Mke wa mtu ameniponza

Mke wa mtu ameniponza

mathew chance

New Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
4
Reaction score
7
Wakuu habari zenu,

Nimeona wengi wanakuja hapa kwa ushauri na wanafanikwa nami nimeona niseme langu naweza pata ufumbuzi. Wakuu nilikuja Dar kwa mara ya kwanza kujiunga na chuo sikua nimefika kabla ya hapo
mwezi mmoja tangu tuanze chuo dada mmoja aliniomba tuwe group moja la discussion
baada ya kuona uwezo wangu class

Baadae tulianza kushangaa huyu dada anakuja amevimba uso wakati mwingine na bandage mkononi akawa anaficha Mara asema alianguka bafuni na kadhalika. Siku moja tukiwa tunasoma wawili tu na tukiwa tumeshazoeana sana akaniambia ukweli kuwa huwa anapigwa sana na mumewe.

Kila akirudi home anakaguliwa kufuli alilovaa kama lina uchafu wa mwanaume, hata kufuli likikutwa na mabaki ya mkojo au ute umeganda pale basi atapigwa vibaya sana. Yaani akawa na maisha ya frustration ile mbaya, Mimi nikawa karibu yake wakati wote kwa faraja na kushauri.

One day aliniomba twende Ununio Beach tukashangae maji Jumapili moja hivi mumewe akiwa safarini
Tukiwa hapo hatukushuka garini tuliagiza pombe tukawa tunanywea garini ilipofika jioni tukawa hoi kwa pombe na giza lilishaingia tukajikuta na peana denda na beach yenyewe bado ni mpya ina vichaka akaingiza gari kichakani tukaamia kiti cha nyuma na tukajikuta tumezini.

Ilikua ni mara yangu ya kwanza kuzini nilisoma Seminari na baadae upadri nilipomaliza mwaka kwenye masomo ya Upadri baba alikuja kunipa good news kuwa nimepata scholarship kutoka shirika moja hivi, natakiwa kuja Dar kuanza chuo, nikapiga chini upadri ndio nikaja Dar es salaam.

Ikawa kila siku ndio mchezo wetu alikua anaogopa kuingia nyumba za wageni.Mwaka wa mwisho akabeba mimba yangu ila alimsakizia mumewe. Infact alifanya mtihani wa mwisho na tumbo kubwa tu,
mwisho wa mwaka December tuka graduate akiwa na mtoto mchanga.

Mwaka uliofuata nikawa nipo mtaani doro sina kazi wala nini. Nikashangaa yule mpenzi wangu amekata mawasiliano ghafla, hadi wiki inaisha kimya.Nikimpigia mimi hapokei baadae namba haipatikani kabisa.
Siku moja akanipigia simu kwa namba nyingine akasema mimi na yeye basi ameshaelewana na mumewe na wana amani na nisimfahamu tena wala kumtafuta niliumia sana moyoni nilikua nampenda sana
nilikaa gheto naugulia naumivu zaidi ya mwezi.

Alikuepo dada mwingine kwenye group yetu walikua marafiki wa kufa na kuzikana na huyu mke Wa mtu na alijua siri zetu na alishiriki shughuli zote za familia ya mpenzi wangu akawa amekuja gheto kuniuliza kulikoni kuna nini kimetokea kati yangu mpenzi wangu nikamweleza kila kitu.

Nikamwambia nina hali mbaya sana kifedha hata hela ya kuandika maombi ya kazi na kutuma sina na kodi imeisha nabembeleza tu kwa landlord. Akasema haina shida kwake ana vyumba viwili na sebule nitumie kimoja nikahama siku ile ile huyu rafiki mtu aliachika alikaa miaka mitano bila mtoto akaletewa zengwe akapewa talaka ni muislam yule mke wa mtu ni Christian. Rafiki mtu alikua anafanya hata tulipokua chuo so akanifanyia mpango nikapata kazi.

Siku moja tukaenda club tukarudi usiku sana nakuja kustuka asubuhi najikuta chumbani kwa huyu rafiki mtu tupo kama tulivyozaliwa kwenye shuka moja nadhani ilikua ni pombe ile tangu siku hiyo letu likawa ni moja tunapika na kupakua,asubuhi ananipitisha kazini jioni ananipitia.

Siku moja nipo bafuni naoga nikasikia watu wanaongea sebuleni nikatoka na taulo nakutana uso kwa uso na yule mke Wa mtu alistuka kwa mshangao na kuanzisha ugomvi pale akasema kumbe mimi ni malaya kiasi kile hadi natembea na rafiki yake wakapelekana nje huko wanazozana mi nikarudi room.

Usiku akaniandikia ujumbe akisema alikosea kuniacha kwamba mumewe hakubadilika aliendelea na tabia za awali za ulevi uliokithiri na kumkagua sehemu za siri kila siku. Hivyo amedhamiria kuachana nae mazima ndio alikua kwenye mchakato wa kunitafuta hata pale kwa rafiki alikuja kumuuliza kama anajua nilipo ndio akashangaa kunikuta pale. So anaomba turudiane yupo tayari kumkimbia jamaa ili tulee mtoto wetu wote.

Kwa kweli bado hajanitoka moyoni nikashindwa kumjibu na vitu alivyokua akinipa anamshinda huyu mrangi mbali tukumbu ile meseji ya whatsaap mumewe usiku akaiona demu alipigwa nusu ya kufa. Kesho yake akamfuata mwanamke wangu kazini kwake akamwambia jamaa yako anatembea na mke wangu nikimpata ataona mwambie hivyo.

Demu akanipigia simu akaniambia Leo tafuta gesti ulale kwa usalama wako. Baadae jamaa akanipigia mwenyewe akasema usalama wako ni kuhama Dar na kuwa atahakikisha anapajua kazini kwangu tupambane. Hivi sasa nakaa kazini huku nachungulia nje kila wakati nikimpigia simu jamaa ili nimwambie mimi sina tena uhusiano na mkewe hanisikilizi kabisa. Anasema nimethubutu kuzaa na mkewe na tumembambika mtoto halafu tutoroke.

Wakuu nipo njia panda, naishi kwa hofu mwanamke wangu anasema nisimuogope mwanaume mwenzangu nim face tu, anasema twende na yeye ataelezea historia nzima ya hill tatizo shida ni je iki fail? Hata hivyo nampenda yule mwingine kama si ndoa ningejua nae maana yeye tunalingana umri sema aliwahi kuolewa after form six, huyu rafiki mtu ananizidi karibu miaka mitano.

Nahitaji msaada wenu
 
Wewe jamaa sijui, ngoja waje wakupe ushauri wengine
 
Umekula vya watu arif, lazima uogope. Nenda kaongee nae kiume, ukikimbia unaacha mtoto halafu inakuwa noma zaidi. Kama huna ujasiri, nenda na washkaji zako kadhaa, ama nenda kisheria.
 
Pole sana broo sasa unajua inauma na ni dharau mwanaume mwenzako kutembea na mkeo kisha kuzaa nae wewe jaribu kuhama ja maa akikuua mahakaman anaushahid alichofanyiwa hivyo kesi hiyo ni ya kuua bila kukusudia ushaur wangu hama mbali huyo anakisasi
 
Ingawa ulifanya makosa kwa kutembea na mke wa mtu lakini linapokuja suala la usalama wa uhai wako hauna haja ya kusubiri zaidi ya kwenda kuripoti Polisi,suala la kutishia uhai wa mtu ni kosa na wewe uhai wako upo mashakani.Kama kuna makosa ambayo utatakiwa uwajibike huko Polisi ni heri uwe tayari kuliko kupoteza uhai wako.
 
Fonts ndogo sana nimeishia katikati,Chukua ushuri huo huo utakaopewa.
 
Waseminasti wengi ni watu dhaifu sana ktk masuala ya mapenzi. Kwa maana hiyo tatizo la kwanza ni hilo. Mapenzi ni Sanaa yenye kutaka maarifa ili kuimudu, wewe huna maarifa, yatafute. Kama kazi umepata kwa nini unaendekeza "mjini msingi kiuno". Kwa nini hutaki kufikiri nje ya boksi kwamba waweza kuwa na maisha yako kwa maana ya kijitegemea. Mtu kukutishia maisha ni kosa ni vizuri ukaenda kutoa taarifa polisi. Pengine utasita kwa sababu ya kuzaa na huyo "mke wa mtu", hilo lisikutishe kwani mbele ya sheria ni kosa Dogo sana.
 
