Mke na Mume(WANANDOA)

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,805
637
Kwa asilimia kubwa wanandoa wakiwa wanaelekea kazini/mahala kwa wale waliojaliwa usafiri/gari huwa wanauchuna ndani ya gari sana. Nimekuwa nikijiuliza hivi kwa nini? hata ukibahatika siku hio ukapewa lifti utadhani wana ugomvi au hawakupenda wewe upande gari yao. Hasa kwenye hizi foleni za dar kwa unaowafahamu utaona uso mkavu na mzito kama mjeshi alie retire wa kikosi cha vita.

Lakini umkute mwanandoa huyo hasa wa kiuume amempakia kimada/nyumba ndogo OMG utaona meno yoote nje na uso wenye matumaini wa kuimaliza siku kwa furaha. Kama ni pikipiki basi kimada anamkumbatia dereva/mume wa mtu kwa nyuma mpaka karibu mtu atapike ini, akiwa ni mke kapakiwa anakaa mzungu wa 4 kabisa na wala hakamati kwa furaha

Hivi wadau na nyie mmewai ku observe hii kitu? na kwa nini mtu msiwe na furaha mkiwa pamoja au ni ka principle ka ndoa ukiwa na mwanandoa mwenzio lazma ukunje uso ili akuone uko serious na marriage life?
 
Ukiwa na mkeo/mumeo huna cha kuongea vyote mmemaliza home lakini kimada ndo wakati wake huo maana muda si muda utarudi home
 
mmmmmh leo kazi ipo na hizi mvua duh!~yap ni kweli hata mm nimeshaona sana lkn nadhani huwa mambo mengi wameshayaongea labda nyumbani kabla hawajatoka so barabarani hawatakuwa na mengi ya kuzungumza,lkn pia mwanamme akiwa na kimada sasa si anataka kuonyesha ufundi wa maneno kabla ya ufundi wa matendo jamani?
 
Ukiwa na mkeo/mumeo huna cha kuongea vyote mmemaliza home lakini kimada ndo wakati wake huo maana muda si muda utarudi home

Al right wandugu lakini hata sura/wanavyotizamana jamani....? ina maana nyumbani washatizamana vya kutosha kwa hio barabarani wanatishana??

mmmmmh leo kazi ipo na hizi mvua duh!~yap ni kweli hata mm nimeshaona sana lkn nadhani huwa mambo mengi wameshayaongea labda nyumbani kabla hawajatoka so barabarani hawatakuwa na mengi ya kuzungumza,lkn pia mwanamme akiwa na kimada sasa si anataka kuonyesha ufundi wa maneno kabla ya ufundi wa matendo jamani?
 
Inategemea na mahusiano yenu yakoje.
Upendo ukiwa juu, mkeo anakuwa ni rafiki yako, hutokosa ya kumuongelesha.
Lakini kama penzi limechakachuliwa na nyumba ndogo, basi mke unamuona kama zigo la uding'a.
Muda wa kuongea maongezi matamu unakuwa haupo, unabaki muda wa kulaumu, kutukana na kugombeza.
wewe dume ndio unakuwa perfect muda wote, na mwanamke anakuwa mkosaji muda wote, hata akikuwekea maji ya moto ya kuoga unamwambia mbona kuyaunga tui maji yangu ya kuoga?
kisha unaanzisha zogo
 
Mihamu tu ndio inayosababisha vituko kwewnye usafiri.
Utakuta mtu yuko na mkewe, halafu macho yake yako juu juu kuchungulia kwenye magari ya wanawake na kuwakonyeza.
Waifu akishtukia, utasikia jamaa akijitetea, ohhh tulikuwa naye JKT kwenye kambi ya pale Kariakoo
 
Ki ukweli Nguli mimi huwa naishia kucheka kuna siku bana nilipewa lift dah nilijuta maana humo ndani ilikuwa kama vile ni mabubu nikawa najiuliza hawa leo wameamkaje asubuhi kibaya zaidi mwanamke ndio akawa anapiga stori zaidi na mimi mwanaume alikuwa ameuchuna tu
 
Ha ha ha lazma jioni au baada ya wewe kushushwa mke alichimbwa biti:smile-big:
 
Ha ha ha lazma jioni au baada ya wewe kushushwa mke alichimbwa biti:smile-big:

Hiyo lazima itakuwa ilitokea maana wakati tunapiga stori jamaa alikuwa anatuchecki kwenye kupitia kwenye kioo nikasema nikushuka lazima timbwili litaendelea tu
 
Hiyo lazima itakuwa ilitokea maana wakati tunapiga stori jamaa alikuwa anatuchecki kwenye kupitia kwenye kioo nikasema nikushuka lazima timbwili litaendelea tu

Mkubwa wakati tunasubiri waziri mkuu usisahau ile hafla ya kuuaga mwaka itakayofanyikia maeneo ya kwa ODM next month kwa kuchinja mbuzi mzima ambaye budget yake tayari ishatolewa na kuwa approved.
 
Mkubwa wakati tunasubiri waziri mkuu usisahau ile hafla ya kuuaga mwaka itakayofanyikia maeneo ya kwa ODM next month kwa kuchinja mbuzi mzima ambaye budget yake tayari ishatolewa na kuwa approved.

Orait Orait aisee hiyo kitu sijaisahau kabisa iko katika plans zangu siwezi kosa banaa wapwaz wote invitations wanazo?
 
tatizo wake zetu nao hawana story mpya kila siku ni kulalamika tuuuuu...., hakuna jipya.., kwenye gari unakunja sura hakuna kucheka, majibu ya mkato, (sawa.., ulitakaje?..., subiri mwisho wa mwezi.. etc)...... !!!

NB: mi wangu tunacheka mwanzo mwisho.....
 
Ndio maana siku hizi kuepuka hayo mambo unakuta jamaa ana gari lake na wife naye ana gari lake kwahiyo wakiamka asubuhi wamekorofishana kila mtu anachukua hamsini zake kwenye gari huyooo kazini bila bugudha jamaa atapakia kimada huko njiani akiwa anaelekea kazini kimpunguzie machungu ya asubuhi
 
bujibuji thanks umetengeza mchana wangu
Inategemea na mahusiano yenu yakoje.
Upendo ukiwa juu, mkeo anakuwa ni rafiki yako, hutokosa ya kumuongelesha.
Lakini kama penzi limechakachuliwa na nyumba ndogo, basi mke unamuona kama zigo la uding'a.
Muda wa kuongea maongezi matamu unakuwa haupo, unabaki muda wa kulaumu, kutukana na kugombeza.
wewe dume ndio unakuwa perfect muda wote, na mwanamke anakuwa mkosaji muda wote, hata akikuwekea maji ya moto ya kuoga unamwambia mbona kuyaunga tui maji yangu ya kuoga?
kisha unaanzisha zogo
 
Kipya kinyemi japokuwa kidonda

UUuuuuuuuuuwiiiiiiiiiiii, ha ha ha ha ha , shehe waniumiza mijimbavu yangu atiiiiiiiiiiiiiiiiiii......................, sasa na wewe umepewa lift unazua na umbea tena mswahili nae anatabu, ya ngoswe kitwa ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe, labda wamenyimana huko walikotoka, au watoto wamefukuzwa shule na ada haijapatikana nk................................
 
Mihamu tu ndio inayosababisha vituko kwewnye usafiri.
Utakuta mtu yuko na mkewe, halafu macho yake yako juu juu kuchungulia kwenye magari ya wanawake na kuwakonyeza.
Waifu akishtukia, utasikia jamaa akijitetea, ohhh tulikuwa naye JKT kwenye kambi ya pale Kariakoo

Ndio zako nini? mzee wa kuuwa winga kulia na kushoto
 
Na tena huwa ni maongezi ya tabasamu na vicheko kwa kimada ,lakini kama ni wife na husband watu wanauchuna utadhani hawajuani vile :smile::smile::smile::smile::smile:
 
Na tena huwa ni maongezi ya tabasamu na vicheko kwa kimada ,lakini kama ni wife na husband watu wanauchuna utadhani hawajuani vile :smile::smile::smile::smile::smile:
Wanawake ni wakorofi sana especially kama baba anadrive...Lazima atakusahihisha bila sababu njiani!...aaahh... pitia njia ile mi nina haraka bana, mara..aahh si unaona sasa tumezibwa...mara bwana unakimbiza sana, hatuna haraka hiyo!, mara nipeleke kwa nanihino, halafu unifuate baada ya nusu saa!..!
Kwahiyo safari inakuwa full-boring, na at least ukiuchuna unakwepa mambo mengine!
Sifahamu sana kuhusu nyumba ndogo!

Nguli thread yoko nzuri kweli, sijui kwanini watu hawajaichangia vya kutosha.......... hii ni kweli kabisa .......
huku kwetu ....... lakini kwa wenzetu mie naona kidogo tofauti, hata mkiwa mnatoka kwenda kazi asubuhi
unaweza kukuta mtu hata hamuagi mwenzio ....... siku ni ndefu jamani na kurudi jioni salama ni majaliwa
...... kuwa na tabia ya kuagana asubuhi kwa ka-kiss au ka-hug jioni mnapokutana nyumbani hakuhitaji
gharama yeyote. Mie kwa mtazaomo wangu, wanawake wanaweza sana kurekebisha hii issue maana
madume tomeshakaa kipolisi. Ila kama mama akijenga tabia ya ku-hugh/kiss mnapokutana
automatically itakuwa ikijijenga kwenye ndoa. Tatizo wakina dada wakishatinga ndani kila
mtu anakuwa mbabe......................
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom