Ukiwa na mkeo/mumeo huna cha kuongea vyote mmemaliza home lakini kimada ndo wakati wake huo maana muda si muda utarudi home
mmmmmh leo kazi ipo na hizi mvua duh!~yap ni kweli hata mm nimeshaona sana lkn nadhani huwa mambo mengi wameshayaongea labda nyumbani kabla hawajatoka so barabarani hawatakuwa na mengi ya kuzungumza,lkn pia mwanamme akiwa na kimada sasa si anataka kuonyesha ufundi wa maneno kabla ya ufundi wa matendo jamani?
Ki ukweli Nguli mimi huwa naishia kucheka kuna siku bana nilipewa lift dah nilijuta maana humo ndani ilikuwa kama vile ni mabubu nikawa najiuliza hawa leo wameamkaje asubuhi kibaya zaidi mwanamke ndio akawa anapiga stori zaidi na mimi mwanaume alikuwa ameuchuna tu
Ha ha ha lazma jioni au baada ya wewe kushushwa mke alichimbwa biti:smile-big:
Hiyo lazima itakuwa ilitokea maana wakati tunapiga stori jamaa alikuwa anatuchecki kwenye kupitia kwenye kioo nikasema nikushuka lazima timbwili litaendelea tu
Mkubwa wakati tunasubiri waziri mkuu usisahau ile hafla ya kuuaga mwaka itakayofanyikia maeneo ya kwa ODM next month kwa kuchinja mbuzi mzima ambaye budget yake tayari ishatolewa na kuwa approved.
tatizo wake zetu nao hawana story mpya kila siku ni kulalamika tuuuuu...., hakuna jipya.., kwenye gari unakunja sura hakuna kucheka, majibu ya mkato, (sawa.., ulitakaje?..., subiri mwisho wa mwezi.. etc)...... !!!
NB: mi wangu tunacheka mwanzo mwisho.....
Inategemea na mahusiano yenu yakoje.
Upendo ukiwa juu, mkeo anakuwa ni rafiki yako, hutokosa ya kumuongelesha.
Lakini kama penzi limechakachuliwa na nyumba ndogo, basi mke unamuona kama zigo la uding'a.
Muda wa kuongea maongezi matamu unakuwa haupo, unabaki muda wa kulaumu, kutukana na kugombeza.
wewe dume ndio unakuwa perfect muda wote, na mwanamke anakuwa mkosaji muda wote, hata akikuwekea maji ya moto ya kuoga unamwambia mbona kuyaunga tui maji yangu ya kuoga?
kisha unaanzisha zogo
Kipya kinyemi japokuwa kidonda
Mihamu tu ndio inayosababisha vituko kwewnye usafiri.
Utakuta mtu yuko na mkewe, halafu macho yake yako juu juu kuchungulia kwenye magari ya wanawake na kuwakonyeza.
Waifu akishtukia, utasikia jamaa akijitetea, ohhh tulikuwa naye JKT kwenye kambi ya pale Kariakoo
Wanawake ni wakorofi sana especially kama baba anadrive...Lazima atakusahihisha bila sababu njiani!...aaahh... pitia njia ile mi nina haraka bana, mara..aahh si unaona sasa tumezibwa...mara bwana unakimbiza sana, hatuna haraka hiyo!, mara nipeleke kwa nanihino, halafu unifuate baada ya nusu saa!..!Na tena huwa ni maongezi ya tabasamu na vicheko kwa kimada ,lakini kama ni wife na husband watu wanauchuna utadhani hawajuani vile :smile::smile::smile::smile::smile: