Sitta juma
Member
- Oct 4, 2016
- 44
- 24
Nauliza mke na Mme mkiachana na mkiwa bado na mtoto mdogo,je nani ànaruhusiwa kuishi na mtoto kisheria!? Kwa kuzingatia umri wa moto na mahari km ilikuwa imetolewa au laa.wenye kujua atueleweshe plsee
Unaposha sheria mkuu ebu tujikite kwenye sheria kuliko nadhariaMtoto atakaa na mama yake mpaka atakapofikisha umri wa miaka 7 then inaamliwa baba amchukue mwanae.japo kama baba anahakika ya matunzo kwa mtoto hata akiwa na umri chini ya hapo anaweza kumchukua mtoto.mimi niliwahi kubeba mtoto wangu akiwa na miaka miwili na leo hii ana miaka 19.
Thanks for clarifications, lakin jikite kwny sheria iliyopo No. 21/2009 Affiliation is repealled one.Unaposha sheria mkuu ebu tujikite kwenye sheria kuliko nadharia
Sheria ya ndoa inahusu zaidi wana ndoa na watoto waliopatikana ndani ya ndoa. Kwa wale ambao hawapo kwenye ndoa, bado sheria inatambua kuwa mtoto ni mali ya Baba. Kwa mfano sheria ya "Affiliation" inampa haki mama wa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa au aliekwishazaliwa kuwasilisha ombi maalumu katika mahakama (Mahakama ya Wilaya) kutaka utambuzi wa baba wa mtoto husika na kumtaka baba huyo (putative father) kutoa matunzo kwa mtoto aliyezaliwa ambaye kwa mujibu wa sheria hii anatambulika kama mtoto haramu (illegitimate child). Matunzo kwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa (out of wedlock) yanaweza kukoma ikwa baba wa mtoto ataiomba mahakama ifanye hivyo kwa kuthibitisha kuwa mtoto ametimiza miaka 14 au mama husika wa mtoto ameolewa au kuingia kwenye mahusiano ya "ki unyumba (cohabitation)" na mwanaume ambaye alikuwa ameacha.
Kwa hiyo kwa mjibu wa sheria ya Ndoa ni sawia kuwa mtoto akiwa na umri usiozidi miaka saba (7) akakaa kwa mama na baba atawajibika kutoa matunzo ya motto mpaka kwenye umri huo. Lakini uzoefu umeonyesha kuwa akina mama wengi wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuchuma kupitia mgongo wa mtoto. Utakuta mama ameolewa na mume mwingine au yupo nje ya eneo ambalo mtoto yupo anapiga "uchangu" na ana mbwaga mtoto kwa bibi au ndugu, lakini bado anataka apewe matunzo ya mtoto huyo ambayo hayamfikii mtoto.
Kanuni ya jumla ni kwamba baba ndie mwenye mtoto. Mtoto anakuwa kwa mama pale tu mazingira ya ustawi wake (walfare of the child) yatapothibitishwa kuwa yatalindwa na kumwezesha mtoto huyo kukua vyema.