Mke wa Padri

kisasangwe

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
292
52
Ni rafiki yetu wa familia. Tulifahamiana tangu high school. Amekua na mahusiano na msichana mmoja ambae baadae alikuja kugundua kua anatoka na baba paroko.amejengewa nyumba pia

Wakiwa chuo kikuu kimoja huko jijini wanakopatikana masangara, rafikiangu huyu alijaribu kumsihi mpenziwe huyu aachane na padri ikiwa kweli alikua tayari kuwa nae kwa rest of maisha yake. Binti alikua anamdanganya mara kwa mara kua ameachana na padri lakini jamaa akaja kuwabamba live room kwa huyo dada. Lilizuka vurugu kiasi kua padri alimtishia jamaa maisha ( hata kimasomo kwani mtumishi huyu ni mdosi katika chuo walichokua wanasoma) yeye hakutaka kumtosa binti kwa madai kua alimpenda sana ingawa tulimshauri aachane nae.

Baada ya muda sasa wamemaliza chuo na kijana kwa mapenzi mema alimtambulisha binti kwa baadhi ya ndugu ikiwemo mama yake mzazi ambae alimpenda sana huyo mkwe. Ila kijana hakuwahi kumwambia mamake tabia ya huyo mpenziwe,akidhani atarekebika.

Dada juzijuzi akadai anakitumbo ndii (haijulikani kama ni padri au jamaa) akademand kutoka kwa kijana kua aende kumtambulisha ili maandalizi ya ndoa yafanywe, kijana alikubali ila kwa masharti kua anataka binti amthibitishie kua hana tena mahusiano na baba paroko.bint akadai kua angempigia simu wakiwa pamoja ili athibitishe lakini siku ilipofika hakukubali kupiga simu. Kijana akampa live kua hapo ndo mwisho wa mapenzi yao.

Binti kwa kujua kua mama mkwe anamfagilia akakimbilia kwa mama kumtaka amsaidie ili mwanae amkubali tena. Kijana akaona isiwe tabu akamsimulia mamake kila uozo wa binti kitu ambacho kiliamsha hasira ya mama. Hataki hata kumsikia na binti kwa kujua hilo juzi kaumwa ghafla na sasa kalazwa hospitali hoi. Baadhi ya ndugu wa dada wanamsihi jamaa amsamehe, sisi kama marafiki tumemsihi amsahau maana mara nyingi hawa watu wanaokua na mapadri huwa hata waolewe huwa wanaendeleza hayo mahusiano.

Kachanganyikiwa hajui afanyeje, wanajamii hebu nipeni ushauri wenu kuhusu huyu ndugu maana msimamo wake naona hauna mashiko.
 
AFE TU!
wa kazi gani huyo!
wanawake wa sasa hawaishi hivyo
 
Wanawake wengi sana sasa hivi ajaribu kumsahau tu, mungu kamsaidia kumuonyesha udhaifu au matatizo aliyonayo ya nini kubeba matatizo ingali unayajua!!!??? APIGE CHINI TU.
 
Huyo msichana anahitaji kuombewa sana. Amekuwa chombo cha adui mwovu katika kumuangusha mpakwa wa Mungu katika dhambi za uzinzi. Inahitaji sana neema na intervention ya Mungu mwenyewe ili waache hiyo dhambi otherwise, ni kama 'kula nyama ya mtu' (quoted from one of J.K.Nyerere's speech) hawawezi kuacha mpaka mmoja apigwe kofi na Mungu au watenganishwe kwa uhamisho wa mmoja wao.Lakini hata wakija kukutana siku zijazo itakuwa ni kazi ileile.
mshauri jamaa aachane kabisa na huyo binti aendelee na maisha yake,wasichana mbona wako wengi tu na wa kila sampuli.
 
hajui afanyeje?
Kwa kifupi hiyo mimba ni ya Padre ndo maana Binti aligoma kupiga simu..
Ila kijana nae sijui kalishwa limbwata wakati jibu ni moja hapo:confused2:
 
hahaha komredi isije kua kale ka avatar kalichangia katika kuangushwa kwenye mchakato wa kura lol......sasa naona umeamua ya nn malimbano bana:becky:

Yaani mkuu acha kabisa! Niliwekeza nyumba sasa natafuta pa kupanga!
 
hahaha Pole sana kiongozi ndo ukubwa huo!! Next time utajua pa kuanzia si umeona mwenyewe michezo hiyo!! hahaha

Sasa hivi nataka nitoke na Kanisa! Ila hawa mapadri wanaharibu kupenda tunda......! Ukisikia nyumba yenye hadhi ya Mchungaji maeneo ya Kijitonyama ni PM
 
Ni rafiki yetu wa familia. Tulifahamiana tangu high school. Amekua na mahusiano na msichana mmoja ambae baadae alikuja kugundua kua anatoka na baba paroko.amejengewa nyumba pia

Wakiwa chuo kikuu kimoja huko jijini wanakopatikana masangara, rafikiangu huyu alijaribu kumsihi mpenziwe huyu aachane na padri ikiwa kweli alikua tayari kuwa nae kwa rest of maisha yake. Binti alikua anamdanganya mara kwa mara kua ameachana na padri lakini jamaa akaja kuwabamba live room kwa huyo dada. Lilizuka vurugu kiasi kua padri alimtishia jamaa maisha ( hata kimasomo kwani mtumishi huyu ni mdosi katika chuo walichokua wanasoma) yeye hakutaka kumtosa binti kwa madai kua alimpenda sana ingawa tulimshauri aachane nae.

Baada ya muda sasa wamemaliza chuo na kijana kwa mapenzi mema alimtambulisha binti kwa baadhi ya ndugu ikiwemo mama yake mzazi ambae alimpenda sana huyo mkwe. Ila kijana hakuwahi kumwambia mamake tabia ya huyo mpenziwe,akidhani atarekebika.

Dada juzijuzi akadai anakitumbo ndii (haijulikani kama ni padri au jamaa) akademand kutoka kwa kijana kua aende kumtambulisha ili maandalizi ya ndoa yafanywe, kijana alikubali ila kwa masharti kua anataka binti amthibitishie kua hana tena mahusiano na baba paroko.bint akadai kua angempigia simu wakiwa pamoja ili athibitishe lakini siku ilipofika hakukubali kupiga simu. Kijana akampa live kua hapo ndo mwisho wa mapenzi yao.

Binti kwa kujua kua mama mkwe anamfagilia akakimbilia kwa mama kumtaka amsaidie ili mwanae amkubali tena. Kijana akaona isiwe tabu akamsimulia mamake kila uozo wa binti kitu ambacho kiliamsha hasira ya mama. Hataki hata kumsikia na binti kwa kujua hilo juzi kaumwa ghafla na sasa kalazwa hospitali hoi. Baadhi ya ndugu wa dada wanamsihi jamaa amsamehe, sisi kama marafiki tumemsihi amsahau maana mara nyingi hawa watu wanaokua na mapadri huwa hata waolewe huwa wanaendeleza hayo mahusiano.

Kachanganyikiwa hajui afanyeje, wanajamii hebu nipeni ushauri wenu kuhusu huyu ndugu maana msimamo wake naona hauna mashiko.

Ningekuwa mimi ningemrudia. Anayependa kujua kwa nini ninasema hivi an-"private message" nimpe mkanda
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom