Mke wa Mpoki amfilisi hatari, wanawake mungu anawaona

venchwa

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
1,677
1,592
Kama mjuavyo Eboue jina lake la Utani ni Mpoki hii ni kutokana na kufanana sana na mpoki wa Tanzania, yanemkuta yafuatayo,

Naikumbuka mechi ya fainali, Klabu Bingwa Ulaya msimu wa mwaka 2005-2006, Barcelona dhidi ya Arsenal, ndani ya dimba la Stade de France, mjini Saint Denis, Paris, Ufaransa. Ilikuwa Mei 17, 2006.

Namkumbuka beki wa kulia wa Arsenal, Emmanuel Eboue alivyofanya kazi kubwa siku hiyo kama ambavyo alizowea kufanya siku zote alipokuwa uwanjani. Bonge la beki, mjuzi wa kukaba, mjanja na mwenye kasi, fundi wa chenga na aliyevutia alivyoutawala mpira (magnificent football controller).

Nakumbuka Arsenal waliingia uwanjani kama underdog, yaani timu isiyopewa nafasi ya ushindi, kisha dakika ya 18 walipata pigo baada ya golikipa Jens Lehman kulimwa kadi nyekundu, kwa kumdaka mguu, Samuel Eto'o aliyekuwa anakwenda kufunga.

Naikumbuka zaidi dakika ya 36, Kolo Toure anampa pasi Eboue ambaye anauvuta mpira kisha anampiga chenga beki wa kati na nahodha wa Barcelona, Carles Puyol lakini baada ya chenga mpira unasogea mbali, na kuwa karibu zaidi na beki wa kushoto wa Barcelona, Giovanni van Bronckhorst 'Gio', aliyeuacha na kuwa goal kick.

Eboue baada ya kumpiga chenga Puyol kisha kugundua mpira umesogea mbali ya umiliki wake, alifanya uamuzi wa haraka wa kujiangusha. Ikawa adhabu ndogo nje kidogo ya mstari wa eneo la penalti (18-Yard Box).

Mpira wa adhabu ulipigwa na straika Thierry Henry kisha beki Sol Campbell alijitwisha kichwani na kuifungia Arsenal bao la kuongoza. Goli hilo lilidumu muda mrefu lakini dakika 12 za mwisho Arsenal walikubali mabao mawili kutoka Barca na kufanya Barcelona wabebe kombe kwa ushindi wa magoli 2-1.

Mechi hiyo ndiyo ya mafanikio zaidi kwa Arsenal kufika fainali Klabu Bingwa Ulaya, wakati Barcelona, kwa ushindi huo walibeba kombe mara ya pili, baada ya kulitwaa mara ya kwanza mwaka 1992. Kutoka hapo (mwaka 2006), Barca walilitwaa tena mwaka 2009, 2011 na 2015.

NIMEJIKUMBUKIA ZANGU TU!

Nimejikuta naikumbuka mechi hiyo kutokana na ustadi mkubwa wa Eboue ambao aliuonesha. Ujanja na 'utapeli wa kimchezo' ambao aliufanya na kuipatia Arsenal goli la kuongoza ambalo lilikaribia kuipa Arsenal taji la kwanza la Klabu Bingwa Ulaya (UCL).

Kitu kimoja ambacho hukumbuka na kukubali ubora wa Eboue nyakati zote ni mtindo wake wa kuchangamka alipokuwa na mpira. Si aina ya wachezaji wenye kupoa. Uchangamfu wake ni kielelezo kwamba alifurahia alichokifanya kiakili na kimwili. Nilimpenda Eboue. Nampenda Eboue!

Basi hivi karibuni nikasoma mfululizo wa habari na makala kuhusu Eboue, kwamba mtalaka wake, Aurelie Bertrand, raia wa Ubelgiji, amemkomba kila kitu na sasa mchezaji huyo wa zamani wa kimaitaifa wa Ivory Coast, anaishi kwa hofu kubwa, tena akilala kwenye vibaraza vya nyumba za marafiki.

Jaji Edward Cross ambaye alisikiliza kesi ya mgogoro wa ndoa kati ya Eboue na Aurelie, alitoa hukumu yenye kumpa Aurelie umiliki wa kila kitu mpaka jumba lake lililopo London, Uingereza, baada ya Eboue kutohudhuria mahakamani.

Tayari magari na mali nyingine zote Aurelie ameshakomba. Eboue anasubiri muda wowote jumba lake litwaliwe na Aurelie kwa amri ya mahakama kwa sababu alipewa wiki tatu alikabidhi kwa mtalaka wake, na muda huo umeshapita bila kutekeleza agizo alilopewa.

EBOUE WA MAJANGA

Hilo ni tukio kubwa kati ya mengine mfululizo yaliyompata. Mwaka jana (2016), kabla ya kuanza kwa msimu wa 2016-2017, Eboue akiwa mchezaji huru, alifanyiwa ukarimu na kocha Sam Allardyce 'Big Sam', wakati huo akiwa kocha wa Sunderland 'Black Cats'.

Eboue baada ya kumaliza mkataba wake na Galatasaray ya Uturuki, alikaa miezi 18 bila timu, ndipo Big Sam akiwa kocha wa Sunderland, alimwita na kumpa kazi kwenye klabu hiyo ya Wearside, Kaskazini Mashariki ya England.

Eboue alitua Wearside lakini kabla ya kuanza msimu, alipokea ripoti ya adhabu kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), akifungiwa kutocheza soka mwaka mmoja kwa kosa la kutomlipa wakala wake wa zamani, Sebastien Boisseau, fedha pauni 1 milioni (Sh3 bilioni) za malipo ya usajili wa zamani.

Baada ya kuondoka Sunderland, Eboue alisema: "Siku naondoka Wearside nililia, machozi yalinitoka. Nilikaa bila timu muda mrefu, Big Sam akaniita na kuniambia 'mwanangu una uwezo, nakupa nafasi, haitakuwa ya muda mrefu lakini itakusaidia', kwa kweli sitamsahau Big Sam."

Achana na ukarimu uliogonga mwamba wa Big Sam ambaye sasa ni kocha wa Everton ya England. Mwaka huu, Eboue alikuwa ajiunge na klabu ya Turk Ocagı Limasol ya Cyprus lakini afya ikaleta utata.

Eboue alipofanya vipimo kwa ajili ya kujiunga na Limasol, alibainika kuwa na virusi visivyo vya kawaida kwenye damu, hivyo kusababisha dili lake la kwenda kucheza soka Cyprus libume.

Akiwa kwenye hali tata, vyombo vya habari vya Uturuki viliandika kuwa virusi alivyobainika kuwa navyo Eboue ni vya Ukimwi. Hata hivyo, ulitolewa msisitizo kwamba Eboue ana virusi visivyo vya kawaida kwenye damu, kwamba ni mapema mno kumsema ameathirika na Virusi Vya Ukimwi (VVU).

DUNIA NI NGUMU SANA

Eboue akiwa kwenye mazingira hayo kuhusu utata wa kiafya na misukosuko ya kupata timu, halafu soka ndiyo ajira yake ya pekee, mkewe naye amemuongezea pigo kwa kumkomba kila kitu, zaidi amemnyima haki ya kuwa karibu na wanaye wawili wa kike.

Watoto hao wa kike ni Clara, 14 na Maeva, 12. Mtoto pekee ambaye Eboue ana nafasi ya kuwasiliana naye ni Mathis, miaka tisa, ambaye ni mvulana, anayelelewa kwenye kituo cha soka cha Arsenal.

Ukiyaweka pamoja yote ambayo Eboue anayapitia, unaona hakika dunia ni ngumu upande wa wake, lakini lipo fundisho kubwa na baya kwa kila mtu. Ni fundisho kuhusu ubinafsi. Kwamba ukiwa na mali zilinde mithili ya kuku na vifaranga vyake.

Eboue ni mjinga? Hapana hata kidogo. Alimwamini mke wake ambaye amekosa ubinadamu kabisa. Wanandoa wanatakiwa kuaminiana kama ambavyo Eboue alimwamini Aurelie. Alipokuwa akimwamini hakujua kama angegeuka.

Hivyo Eboue si mjinga, ameponzwa na imani yake kwa mtu ambaye kiusahihi anatakiwa kumwamini. Hata hivyo, aliyeaminiwa hakupaswa kuaminiwa.

Swali ni moja; mwenye kustahili kuaminiwa ana rangi gani? Jawabu ni kuwa anayestahili na asiyestahili wote hawana alama. Hivyo kwa yaliyompata Eboue, somo ni kugeuka kuku, lalia mali unazochuma kama kuku anavyolalia vifaranga vyake.

Kuna mtu atasema Eboue ni mjinga, badala ya kuwekeza kwa majina ya ndugu zake au mama yake, amewekeza kwa jina la mkewe. Jawabu ni moja tu; ni wangapi walidhulumiwa mali na ndugu zao?

Ni wangapi walipofariki dunia, watoto wao hawakufaidi mali zilizochumwa na wazazi wao kwa sababu ya ndugu wenye roho mbaya walioamua kudhulumu kila kitu?

Mbele ya mali binadamu haaminiki. Pengine Eboue aliona awekeze kwa jina la mke wake ili hata akifa watoto wake wasiteseke. Maana ndugu wa Kiafrika hawajambo, mtu akifa ndugu wanagombea urithi, wanawanyang'anya mpaka watoto.

Kuhusu kumwandika jina mama, hayo ni mawazo ya hovyo. Mama anatakiwa arithi kwa mtoto au mtoto arithi kwa mama? Usisahau pia mkasa wa staa wa Togo, Emmanuel Adebayor alivyovurugana na mama yake kisa mali. Zingatia; mbele ya mali binadamu si wa kumwamini. Wazazi huweza kuua mtoto wao ili wamdhulumu mali zake.

