Mke kasaliti ndoa, nifanyeje?

Mke kasaliti ndoa, nifanyeje?

Kuchapiwa ni siri ya ndani!! Kung'uta mavumbi, msamehe endeleeni na ndoa!!
 
Habari wadau
Nna mke na mtoto mmoja na hivi karibuni nimekamata mawasiliano yaliyoonesha kuwa wife ananisaliti na jamaa mmoja hivi nikafatilia vizuri ikawa ni kweli na alikwishatembea nae mara moja, nikawa nimemuuliza kama anampenda sana tuachane aende zake wakaishi pamoja lakini akasema kuwa alipitiwa tu na nimsamehe.
Hii sijamshirikisha mtu yeyote kwa familia zetu na nikawa nimemuangalia tu tunaendelea kuishi ila simuamini tena kama nilivyomuamini awali naomba ushauri kwenu wadau nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
mi naomba kuuliza ivi siku izi wanake wanaongoza kwa kusaliti ndoa? sababu haipiti siku hajaja mwanaume umu ndani kulalamika mke ananisaliti.

kama anakusaliti na wewe si ukasaliti, kwani wewe umesalit wangapi ? na ukiona mwanamke kachepuka mwanaume nawe jichunguze,ushaambiwa hapa kazi tu, na hiyo ndo kazi yenyewe...

haloooooooo ccm mbele kwa mbele....
 
huo ni mgawanyo wa kazi, wewe ukinunua chupi wenzako watakusaidia kuvua, mambo ya ndoa peleka sehemu husika sio kuleta mtandaoni, jifunze kuwa gentleman
jibu nzuri, kunywa soda nakuja kulipa.
 
Kwann ukose amani kwa hayo yote utakuwa huishi kwa amani wakati ndoa ni furaha

Kama katoka nje basi fahamu ataiweje huyo hawezi kuwa muaminifu

Kwann ujipe stress awafuate anaowataka
labda kitu kimoja hukitambui
tunatakiwa kuwa na wapenzi au wake ambao hatutakiwi kutumia nguvu kuwa-keep

hili mwanzo aliliweza but huyo mke kashajiona ni mkubwa kuliko ndoa dawa yake ni kumbana ili ajue ndoa ni kubwa kuliko yeye
 
Kwa sisi waislam Mtume Muhammad (S.A.W) alituambia kuwa "Ukizini na Mke/Mtoto/Dada/Mama/Shangazi/N.k wa mwezako jua na wako lazima aziniwe" naomba kukuuliza ndugu wewe hajawai kuzini kabla?
 
Kukushauri ni kazi.Sikiliza moyo wako unavyokeambia.Kiukweli mtu mwenye hiyo tabia kuacha ni vigumu sana na hasa kama huyo anayetembea nae anampa anachotaka ambacho labda wewe hufanyi.Mara nyingi huwa wanarudia, cha msingi jitahidi kumuweka bize kidogo ikiwezekana hata kumfungulia biashara ambayo itamuweka bize asiwaze sana michepuko!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa lako ni kumchunguza, ona sasa unavyohangaika.... Ushauri wangu maana umeshafanya kosa.... Achana na simu ya mkeo
 
Hivi haya majibu mtu unayapokeaje
1.NILIPITIWA TU
2.SHETANI ALINIPITIA
....
.NI MAJIBU YA KIHUNI SANA....Unapitiwa ukigongwa kwenye sherehe huko but unatongozwa na mnapanga mkutane mnakutana then unaniambia ULIPITIWA......???
Hakuna jibu nitakalolipokea zaidi ya kukupa chako na usepe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi waislam Mtume Muhammad (S.A.W) alituambia kuwa "Ukizini na Mke/Mtoto/Dada/Mama/Shangazi/N.k wa mwezako jua na wako lazima aziniwe" naomba kukuuliza ndugu wewe hajawai kuzini kabla?
kwahiyo maana yake itakuwa amezini na mke wa mtu huyu
 
1. Do not pretend, listen to your heart ... respond to your natural instinct
2. Chambua sababu sababishi na kama zimechangiwa na wewe kutotekeleza wajibu wako kama Mume na akaomba msamaha kutoka moyoni then huna budi kumsamehe.

We only live once na hakuna binadamu aliyekamilika
 
Back
Top Bottom