Mke wa Mugabe atoa kipondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Mugabe atoa kipondo

Discussion in 'International Forum' started by Mfumwa, Jan 19, 2009.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mke wa rais Mugabe ampa kipigo mpiga picha wa Uingereza
  Monday, January 19, 2009 5:30 AM
  Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe amempa kipondo mpiga picha toka Uingereza alipojaribu kumpiga picha ya karibu wakati mke huyo wa rais alipokuwa likizo nchini Hong Kong kumtembelea binti yake.
  Mpiga picha huyo toka Uingereza amelalamika kuwa mke wa rais wa Zimbwabwe alimpiga magumi ya uso mara kibao alipojaribu kumpiga picha karibu na hoteli moja ya kifahari jijini Hong Kong.

  Richard Jones aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Grace Mugabe, 43, aliwaamuru walinzi wake wamkamate mpiga picha huyo na kumshika kwa nguvu wakati mke huyo wa rais alipokuwa akitoa kipondo kwa mpiga picha huyo.

  "Alinitandika ngumi kadhaa usoni" alisema Jones. "Alikuwa amevaa pete ya almasi ambayo ilinisababishia majeraha kadhaa usoni".

  Jones, 42, kutoka Machen kusini mwa Wales, alikuwa Hong Kong kwaajili ya gazeti la The Sunday Times lenye makazi yake London, Uingereza.

  Jones alisema kuwa ngozi ya uso wake ilipata mipasuko zaidi ya 10 ingawa hakuhitaji kupelekwa hospitali.

  Msemaji wa polisi wa Hong Kong Odelia Tam alisema kuwa polisi wanachunguza mkasa huo na kwamba hadi sasa hakuna aliyekamatwa.

  Ubalozi wa Zimbwabwe Beijing ulikataa kujibu simu zote zilizokuwa zikitaka ufafanuzi wa suala hilo.

  Mke huyo wa rais wa Zimbwabwe alikuwa Hong Kong kumtembelea binti yake Bona anayesoma nchini humo.

  Inasemekana Grace Mugabe aliondoka Hong Kong baada ya mkasa huo wa kumpa kisago mpiga picha huyo.

  Source: http://****************/NewsDetails.aspx?NewsID=841574&&Cat=2
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Grace Mugabe,is some instances you are supposed to use brain, not brawn.This advise will serve you best when the old man is out of office!
   
 3. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli hii ni karne ya 21, mwanamke mweusi anamtwanga mwanaume mweupe ngumi tena za uso? Tumetoka mbali
   
 4. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hela babu!!...money and power have no race...
   
 5. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Upaparazi una kadhia zake kumbe..!

  Grace Mugabe..., dhambi ya mumewe inamtafuna!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jan 20, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Garace Marufu Mugabe hana akili, limbukeni, muuaji, na malaya. Amechangia sana kumfanya mzee Mugabe awe mjinga pia na kuiharibu nchi ile ya Zimbabwe. Uchumi wa Zimbabwe ulianza kuharibika baada ya Mugabe kumuoa Grace ambaye anatembea kila siku kwenda nchi za nje na kukaa kwenye mahoteli ya kifahari bila hata kuwa na mumuwe. Ni mpenda shopingi kuliko mama Imelda Marcos.

  Mama yule alianza kutembea na Mugabe wakati angali sekretari wake na wakati huo alikuwa na bwana yake mwingine aliyekuwa akiitwa Stanley Goreraza. Hakuna uhakika kama watoto wake wawili wa kwanza na Mugabe ni wa Mugabe kweli au ni wa Goreraza.

  Baada ya kuolewa na Mugabe, aliendelea kuwa anatembea na wanaumbe mbalimbali akiwemo James Makamba ambaye baadaye alifukuzwa nchini na Mugabe. Hakuna uhakika kama yule mtoto wake wa tatu ni wa Mugabe kweli au ni wa Makamba. Mama yule alikuwa akienda kulala na Makamba kwenye mahoteli makubwa huko nchi za nje kwa kutumia hela ya walipa kodi wa Zimbabwe; alikuwa akimrubuni mlinzi wake kwa kulala naye pia na kumwonya asitoe siri hizo nje. Hata hivyo habari hizo zilifika kwa mkuu wa ulinzi wa rais wakati huo bwana Winston Changara na hakufurahi. Sasa Grace baada ya kugundua kuwa bwana Changara hafurahishwi na ufuska wake akamsukia njama na baadaye kumwua.

  Mama yule ni hatari sana.
   
Loading...