Pole sana broo sasa unajua inauma na ni dharau mwanaume mwenzako kutembea na mkeo kisha kuzaa nae wewe jaribu kuhama ja maa akikuua mahakaman anaushahid alichofanyiwa hivyo kesi hiyo ni ya kuua bila kukusudia ushaur wangu hama mbali huyo anakisasi

Hapa unapotosha. Huyo mume wa mtu akimdhuru kwa vyovyote hana kinga yoyote kisheria! Hapo ameua kwa kukusudia kwani hasira (heat of passion) imeshaisha.

Back to topic: Pole kwa masaibu. Nimefurahi umesema 'nikajikuta tumezini' ila sio poa kuisingizia pombe.
Cha maana tafuta tu wazee watu wazima waeleze hilo jambo (usipuuze kwenda polisi kutoa taarifa ya kutishiwa maisha...just in case huyu mume wa mtu atakuwa irrational). Hofu yangu ni je, huyu mke wa mtu anakupenda au anakwepa vipigo?
 
Rudi mkoani kwenu katafute kazi huko acha mapenzi ya muvi utauliwa mjini hapa! Kwanza umeiba mke wa mtu, huoni kosa unalazimisha unampenda, haya endelea kumpenda ukabakwe na wanaume wenzio.
If i were u, ningerudi mkoani kwangu nianze sifuri na kukata mawasiliano kabisa hadi kupoe,
si lazima kukaa mjini kwa kuvizia ushaharibu
 
ndo maana nakuaga addicted na jf, kila sekunde linashushwa zaga jipyaaaa!!!....very interesting....
zaga jipyaaaa.
ngoja nije,
 
mkuu nikushauri kitu kimoja tu, kwanza jamaa ni msitarab na hana papara, otherwise kwa case kama hiyo ilikuwa haina kukupigia simu wala nini angekutafta na kukupata na kutenganisha kichwa na kiwiliwili kwishaaa....
udate mke wa mtu, umpe mimba, jamaa aleee, kisha ajue...
think ov ut side!!! huyu jamaa ana uvumilivu either atakufanyia mbaya in future ni just suala la muda tu.
ushaur wangu, mtapeli huyo ulonae hela za kutosha kama unajua ATM yake password vuta mkwanja, kisha piga chini kazi then potelea mkoa mwingine usake maisha.
otherwise hujui yule jamaa siku zinavyienda anazidi kuchemka hasira tu tena akimuona mtoto....
atakuua wallah
 
Luka 16:18 Yeyote anayemwacha mke wake na kuoa mwingine, anazini; na yeyote anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

wachana na wake za watu na utubu.
 
pili naomba kuuliza wadau, mm sijawqh kunywa pombe toka nizaliwe, sasa kama ukinywa pombe unapoteza network yan unayembea njian hujijui..hadi unaingia ndan kwa mtu hujijui....unavua nguo hujijui.....unapanda bed hujijui....unalalla bila kujua....unadate na mtu bila kujua, ila asbh ukiamka ndo unajua yote haya.!!!!
daaaah maana kila mtu humu naona thread yake ni pombe kushtuka asbh, pombe kushtuka asbh...
NAAMINI POMBE INAWAPELEKAGA AHELA MNASAVEY KISHA MNARUDI DUNIANI ASEEE, MAANA KAMA YOTE HAYA YANAFANYIKA MTU HUJIJUI DAAAAH NGOJA NIJE NAMI NITEST ILI NISIJUE KINACHOENDELEA DUNIANI KWA MASAA 12 CONSECUTIVE.
 
Waseminasti wengi ni watu dhaifu sana ktk masuala ya mapenzi. Kwa maana hiyo tatizo la kwanza ni hilo. Mapenzi ni Sanaa yenye kutaka maarifa ili kuimudu, wewe huna maarifa, yatafute. Kama kazi umepata kwa nini unaendekeza "mjini msingi kiuno". Kwa nini hutaki kufikiri nje ya boksi kwamba waweza kuwa na maisha yako kwa maana ya kijitegemea. Mtu kukutishia maisha ni kosa ni vizuri ukaenda kutoa taarifa polisi. Pengine utasita kwa sababu ya kuzaa na huyo "mke wa mtu", hilo lisikutishe kwani mbele ya sheria ni kosa Dogo sana.
******
mdanganye mwenzako kwamba mambo ya kisheria, akiuawa kwa hasira za mtu ni kwel sheria itaendelea na yeye atakuwa mbinguni akichungulia kwa chini kupitia tobo la mbingu kumuona hakimu akisemaje pale kisutu.
mke wa mtu anauma usitie jeuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom