Mke kaiba fenicha zangu na kupangishiwa na baba mkwe, na baba mkwe anataka kunifunga jela

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Wanajamvi, maoni yenu tafadhali.

Mchana nilimtaarifu mke wangu kuwa usiku nitahitaji huduma, akadai kuwa vidonge siku hizi vinamkosesha hamu ya kula n.k. hivyo akachome sindano, nikampa hela na akaenda hospitali.

Jioni tukakwaruzana kwa swala la hausigeli kuchelewa kurudi nyumbani baada ya kutumwa. Hali hiyo ilizua taharuki baada ya mke wangu kumuuliza binti yuko wapi na hatoi majibu, basi tukalala hatuongei.

Usiku mimi nikataka penzi, ile kumwamsha akadai yuko period, nikamwambia basi nipe hela niliyokupa ukachomee sindano maana ulinidanganya, akadai hela hana. Nilijisikia hasira kwasababu ameniongopea kuhusu pesa yangu, lakini pia anataka kucontrol mambo ya chumbani,hivyo nilimshushia ngumi moja ya kichwa, akaamka kama amewehuka, makelele kibao kasha akakimbilia kwa mpangaji jirani, ni bibi.

Ilikuwa saa 7 usiku, baba akaja kunisihi na mke akaingia ndani huku akikusanya nguo zake akidai anaondoka akalale sebuleni, aliendelea na kauli chafu nikamshushia ngumi ingine matata, akakaa kimya, akalala sebuleni.

Kulipokucha, kumbe alishaondoka alfajiri pamoja na Smartphone yangu na ufunguo wa nyumba, ukweni ni mtaa wa 3. Nikaenda kwao kwa niaba ya kuchukua simu na ufungua lakini baba mkwe akanisukumia nje kama mbwa. Nilighadhabika, pia simu ilikuwa na appointment muhimu kuliko kito chochote kwa siku hiyo. Nikaenda kupiga viroba kadhaa, nikanunua panga jipya na kuwarudia. Aisee, mama mkwe alivyotaharuki nilicheka sana kimoyomoyo lakini lengo ilikuwa kuwapiga mkwara wanipe simu yangu.

Baba mkwe akaninyemelea kwa nyuma na kuninyakua panga, nikawa nimeishiwa ujanja, nikajiondokea zangu. Nilirudi nyumbani nikachoma nguo zote mke wangu hadi mafuta ya kujipaka, yaani kila kitu chake nikapiga petrol.

Jioni nikaletewa barua ya wito wa Polisi ati niende kesho asubuhi nasubiriwa vinginevyo nitafikishwa mahakamani, mimi kulipokucha nikabadili kitasa (maana aliondoka na ufunguo ), nikabeba begi la nguo na kusepa. Baadae nikaanza kutukanana nao kwa simu; mkwe, mke, polisi na wote wanaomsapoti huyu mke niliyemtaraki kwa staili hiyo, nikabadili na namba na simu.

Sasa, yupi mwenye makosa? Ingawa najua laiti ningevumilia kunyimwa penzi usiku ule, yasingefika hapa, pia ningeamua kutoifata simu yangu, yasingefika hapa. Pia na yeye angekubali kutekeleza wajibu wake chumbani (ikumbukwe nimemuandaa tangu mchana), yasingefika hapa. Na angekuwa mtiifu na kutonijibu kuntu jioni ile kuhusu hausigeli, yasingefika hapa.

Mkwe kaapa kunifunga, kunibambikia kesi. Nimerudi juzi kati, nikakuta walivunja nyumba na kuchukua kila kitu hadi ndala za chooni, labda walidhani nitawafuata tena. Mwanamke kapangishiwa na baba mkwe kwa fenicha zangu.

Ndo hivyo sasa polisi nina RB, je ni salama nibaki hapahapa Dar nianze maisha upya under hidden identity au nivuke boda? Nipe mchango wa mawazo, kunikosoa hakutanisaidia maana sikuomba yanipate haya majanga.
 
Pole.kaombe msamaha ndo uhame nchi
Huyo mke kakuvumilia mengi zaidi ya haya unayo simulia

Hv kuchoma sindano si elfu tatu?? Ndo upige mke mkweli??