Tukubali hoja ya Eboue kuwa hakuwa na elimu ya kutosha kuhusu udhibiti wa fedha. Hoja hiyo ikupe mwongozo wa kushika kuhusu udhibiti wa mali zako, huku ukiwaandalia watoto wako halali yao ya urithi. Ukizubaa, wasiostahili watarithi mali za wanao.

Pengine Aurelie amepata "penzi jipya", kajamaa fulani kanatanua na magari ya Eboue ambaye hivi sasa anapanda 'daladala' za London kwa kujificha asijulikane. Somo; utampa kila kitu kwa sababu ya mapenzi leo, kesho atakuumiza kwa vyote ulivyompa baada ya mapenzi kwisha.

Kosa lingine ambalo Eboue amefanya ni kutohudhuria mahakamani. Pengine angesimama mbele ya Jaji na kujieleza angeeleweka. Hapa Eboue alizingua kuifanyia kiburi mahakama. Inawezeka Jaji alitoa hukumu hiyo ili kumkomoa.

Eboue mshahara wake kwa mwaka Galatasay ulikuwa pauni 1.5 milioni (Sh4.5 bilioni) kwa mwaka. Eboue anasema kuwa alipokuwa Uturuki alikuwa anatengeneza euro 8 milioni (Sh21 bilioni) kwa mwaka.

Fedha hizo Sh21 bilioni kwa mwaka ni sawa na kusema Eboue alikuwa akiingiza Sh1.75 bilioni kwa mwezi, Sh437.5 milioni kwa wiki, Sh62.5 milioni kila siku. Hizo fedha ni nyingi mno. Mke kasepa nazo. Mke waliyezaa watoto watatu. Kweli, hata zimwi likujualo linaweza kukumaliza.

Eboue anasema, katika euro 8 milioni (Sh21 bilioni), yeye alikuwa anabaki na Euro 1 milioni (Sh2.7 bilioni) na euro 7 milioni (Sh18.6 bilioni) alikuwa akimtumia mkewe. Yaani mke pamoja na kupokea Sh18.6 bilioni kila mwaka, amemtenda haya Eboue? Aisee, zimwi likujualo linaweza kukumaliza.

Inawezekana Aurelie anamuona Eboue hafai tena baada ya ripoti yake ya kiafya. Hata hivyo, kwako umakini unahitajika sana. Unachokipata kiatamie kama kuku na mayai yake au kuku na vifaranga vyake.

C&P

Viva United
Viva Lukaku
 
5d8fd3870bbe2ff8f0a46faec1201031.jpg
 
Wazungu nao Kumbe gold digger tena wanakuchinjia mbalii bila huruma,, me nlijua ni waafrica wanaolewa na kuoa wazungu tuu sio mbaya dunia duara,, nlisikia kapata kazi ya ukocha team yake ya zamani mojawapo
 
Sijapata kushukuru wajuaji wa jf ila hapa nina wajibu wa kusema Ahsante. nakiri nisingefahamu maisha ya nguli huyu popote pale. Nimejifunza vingi kupitia stori yake.
 
Wazungu wengine masikini tuu! Angemchukua mwafrika mwenzake hayo yote yasingemkuta!!

Hiyo mbunye inaonesha ina utamu zaidi ya vanilla!!
 
mpoki alioa lini?

ila bora bwana yule mhaya hajisomi kabisa

dadako amekimbia dushe njoo muonee Ushauri: Aliomba MACHINE kwa Mungu, alipopewa akaikimbia...

Mwengine amefumaniwa huku STORY: FUMANIZI LA UKUBWANI

na mwingine hajui kutongoza hukuu Stori: Jinsi ya Kumtongoza Mwanamke
 
Thenk yiu
We jamaa kwa kudesa tu..umetisha.
Dah!
Haya.
yaani litopic lote hilo
Sio mbaya Galatasaray wanampa kazi, hope atapata hela ya kula..

Daah, hawa viumbe wana roho mbaya sana
Sijui ni nani aliyewaweka wanawake kwenye kundi la binadamu
Ebwana ndevu sana mshkaji wangu... Ntarudi badae!
Faida za wanawake ni kubwa kuliko tunavyofikiria
Wazungu wengine masikini tuu! Angemchukua mwafrika mwenzake hayo yote yasingemkuta!!

Hiyo mbunye inaonesha ina utamu zaidi ya vanilla!!
usicheze Na hiyo jinsia
dadako amekimbia dushe njoo muonee Ushauri: Aliomba MACHINE kwa Mungu, alipopewa akaikimbia...

Mwengine amefumaniwa huku STORY: FUMANIZI LA UKUBWANI

na mwingine hajui kutongoza hukuu Stori: Jinsi ya Kumtongoza Mwanamke
 
Wazungu wengine masikini tuu! Angemchukua mwafrika mwenzake hayo yote yasingemkuta!!

Hiyo mbunye inaonesha ina utamu zaidi ya vanilla!!
Waafrika hawajui kutapeli?

Wanawake wa Africa wana afadhali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom