Mke kasaliti ndoa, nifanyeje?

Mke kasaliti ndoa, nifanyeje?

Mchatm

Member
Joined
Aug 1, 2017
Posts
11
Reaction score
5
Habari wadau,

Nina mke na mtoto mmoja na hivi karibuni nimekamata mawasiliano yaliyoonesha kuwa wife ananisaliti na jamaa mmoja hivi nikafatilia vizuri ikawa ni kweli na alikwishatembea nae mara moja.

Nikawa nimemuuliza kama anampenda sana tuachane aende zake wakaishi pamoja lakini akasema kuwa alipitiwa tu na nimsamehe.

Hii sijamshirikisha mtu yeyote kwa familia zetu na nikawa nimemuangalia tu tunaendelea kuishi ila simuamini tena kama nilivyomuamini awali.

Naomba ushauri kwenu wadau nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tafuta dogo doho ambae ni mrembo zaidi yake umgegedee chumbani mwenu..tengeneza mazingira akufumanie
Akiona atajua maumivu ya kuchapiwa na ataacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
utaacha wangapi ndugu ??

kama wewe alikukubalia kwanini awakatae wengine ?
muwekee masharti magumu mnyime muda mbadilishie aina ya simu

kisha mtafute aliyetembea nae ongea nae kiume akiendelea mletee ubabe
 
Habari wadau
Nna mke na mtoto mmoja na hivi karibuni nimekamata mawasiliano yaliyoonesha kuwa wife ananisaliti na jamaa mmoja hivi nikafatilia vizuri ikawa ni kweli na alikwishatembea nae mara moja, nikawa nimemuuliza kama anampenda sana tuachane aende zake wakaishi pamoja lakini akasema kuwa alipitiwa tu na nimsamehe.
Hii sijamshirikisha mtu yeyote kwa familia zetu na nikawa nimemuangalia tu tunaendelea kuishi ila simuamini tena kama nilivyomuamini awali naomba ushauri kwenu wadau nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww hjawahi kchepuka hata siku moja
 
utaacha wangapi ndugu ??

kama wewe alikukubalia kwanini awakatae wengine ?
muwekee masharti magumu mnyime muda mbadilishie aina ya simu

kisha mtafute aliyetembea nae ongea nae kiume akiendelea mletee ubabe
Huyo nilishamtafta na akakili kuwa hataendelea na hiyo kitu ila si unajua tena wakishaonja hawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujawahi kumsaliti hata mara moja tangu uwenae? jifunze kusamehe hakuna mkamilifu duniani mpe nafasi nyengine ..
 
huo ni mgawanyo wa kazi, wewe ukinunua chupi wenzako watakusaidia kuvua, mambo ya ndoa peleka sehemu husika sio kuleta mtandaoni, jifunze kuwa gentleman
 
ushauri wanini tena mkuu fungua bucha mtu..............................
 
Watu mna moyo unasalitiwa na mke na ushahidi unao bado unakuja humu kuomba ushauri, utachapiwa sana maana huna maamuzi ya kiume
 
utaacha wangapi ndugu ??

kama wewe alikukubalia kwanini awakatae wengine ?
muwekee masharti magumu mnyime muda mbadilishie aina ya simu

kisha mtafute aliyetembea nae ongea nae kiume akiendelea mletee ubabe
Kwann ukose amani kwa hayo yote utakuwa huishi kwa amani wakati ndoa ni furaha

Kama katoka nje basi fahamu ataiweje huyo hawezi kuwa muaminifu

Kwann ujipe stress awafuate anaowataka
 
Hizi kesi mbona zimekuwa nyingi hivi?? Tatizo liko wapi?? Tamaa???
 
Back
Top Bottom