Mke wa mtu anasema eti ana mimba yangu.

arsenality

Member
May 28, 2017
23
10
Habari za asubuhi wapendwa?
Ni mwaka mmoja sasa tangu nilipokutana na dada mmoja kwenye gari.Dada yule sikuwa nafahamiana nae kabla ya siku hiyo ya safari na nilikua sijawahi kumuona popote.
Siku niliyokutana naye tulikua ndani ya Toyota hiace inayobeba abiria kutoka huku kijijini niliko kwenda mjini.Dada yule alikua amekaa siti ya mwisho na mimi nilikaa siti ile inayotazamana nyuma gari linapotoka.Katika kutizama tizima huku na kule nilikutanisha macho na mdada yule ambaye kwa kweli nikiacha kumsifia kwa uzuri alionao nitakuwa simtendei haki.Tulitazamana kwa mda na kisha akainama kwa aibu tukaendelea na safari yetu.Sikua na wazo lolote juu yake kwani niliamua kumpotezea kwa kuwa nilijua siwezi kumpata na kuendelea kumfikilia ingenipotezea mda tu.
Safari yangu mimi ilikua haifuki mwisho nilikua nashukia njiani ili nipande gari jingine.Nilipofika sehemu ya kushuka niliteremka kwenye gari na kwenda upande wa pili wa barabara ili nisubilie gari jingine niendelee na safari yangu.Baada ya mda kidogo nilishangaa kumuona yule dada naye akija upande ule niliokuwepo.Alifika pale nilipo na kunisalimia vizuri nikaitikia.Mwanzoni alionekana kua na aibu lakini sikutaka hali ile itawale kwani mda mwingi nilikua najitahidi kuongea nae na kumchekesha sana mpaka tukazoeana ndani ya mda mfupi.Magari ya kuja kule tulipokua tunaenda yalichelewa kuja hivyo tukakubaliana tutembee kwa mguu mpaka pale magari yatakapotufikia tutapanda.Basi tukaanza kutembea huku story kati yetu zikizidi kunoga.Ikafikia hatua tukapeana namba za simu ikiwa ni pamoja na kujitambulisha marital status.Mimi sina mke nilimwambia na yeye akaniambia hana Mme.Mpaka gari linatufikia tulikua tumeongea mengi.Tulifika mwisho wa safari yetu na tukaahidiana kuwasiliana mara kwa mara.Kweli ahadi ya kuwasiliana tuliitimiza ipasavyo hadi tukawekeana appointment za kukutana na kweli tukaanza kukutana.
Ilifika hatua tukaanza kugegedana na yule mrembo sijui alinogewa au kitu gani kilichotokea dada yule akawa afunga safari kuja kwangu anakaa siku mbili tatu na kuondoka.
Kipindi chote hicho sikujua kuwa dada yule alikua ameolewa.Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana siku ya krisimasi nilimchenjuana naye baada ya hapo alipoteza simu na tukawa hatuna mawasiliano.Mwezi wa pili mwaka huu alinipigia simu na kuniambia kua ana ujauzito wangu.Sikuwa mbishi sana nilikubali kwa sharti moja tu kuwa mtoto atakayezaliwa lazima afanane na mimi na yeye akasema haina shida anaamini kuwa ujauzito ni wangu.
Kilichonistua ni kitu kimoja mwezi wa tatu mwaka huu niliambiwa kuwa dada yule ni mke wa mtu na tayari ana watoto wa wawili aliozaa na mme wake.Maneno yale yalinipa hamasa ya kutaka kujua ukweli.Nilimpigia simu yule dada na kumuuliza kuwa nilichoambiwa kina ukweli wowote?Akanijibu kua ni kweli yeye ameolewa na ana watoto wawili.Nilipomuuliza kwa nini hakua mkweli kwangu?alinijibu kua alitokea kunipenda sana akahofia kuwa nitaogopa kua naye kwenye mahusiano.Nikamdadisi kuhusu uhusika wangu kwenye ujauzito wake akanijibu kua mimba ile ni yangu kwa asilimia miamoja.
Majuzi alikuja hapa kwangu akaniambia kua mme wake ameukataa ule ujauzito na kamwambia ili waendelee kuishi naye lazima akautoe hivyo amekuja kwangu kuomba ridhaa ya kutoa mimba kwangu.Nilipatwa na kigugumizi sikuwa na jibu la kumpa.Siku hiyo alilala kwangu na kesho yake akaondoka kuelekea kwa mama yake ili akaitoe mimba.Roho yangu iliumia kuona kiumbe kisicho na hatia kikienda kuangamizwa kisa makosa yangu ya kutokua makini na kukurupukia warembo bila kujua background zao.Siku nzima sikua na amani moyoni japo nilijua mwanamke yule aliamua kufanya vile ili kunusuru ndoa yake.
Baada ya siku moja tangu yule mwanamke atoke kwangu alinipigia simu kuwa mama yake ameongea na mme wake na tayari mwanaume amekubali kua ujazito ni wa kwake hivyo swala la abortion ameliacha na anajipanga kurudi kwa mmewe ili taratibu za kliniki zianze.Kwa kiasi nilifurahi kwa kuwa maisha ya mtoto aliyeko tumboni yamesalimika.
Ninatatizwa na haya mambo kwa sasa
1:Je huyu mwanamke ni mkweli?
2:Kama ni kweli iweje aamue kuzaa nje ya ndoa wakati ana mme?
3:Kama mtoto ni wangu nitapataje fursa ya kutambulika kama baba yake mzazi?
4:Tatizo hili linanigharimu sana mda mwingi nawaza nifanyeje ili liondoke kichwani mwangu?
Naomba msaada wenu wa mawazo maana hapa sijielewi nimejaa stress.
 
