JembePoli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,324
- 996
Habari zenu wana MMU bila shaka hamjambo,
Mimi ni mume wa mke mmoja lakini pia sisi tulizaliwa wawili (pacha) wote wakiume, baada ya kutokea matatizo ya kufiwa na wazazi wetu tukiwa na miaka 14 tu ilibidi ndugu watuchukue mimi nilienda kwa baba mkubwa Mbeya mwenzangu alienda kwa mjomba Mwanza tukawa tumetengana kwa namna hiyo,tulitembeleana mara moja kwa mwaka kutokana na ratiba za masomo.
Nilipokuwa kidato cha tatu mzee hakulizishwa na mwenendo mzima wa masomo yangu ukilinganisha na pacha wangu wa Mwanza hivyo akaniamishia shule nyingine pale pale Mbeya.Pale ndio nilijuana na binti mmoja matata sana nikafanya bidii akawa rafiki yangu huku nikitafuta siku kumfanya awe mpenzi wangu (maana ulikuwa urafiki wa kaka na dada) sikufanikiwa maana miezi kadhaa mbele nae alihama maisha yakaendelea.
Tukaja kuonana tukiwa wakubwa tena akiwa ni mchumba wa pacha mwenzangu walifunga ndoa miaka 4 iliyopita hawajabahatika kupata mtoto kwa muda wote wa ndoa yao na madaktari wanasema hawana tatizo lolote.
Mimi kama nilivyosema ni mume wa mke mmoja na ndoa yangu inamwaka mmoja tu mpaka sasa bado sijabahatika kupata mtoto japo naamini MUNGU atatujalia tutapata.Kwa sasa tunaishi mkoa mmoja japo wilaya tofauti wote tukiwa na familia.
Jumapili nilikutana na shemeji yangu mke wa pacha akanieleza jinsi ambavyo mumewe amekuwa akitamani mtoto kiasi hata akiwabebea zawadi watoto wa majirani zao yeye kama mwanamke imemuuma akafikilia aje aniombe nitembee nae siku ya hatari ili tu ashike mimba kwa kuwa sisi ni damu moja.
Nikamjibu haitawezekana (mimi na pacha hatufanani labda uwe makini sana) kwanza yule ni ndugu yangu siwezi mfanyia hivyo,alichonambia na kusisitiza ni anaomba kwani inawezekana damu zao haziendani na madaktari wanawasibitishia hawana tatizo na yeye hataki kuona mumewe anahamanika japo anasema hajawahi kuona hata siku moja mmewe akionyesha kuchukizwa na hali ya wao kutokuwa na mtoto kwani huwa akimwambia upo wakati nae ataitwa baba japo anahisi mumewe ipo siku atachoka hali hiyo na atabadilika hivyo ananiomba sana.
Nimefikiria sana;
1~Hata nikiendelea na msimamo wangu wa kukataa si ataenda kwa mwanaume mwingine na kumbambikia ndugu yangu,hata kama nikiingilia si nitaonekana mwehu.
2~Anajua kuwa ninampenda lakini ilikuwa zamani (japo ni mzuri na ni mara 2 ya mwanzo) sasa ninamke sitapenda kumsaliti,japo hawezi kujua ila tu dhamila yangu inanihukumu.
3~Vipi akijua pacha si ndio undugu utakuwa hakuna tena/japo hata mimi napenda kuitwa baba na kwa vyovyote mtoto wao ataniita baba.Kuna msemo unasema ukiwaza sana utaona yote ni majibu sahihi naombeni mnisaidie ki mtazamo wenu.
Tafadhari japo ni ndefu soma kwa umakini na ikumbukwe hatujafanya lolote na shemeji yangu na kuna baadhi ya majina na shule nimeficha kwani inaweza kuleta shida kwani inawezekana nae/nao wanapita pita humu.