa mtu.
 
Nawe ulikuwa anam-bajua beki tatu nyumbani.
 
Mwadada84

Msamehe ndugu!
Mpe nafasi nyingine, akipata kazi mbali na hapo, weka misimamo yako kwa unavyomfaham, atakaa sawa tu!! Poleeee
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom