Mke wangu amebadilika sana

Mke wangu amebadilika sana

Choosen85

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,190
Reaction score
5,045
Mke wangu nimeishi naye wastani wa miaka 4 sasa alikuwa mnyenyekevu, mpole, si muongeaji sana hata akiwa na wenzie, heshima kwangu ni miongon mwa vitu nilijivunia kuishi naye, kuniskiliza na hakuwa mtu wa kujibizana na mimi.

Sasa ameanza kunijbu majibu ya mkato na wakati mwingine naweza mkemea jambo fulani akatoka nje huku anabamiza milango kavuta mdomo sjawahi kumpiga maana siamini katika kupiga mwanamke, nimejikuta natafakari mambo mengi sana maana nilimpa mtaji wa biashara pengine huko kwenye biashara yake amekutana na watu wamempa kiburi na kumfundisha tabia ngeni kwangu ukizingatia hata sex yenyewe siku hizi ni kama anakwepa tofauti na kipindi cha nyuma alikuwa anapenda sana hilo tendo au vihela anavyopata vinampa kiburi sielewi.

Juzi niliamua kwamba asifanye jambo lolote linalonihusu yaani asifue nguo zangu nitafua mwenyewe, asinipikie nikitoka kazini napika mwenyewe, sihitaji k yake tena na wala staki story nae. Kabaki amenuna tu na mi sina habari.

JE WAKUU NIMEAMUA VEMA AU NIFANYE NINI?

---------

Wakuu kheri ya 9D kwa wapigania haki wote wa TANGANYIKA.
 
eti ulimpa mtaji wa biashara aji komboe, yesuu 🤔.

Mzee unge anzisha biashara, kisha yeye awe kama mwajiriwa aki zingua ni kutimua.

Hapo asha kutana na wa level zake, we kunguni uta mwambia nini 😂 😁

Kuna Boss wangu mkinga aliniiambia ukipata mwanamke Bomu ni shida Sana, hakuna sehemu utafika.
Alisema wao kwenye ukoo wao wote mwanamke haruhusiwi kukaa nyumbani tu kama Kwa siku wewe kama baba hauingizi 600k kama faida, 🤣 lazima na yeye awe na jambo la kufanya (na mara nyingi wanafanikiwa)
Sasa hapo ni umepata mwanamke mwenye Akili, Hawa wenzetu ukimfungulia biashara, ni either biashara ife au ufanikiwe akuone mume haufai.
 
1. Huyo ni mkeo siyo mchepuko, muite ukae naye, ongea naye tena kwa unyenyekevu sana ujue kuna tatzo gani, yawezekana kasikia jambo kukuhusu.
2. Mpe nafasi ya kujieleza, usiwe mbabe
3. Jaribu kumdadisi kuhusu biashara zake kama kuna heri
4. Jaribu kuchunguza marafiki zake wa karibu
5. Usitengeneze taharuki sana kwa kumkatisha majukumu ambayo anatakiwa akufanyie.
6. Jaribu kumletea vizawadi mara kwa mara.

7. Kubwa zaidi:
MSAMEHE MADHAIFU YAKE, NA MUOMBEE KWA IMANI YAKO ILI NDOA YENU IFANYIKE KUWA BARAKA.

8. yakizidi sana itisha kikao cha wazazi pande mbili (kwako na kwake), hapo usimuite mchungaji wala padr wala shekhe maana hao wote wana mambo yao ya kikuda sana'
 
Nenda ukashinde wiki nzima kwa biashara yake, umsaidie kuwepo bila kusema wewe nani yake. Leta mrejesho Acha kuumiza kichwa..baada siku zingine nenda kwa kushitukiza.. utamjua tu mwenzako/wenzako

Rudi kuwa kama kawaida.. yaani bwegwe kama boyaaaa.. pole na kila la kheri.. vizuri usimpige..
 
Back
Top Bottom