Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,095
- 79,493
MWANANGU, MPENDE MKE WAKO NA MHESHIMU MAMA YAKO.
Na. Robert Heriel.
Usichoke kusikia Maonyo ya Baba yako. Mimi ndiye nikupendaye. Naye Mungu atakupa maisha yenye furaha na amani siku zote za maisha yako.
Hakuna maisha mazuri bila kuwa na mke mwema. Mke mwema ni zawadi kutoka kwa Mungu. Huyo ndiye atakayekupa furaha ya moyo wako.
Mke mwema ni zaidi ya Utajiri. Ni zaidi ya kileo. Ni zaidi ya mapambo. Basi ukimpata kamwe usijemhuzunisha moyo wake.
Basi najua yakuwa zitakuja zama ngumu katika mahusiano yako. Zama hizo zitapima msimamo wako na maamuzi yako.
Katika zama hizo litatokea jaribio la kukupima kuwa ni yupi umpendaye kati ya Wazazi wako na Mke wako. Nimemtolea mfano Mama kwa kuwa yeye ndiye apendaye kupendwa na huenda anastahili jambo hilo.
Kama itatokea jambo hilo basi usihofu wala usipate tabu. Nisikie Mimi niliyebaba yako. Mimi nikupendaye sana.
Mpende Mke wako kuliko mtu yoyote yule. Mpende kuliko Mama yako. Mpende kuliko hata mimi Baba yako. Kuliko kaka wa Baba yako au mama yako.
Najua Mama yako ambaye ni mke wangu atataka umpende yeye kuliko mke wako. Kamwe usifanye hivyo. Wala mama yako ambaye ni mke wangu asikuhadae wala kukudanganya. Wala asije akakutishia kwa maneno yake. Akikuambia yeye ndiye aliyekuzaa na kukubeba tumboni miezi tisa. Usiogopeshwe na Maneno yake. Bali mwambie Ahsante kwa kunizaa na kunilea. Tena Ahsante Mama yangu kwa kunifanya hivi nilivyo. Ninakupenda na kukuheshimu. Lakini masuala ya Mimi na Mke wangu tafadhali naomba uniachie mwenyewe.
Nakuambia haya kusudi usije ivuruga amani ya moyo wako. Walakini jichunge uongeapo na Mama yako ambaye ni mke wangu. Usimkaripie wala kumfokea. Usithubutu kumpiga wala usionyeshe kumpuuza kwa maana huyo ni mama yako. Ni bora ujiepushe na shari zake kwa kuondoka bila kusema lolote. Tena mwambie kuwa mtazungumza jambo hilo wakati mwingine kwani muda huo kuna mtu unaenda kukutana naye. Nawe atakapo kuruhusu uondoke kisha umsahaulishe kwa mbinu nilizokupatia. Umtumie vizawadi vya hapa na pale. Ili akuache na asikuseme kwa mabaya.
Mke ndiye umpende kuliko Mama au mimi Baba yako. Huyo ndio mwili wako. Huyo ndiye atakaye kuzalia watoto wako na kukuundia ukoo wako. Huyo ndiye atakaye kula kiapo cha kifo kwa ajili yako.
Kumbuka Mama yako alikula kiapo cha kifo na Mimi Baba yako wala sio wewe. Upendo wangu kwa mama yako unatosha. Wewe unachopaswa ni kumheshimu na kuniheshimu na mimi Baba yako.
Mke mwema ni zaidi ya jambo lolote hapa duniani. Mpende kuliko Mama yako.
Mwanangu, Imezuka tabia katika zama hizi kuwa Wanaume wanawapenda zaidi wazazi kuliko wake zao. Jambo hilo ni kinyume na amri ya Mungu wa Baba yako.
Kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa Kusema; Waheshimu Baba na mama yako, Siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upeweyo na BWANA, Mungu wako.
Unapaswa kuniheshimu Mimi na Mama yako na si kunipenda kuliko Mke wako. Usiogope kufanya jambo hili. Mungu wa Baba yako hatakulaani kwa kumpenda Mke wako kuliko Mama yako bali atakulaani ikiwa humheshimu Mama yako na mimi Baba yako.
Kama alivyoandika Mwanateolojia Paulo katika nyaraka zake. Yakuwa Enyi wanaume wapendani wake zenu kama Yesu alivyolipenda kanisa. Ndivyo upaswavyo kufanya.
