Wajameni tujadili hili kwa maana inaonekana ndoa kwa sasa ni mjukuu au zilipendwa hebu tushauriane shida nini ??
Mbona mmekata tamaa haswa wanaume??
Tatizo nini??
Kwanza hebu tutafakari maandiko haya ya kibiblia; Zaburi 12: 4) Mke mwema ni taji na fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.
Mithali 14:1 Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Mithali 25:24 Afadhali kuishi pembeni juu ya paa, kuliko kuishi pamoja na mwanamke mgomvi.
Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa.
Naam. Sifa za mke mwema ni pamoja na hizi zifuatazo;
Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima.
Huamka kabla ya mapambazuko akiitayarishia jamaa yake chakula na kuwagawia kazi watumishi wake.
Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua, na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu na kuimarisha mikono yake.
Hutambua kwamba shughuli zake zina faida; hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
Husokota nyuzi kwa mikono yako mwenyewe, kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
Huufungua mkono wake kuwapa masikini, hunyosha mkono kusaidia fukara.
Huwahofu watu wake ijapo baridi ya kipupwe, maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
Hujitengenezea matandiko, mavazi yake ni zambarau ya kitani safi.
Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza, huwauzia wafanyabiashara mishipi.
Nguvu na heshima ndizo sifa zake, hucheka afikiripo wakati ujao.
Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa ukarimu.
Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake, kamwe hakai bure hata kidogo.
Watoto wake huamka na kumshukuru, mumewe huimba sifa zake.
Husema, “wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu, lakini wewe umewashinda wote”.
Madaha huhadaa na uzuri haufai, bila mwanamke amchaye Mwenyezi Mungu atasifiwa.
Jasho lake lastahili kulipwa, shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.