Wew unaakili ya makinikia...ulishakubali mimba ikatolewe leo unakuja kuuliza utapataje fursa ya kutambulika kama baba...mwanaume mwenzio keshakubal kama mtoto ni wake..wew kaa mbali nyau wew
 
Wew unaakili ya makinikia...ulishakubali mimba ikatolewe leo unakuja kuuliza utapataje fursa ya kutambulika kama baba...mwanaume mwenzio keshakubal kama mtoto ni wake..wew kaa mbali nyau wew
Mara nyingi ustarabu huwa ni kitu cha bure kabisa czani kama kulikuwa kuna haja ya kumtukana ,jamaa kajieleza vizur tu kama ulikua huna ushauri ungekaa kimya tu
 
Wew unaakili ya makinikia...ulishakubali mimba ikatolewe leo unakuja kuuliza utapataje fursa ya kutambulika kama baba...mwanaume mwenzio keshakubal kama mtoto ni wake..wew kaa mbali nyau wew
Ni bora ungetoa ushauri ndugu kuliko kutoa tusi zito kama hilo yani unajua kumwita mtu kinikia kwa kipindi kama hiki unakua humtendei haki.Kinikia ni tusi la mwaka.Pia elewa psychologically siko vizuri.Tambua kua yule dada alishauriwa asitoe mimba na mama yake mzazi baada ya usuruhishi kufanyika kati ya mke na mme.Lakini yule dada anaendelea kuniambia kua mimba ni ya kwangu sasa hapo ndo ninapopata mkanganyiko wa mawazo.
 
funguka kwa mwenye mali ajue wewe ndo umekula mali yake na kuacha ki zygote chako mambo yawe mswanoo hapo hata mkipigana mwisho wa mchezo wewe ndo baba
 
Suala kukutanisha vikojoleo halijawahi kuacha wenye tamaa salama...

Una stress gani wakati mme wake kaikubali mimba...Relax
 
SWALI LA KIMAKINIA,inakuwaje utembee na mke wa mtu!!!
SWALI LA KICHENJUAJI,Inakuwaje unatembea na mke wa mtu bila kondom!!!
SWALI LA KIMIKATABA,Inakuwaje unampa mimba mke wa mtu??!!!!
1:Sikujua kama ni mke wa mtu

2:Mwanzoni nilitumia kinga baadae tulivyopima tukawa huru kuchenjuana bila soksi

3:Hatukusaini mkataba wowote ilitokea accidentally.
 
Back
Top Bottom