Mke wa Professor! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Professor!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,414
  Likes Received: 5,684
  Trophy Points: 280
  Mke wa Professor!  [​IMG]John ni professor katika chuo kikuu kimoja nchini Canada.
  Huandika papers za nguvu, na kutoa lectures zenye heavy stuff na hutumia muda mwingi sana library.
  Mke wake ambaye anaitwa Linda anampenda sana mume wake ingawa kimadarasa wapo tofauti sana ni kama mlima kilimanjaro na kichuguu.

  Linda anapenda sana kuwa karibu na mume wake John tatizo utaongea kitu gani na Professor mwenye uelewa wa juu kiasi hicho?

  Linda akafika mahali akajiuliza itakuwaje maisha kama haya ambayo mke na mume hawana kitu cha kuongea pamoja?

  Baada ya kutafakari kwa umakini sana akagundua kwamba mume wake anaandaa paper inayohusu ndege (birds) na kwa kuwa hata yeye anawafanya ndege akaona ndiyo mwanya pekee wa kuunganishwa na mumewe.

  Linda akaenda kununua vitabu vinavyohusu ndege, na akamuomba mumewe wahudhurie semina na kitu chochote kinachohusu ndege na ikajibu kwani hata mumewe akawa anapenda sana kuhusu ndege na wamekuwa sasa wanafanya hata vacation mahali ambapo wanaweza kwenda kuangalia ndege (bird watching)

  Ni miaka 20 sasa wanafanya kitu kimoja na kufurahi pamoja. Linda hajui lectures ambazo mumme wake hutoa chuo na pia hajui kozi gani anafundisha ila anajua kitu kimoja tu kwamba yeye na mumewe linapokuja suala la ndege huongea pamoja na kuwaunganisha pamoja kama wanandoa.

  Kuna usemi kwamba hobbies ni kitu kinachowaleta wanandoa pamoja na ni kitu kizuri mno.
  Inawezekana mumeo ana interest na kitu fulani na kupitia hicho kitu ukiungana naye unaweza kumleta karibu zaidi katika maisha yako kuliko unavyopingana naye.

  Jambo la msingi ni kuhakikisha hicho kitu si dhambi.
  Kama mumeo ni mlevi wa kutupwa kuungana naye ni kujimaliza mwenyewe!


   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  nzuri sana..
  nimeipenda
   
 3. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa hawa mabinti wa bongo, labda uanze stori za twanga pepeta au ni mwanamuziki yupi kaachika... bila hivyo mtaangaliana, wewe ukinywa bia yako ya kawaida ya kili nae akiruka kutoka heineken kwenda wine ili akukomoe
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Soulbrother,
  Spot on.....halafu kuna hii kinywaji Savannah...naichukia sana imagine inauzwa TZS 3,500 per kabottle...halafu mtu natumia half of it kusuuzia glass...argh!!!! na warembo wote siku hizi wako nayo...no more KILI,NDOVU,SAFARI...
   
 5. A

  AM_07 Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kweli akina dada wengine (sio wote) wanaboa ukiwa toa out, mwanaume unakata serengeti ya elfu mia tano yeye anakamata savanah worse enough ya kwanza nusu anasuzia glass ya pili anaacha nusu anakwambia " am ok" kama tahira vile,
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  jamani nimecheka mpaka bac...haaa sasa c muwe mnawaambia mna hela ya tusker tu....kwanini mtu upate shida hivyo na pesa yako? utafute kwa shida u2mie kwa shida....lol
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  lakini sasa na nyie mnataka kuwazuia kunywa wanachotaka kisa mnasema ya ghali, mnawaenekeza tu kwanini cku ukiwa huna pesa ya kumnunulia hiyo ya ghali ucmwambie leo mfuko umetoboka nina ya Eagle tu?....mnayataka wenyewe kwa kujiona kila cku muwaonyeshe warembo wenu mpo juu.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  So whats your comment on this..Watu wanapokuwa na tofauti kubwa ya kielimu, what do you think is the fate?
  Pals, let alone the tusker-thing, say something on the pertinent issue above!

  Distortion at its power

  Wht i want to say is that hii hali inatokea sana. Mi nishawahi ona jamaa ana mke, ambapo wageni na marafiki wa jamaa wakija, mke anajificha chumbani, kisa hawezi kuchangia chochote katika maongezi.

  HATA KUTOKA NAE OUTING INAKUWA tabu kabisa..

  Lakini really you have tought us a very good plan to combat such kind of a situation...Naikubali njia hiyo, and i think its practicable!
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  yani cna mbavu kabisa......nimecheka mpaka nimesahau shida zangu....jamani mnateseka kweli.
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hii story iko upande mmoja tu vipi na kwa kina baba nao, nadhani mapenzi ni wote kufahamiana na wote kukubali kushare hobbies za kila mtu, maana wasiwasi wangu ni kuwa mtu mmoja anaweza kujiforce kufuata hobbies za mtu mwingine na mwisho wa siku likawa ni penzi la upande mmoja tu
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Wht i want to say is that hii hali inatokea sana. Mi nishawahi ona jamaa ana mke, ambapo wageni na marafiki wa jamaa wakija, mke anajificha chumbani, kisa hawezi kuchangia chochote katika maongezi.

  HATA KUTOKA NAE OUTING INAKUWA tabu kabisa..

  Lakini really you have tought us a very good plan to combat such kind of a situation...Naikubali njia hiyo, and i think its practicable!


  na huyo jamaa ana kubaliana na hiyo ctuation ya mkewe, kwanini acmchangamshe kwa hili, sasa atafanya hivyo mpaka lini kwani hawezi kukaa hapo akawackiliza tu japo atajifunza pole2 kuliko hiyo njia wanayoifanya sasa?
   
 12. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa mtazamo wangu huyu Prof hakuwa anamtendea haki huyo mkewe. Alipaswa ajishushe!! Amekuwa akijua siku zooote kuwa mkewe ana elimu ya kiwango cha chini na akaamua kuwa naye na maendeleo yooote mpaka akawa prof yuko naye. Kwa vyovyote vile alikuwa anajua ni nini kiliwaunganisha, na bado kinawaunganisha, sasa km mama amejikuta anakuwa lonely mpaka kaamua kuwapenda ndege duh!!!...
   
 13. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mi uwa najiuliza sana, hivi wake na waume hao wakati wa urafiki na uchumba kabla ya ndoa walikuwa wanaishije/wanaongea nini?
   
 14. S

  Stone Town Senior Member

  #14
  Nov 26, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii story nimeipenda sana ila nadhani kuna kitu kimesahaulika kidogo katika mapenzi hakuna mmoja kuwa juu na mwengine kuwa chini yaani hata kama mtu mbumbumbu kiasi gani wewe huwezi kumuona hivyo kwa kuwa wakati mwengine mtu aliyekuwa hajasoma anaweza akakupa muongozo wewe mwenye elimu ukashangaa.

  ni vizuri kufahamishana tu na sio mwengine akimbie chumbani huko ni kujinyima uhuru wa kuongea na kusikia ukijificha utajifunza wapi? utajua lini? utapata uzoefu wapi na lini? lazima ujiamini na hakuna kukata tamaa kutokusoma kusitoe fursa ya wewe kudhalilika na kujidhalilisha maana unapojidhalilisha mwenyewe hakuna atakayeweza kukuinua lazima mwenyewe ujipe moyo wa kuweza na kuonesha uwezo wako.

  hujasoma shuleni basi hata uzoefu wa mitaani huna? haiwezekani kwa maisha ya sasa mbona elimu haipatikani shule tu?
   
Loading...