Ni mmoja kati ya walioitwa kutoa ushauri baada ya mwanaume kugundua bosi wake ni mchepuko wa mkewe na kazi anayoifanya aliombewa na mke wake.
Story iko hivi
Jamaa alikuwa na kazi nzuri na maisha ya mtanzania wa kati, Mkewe alikuwa akisimamia mradi aliofunguliwa na jamaa.
Baada ya Kazi kubuma jamaa aliamua kukaa nyumbani na kuacha mke aendelee kuiendesha familia Kwa mradi wa jamaa.
Siku zilienda jamaa akawa anapokea malalamiko kutoka Kwa mke kuwa hatafuti pesa, kazi yake ni kukaa tu.
Siku zimeenda mke akaja na taarifa nzuri ya kumpatia jamaa kazi nyingine nzuri kuliko ya mwanzo.