kisasangwe
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 292
- 52
Ni rafiki yetu wa familia. Tulifahamiana tangu high school. Amekua na mahusiano na msichana mmoja ambae baadae alikuja kugundua kua anatoka na baba paroko.amejengewa nyumba pia
Wakiwa chuo kikuu kimoja huko jijini wanakopatikana masangara, rafikiangu huyu alijaribu kumsihi mpenziwe huyu aachane na padri ikiwa kweli alikua tayari kuwa nae kwa rest of maisha yake. Binti alikua anamdanganya mara kwa mara kua ameachana na padri lakini jamaa akaja kuwabamba live room kwa huyo dada. Lilizuka vurugu kiasi kua padri alimtishia jamaa maisha ( hata kimasomo kwani mtumishi huyu ni mdosi katika chuo walichokua wanasoma) yeye hakutaka kumtosa binti kwa madai kua alimpenda sana ingawa tulimshauri aachane nae.
Baada ya muda sasa wamemaliza chuo na kijana kwa mapenzi mema alimtambulisha binti kwa baadhi ya ndugu ikiwemo mama yake mzazi ambae alimpenda sana huyo mkwe. Ila kijana hakuwahi kumwambia mamake tabia ya huyo mpenziwe,akidhani atarekebika.
Dada juzijuzi akadai anakitumbo ndii (haijulikani kama ni padri au jamaa) akademand kutoka kwa kijana kua aende kumtambulisha ili maandalizi ya ndoa yafanywe, kijana alikubali ila kwa masharti kua anataka binti amthibitishie kua hana tena mahusiano na baba paroko.bint akadai kua angempigia simu wakiwa pamoja ili athibitishe lakini siku ilipofika hakukubali kupiga simu. Kijana akampa live kua hapo ndo mwisho wa mapenzi yao.
Binti kwa kujua kua mama mkwe anamfagilia akakimbilia kwa mama kumtaka amsaidie ili mwanae amkubali tena. Kijana akaona isiwe tabu akamsimulia mamake kila uozo wa binti kitu ambacho kiliamsha hasira ya mama. Hataki hata kumsikia na binti kwa kujua hilo juzi kaumwa ghafla na sasa kalazwa hospitali hoi. Baadhi ya ndugu wa dada wanamsihi jamaa amsamehe, sisi kama marafiki tumemsihi amsahau maana mara nyingi hawa watu wanaokua na mapadri huwa hata waolewe huwa wanaendeleza hayo mahusiano.
Kachanganyikiwa hajui afanyeje, wanajamii hebu nipeni ushauri wenu kuhusu huyu ndugu maana msimamo wake naona hauna mashiko.