Umpende mke wako zaidi kuliko mtu yeyote. Usiogope kufanya hivyo. Nawe ndivyo familia yako itakavyostawi sana. Nawe utanenepa Mifupa na Roho. Utaomba kwa Mungu wa Baba yako naye ataachia baraka katika familia yako.
Naye mke wako atakutii na kukuheshimu kwa kuwa anajua unampenda kuliko mtu yeyote. Ingawa imeamuriwa kuwa Mpende jirani yako kama nafsi yako ilivyo lakini Upendo wa mke na Mume na uzidi zaidi. Tena upendo wa wewe na Mungu ndio uwe zaidi ya yote.
Ikiwa hutanisikiliza mimi Baba yako. Nawe ukampenda Mama au mimi Baba yako kuliko mke wako basi haya yote yatakupa. Utanyanyaswa na mke wako uamkapo na ulalapo.
Mkeo hatajiona kama ni sehemu moja na wewe hivyo atakuchukulia kama watu wengine. Hivyo atakufanyia bila kujali tena bila huruma. Nawe utamgeuza mke wako kuwa Adui yako wewe mwenyewe. Naye atageuza watoto wako watakuwa maadui zako na ndugu zako.
Nawe utakapokuwa mzee na mwili wako kuchoka ndipo atakapo kugeukia na kukutesa na kukusononesha. Nao watoto wako wakuwazaa watakuona kama adui.
Lakini Kama utampenda mke wako. Na kumjali, na kumthamini. Basi utaishi kama Mfalme katika dunia. Naye mke wako atakupenda na kukutii. Nao watoto watakupenda na kukufurahisha moyo wako.
Utazeeka na mke wako atakuhudumia utakapoishiwa na nguvu za mwili. Utakufa katika uzee mwema. Nao watoto watakukumbuka na kukuombea baraka daima. Nao watakusema kwa mazuri uliyoyafanya.
Asikudanganye mtu ukawapenda watoto wako kuliko kumpenda mke wako. Kumpenda mke ni kupenda watoto. Kwani Mkeo atawaambia Watoto wako mambo mazuri uyafanyayo lakini ukiwapenda watoto na usipompenda mke wako. Utakuwa unajihangaisha tuu Mwanangu kwani Mke wako atawaambia watoto wako mabaya yako. Nao watakuchukia hata kama unawapenda na kuwahudumia. Nao watakuchukia bila sababu lakini ukimpenda mke wako basi watoto wako watakupenda bila sababu.
Kumbuka Sheria niliyokuusia. Mpende mke wako kuliko mtu yeyote. Kuliko Mama yako, Kuliko mimi Baba yako. Kuliko watoto wako na ndugu zako. Huyo ndiye mwili wako.
Huyo ndiye aliyekuwa tayari kusimama mbele za watu na kula kiapo cha mauti wakati wengine wakila viapo na Watu wengine. Mpende sana.
Nilikuambia kuwa Mama yako alikula kiapo na Mimi wala sio wewe. Akisema anakupenda ni kweli anakupenda lakini ni kwa sababu wewe ni mtoto wake. Kumbe usingekuwa mtoto wake asingekupenda.
Lakini mke wako amekupenda tuu. Wewe sio kaka yake. Wala hamna undugu lakini amekupenda. Tena ameamua kula kiapo cha kifo kwa ajili yako.
Nina uhakika mimi Baba yako na mama yako kama usingekuwa Mtoto wetu tusingekupenda kama tunavyokupenda.
Msikilize Mke wako kuliko Mama yako. Maana Mama yako hatakusikiliza wewe kama anavyonisikiliza mimi Baba yako. Mimi ndiye mume wake. Nina amri mbinguni na duniani ya kumtiisha mama yako na kumpenda.
Walakini jifunze kuwa kama mwanamume. Utende kama mwanaume. Useme kama mwanaume. Ukijua kuwa kila mtu ananafasi yake katika maisha yako.
Usisahahu yale niliyokuandikia Katika nyaraka zilizopita. Ili usije ukajikwaa. Mungu wa Baba yako atakuwa pamoja nawe siku zote.
Mke mwema ni zaidi ya dhahabu katika maisha yako.
Ni Mimi Baba yako katika Zama zangu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300.