Mke wa rafiki yangu;

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
3,134
3,579
Habari za wakati huu wana Jf
Ebwana leo nimekuja na kisa cha ukweli kabisa ambapo at the end mtanipa ushauri nini cha kufanya kama hamtajali!

Rafiki yangu mmoja jina (kapuni) maarufu sana hapa town alifanikiwa kuoa kitoko kimoja matata sana bellow 25 kutoka singapore ya tz (Singida)
Kama mnavyojua watoto wa Singapori rangi za mtume ukizingatia na umri huo mtoto anaita yaani mashaalah ila jamaa angu ni above 40!

Ndoa yao baada mwaka mmoja mambo yalianza kubadili mke akazoea jiji la Bashite na kuanza kutamani vijana wenzake, miezi kama mitatu iliyopita yule binti alikutwa na sms za boyfriends zake akaulizwa basi anasema "Sikutaki naomba talaka yangu sikupendi" yani baada ya ndoa ndo sikupendi huh haya bana!

Kwa kauli hiyo ikawa ugomvi mzito hawakulala kesho mume akaenda kazini mke akaita canter na kubeba kila kitu ndani na kutokomea kusikojulikana msichana wake wa ndani akampigia simu mume akafika but it was too late kwani walishaondoka ikabidi tuhoji kuwa apart from driver alikuja na nani kuchukua msichana wa ndani akasema kuna kijana mmoja sharobaro suruali kata K ndo alikuwa naye anamwambia bby usijali "heri lawama kuliko fedhea".


Hatukuishia hapo ikabidi tuende ktk mamlaka zinazohusika kutoa taarifa pamoja na companies za simu kuangalia alikuwa anawasiliana na nani na wapo wapi kwa kutumia GPRS tuligundua wapo chamanzi na kesho yake tukafatilia tena na kugundua kuwa kashatoka nje ya mkoa, mchana wake mama yake kutoka Singida akasema kuwa ameshafika Singida!

Jioni hiyohiyo jamaa akachoma mafuta kwenda Singida kwa makubaliano yangu mimi na yeye kuwa akampe talaka yake huko huko kwa wazazi wao pia aiwahi hela yake kabla ya ya kuichange kwani ilikuwa zaidi ya dola elfu tano!

Jamaa baada ya kufika Singida siakaomba wapatanishwe huku anajua kuwa mke anamcheat na tulishathibitisha hilo basi baada ya siku tatu nashangaa wanarudi tena duh!


Jamaa kwa aibu akaanza kujisemesha "ndoa kuoa rahisi ila kuivunja kazi" ni kweli ila sio kwa vituko mkewe anavyomfanyia mana siku nyingine anarudi saa nane usiku akiulizwa anasema nilikuwa kwa mpenzi wangu!!

Week tatu zilizopita mke karudi asubuhi kaulizwa kajibu "embu niache nile ujana wangu usinizeeshe"

Mke anadai talaka mume hataki ikabidi ndg wa mume waingilie jamaa atoe talaka na hilo likafanikiwa cha kushangaza yule binti juzi kushinda jana kaolewa tena jamaa eti kaumia!!

Nishaurini nimshauri nini rafiki yangu huyu juu ya hili.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwani jamaa hataki mitara..?? Mwambie wakaolewe wote tu hukohuko..,,, Akachumbiwe tu na yeye..

Si kashindwa kuwa mume , uke wenza atauweza hakika.,, !!

Wanaume wa dar tutawatunuku nishani za uzumbukuku ...!!
 
huna cha kumshauri sababu jamaa yako anampenda sana huyo mkewe

muache akichoka ataachana nae ugonjwa wa mapenzi mbaya sana unaweza mshauri tena mwisho wa siku watarudiana tena
 
Umshauri nini sasa na binti kashakula talaka zake.


Cha kufanya kaa naye karibu asije kugeuka kichaa tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hapo tatizo ni kwamba kuna mmoja kaanza mapenzi ukubwani halafu kuna mwingine kiasili kwa mkoa anaotokea huwa wanakua siyo wachoyo (siyo wote, ila huyu ni kundi la wasio wachoyo)
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Embu tuma picha ya huyo mkewe tumthamimishe....... Maana hii habari bila picha ya huyo Mwanamke haitonoga.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hahahaha daaah uyo jamaa yako ni fala miaka 40 na bado anaumia kisa mapenzi daaaah ama kweli dunia inamambo

mwambie ivii uyo mwanamke anae mlilia ndo atamuondoa duniani alafu mkumbushe kuhusu pressure na kisukari mwambie viko karibu sana na yeye akiendelea na undezi wake wa kulilia mapenzi
 
Huyo mwanamke hajitambui na aliyemuoa ajiandae kisaikolojia maana naye yatamkumba kama ya jamaa yako.
 
Dah! Ni bora kuzaliwa Faru John ngorongoro kuliko kuzaliwa Mwanaume BOYA mjini Dar es salaam.
 
Vip dollar 5000 na kenta lilobeba vitu vyote ndani lilivirudisha?

Hajarudishiwa hela aliongopa eti ameibiwa ubungo na baadhi ya material kama flat screen vilipelekwa Singapore vingine vilitokomea kusikojulikana eti jamaa akayafumbia macho duh!

Mungu aniepushie kwani ingekuwa mimi now nipo segerea.
 
Back
Top Bottom