Una hasira kali jifunze pia kuishusha
 
hizo sindano ndo sindano za kuzuia mimba? kumbe kuna utaratibu huo pia kila ukitaka mchezo uchome au inakuwa ya muda gani mmh
 
Aise sina cha kukushauri ili uishi kwa Amani ni vyema ukareport polisi uelezee kila kitu, hiyo kesi inaweza kusuluhishwa hapo hpao kituoni kama yakifamilia. ila sikku utakayokwenda kureport hakikisha unakwenda na ndugu zako, au wazee wako na pia umfahamishe boss wako kazini ili hata kama utawekwa ndani siku 2 au 3 itakuwa hujapoteza kibarua. au pia unaweza usireport kituoni lakini ukatafuta wazee watu wazima ukaenda kuomba msamaha yakaisha.
 
hizo sindano ndo sindano za kuzuia mimba? kumbe kuna utaratibu huo pia kila ukitaka mchezo uchome au inakuwa ya muda gani mmh
Kwa nilivyo muelewa ni sindano za kuzuia mimba

Ila mama alikosa mzuka kutokana na kutumia vdonge hvyo akawa anataka ajarbu njia nyingneya kuzuia mimba ndo aka opt sindano

Ila mzee kaomba usiku tendo mama anasema yupo blid (wifi kachoka natabia za mume na pili vdonge vna mkosesha hamu)
Ila huyu kaka etu alisahau vyote kichwa cha chin kilipo anza kufanya kaz
 
Wanajamvi, maoni yenu tafadhali:

Mchana nilimtaarifu mke wangu kuwa usiku nitahitaji huduma, akadai kuwa vidonge siku hizi vinamkosesha hamu ya kula n.k. hivyo akachome sindano, nikampa hela na akaenda hospitali.

Jioni tukakwaluzana kwa swala la hausigeli kuchelewa kurudi nyumbani baada ya kutumwa. Hali hiyo ilizua taharuki baada ya mke wangu kumuuliza binti yuko wapi na hatoi majibu, basi tukalala hatuongei.

Usiku mimi nikataka penzi, ile kumwamsha akadai yuko period, nikamwambia basi nipe hela niliyokupa ukachomee sindano maana ulinidanganya, akadai hela hana. Nilijiskia hasira kwasababu ameniongopea kuhusu pesa yangu, lakini pia anataka kucontrol mambo ya chumbani…hivyo nilimshushia ngumi moja ya kichwa, akaamka kama amewehuka, makelele kibao kasha akakimbilia kwa mpangaji jirani, ni bibi.

Ilikuwa saa 7 usiku, biba akaja kunisihi na mke akaingia ndani huku akikusanya nguo zake akidai anaondoka akalale sebuleni, aliendelea na kauli chafu nikamshushia ngumi ingine matata, akakaa kimya, akalala sebuleni.

Kulipokucha, kumbe alishaondoka alfajiri pamoja na Smartphone yangu na ufunguo wa nyumba, ukweni ni mtaa wa 3. Nikaenda kwao kwa niaba ya kuchukua simu na ufungua lakini baba mkwe akanisukumia nje kama mbwa. Nilighadhabika, pia simu ilikuwa na appointment muhimu kuliko kito chochote kwa siku hiyo. Nikaenda kupiga viroba kadhaa, nikanunua panga jipya na kuwarudia. Aisee, mama mkwe alivyotaharuki nilicheka sana kimoyomoyo lakini lengo ilikuwa kuwapiga mkwara wanipe simu yangu.

Baba mkwe akaninyemelea kwa nyuma na kuninyakua panga, nikawa nimeishiwa ujanja, nikajondokea zangu. Nilirudi nyumbani nikachoma nguo zote mke wangu hadi mafuta ya kujipaka, yaani kila kitu chake nikapiga petrol.

Jioni nikaletewa barua ya wito wa Polisi ati niende kesho asubuhi nasubiriwa vinginevyo ntafikishwa mahakamani, mimi kulipokucha nikabadili kitasa (maana aliondoka na ), nikabeba begi la nguo na kusepa. Baadae nikaanza kutukanana nao kwa simu; mkwe, mke, polisi na wote wanaomsapoti huyu mke niliyemtaraki kwa staili hiyo, nikabadili na namba na simu.

Sasa, yupi mwenye makosa? Ingawa najua laity ningevumilia kunyimwa penzi usiku ule, yasingefika hapa, pia ningeamua kutoifata simu yangu, yasingefika hapa. Pia na yeye angekubali kutekeleza wajibu wake chumbani (ikumbukwe nimemuandaa tangu mchana), yasingefika hapa. Na angekuwa mtiifu na kutonijibu kuntu jioni ile kuhusu hausigeli, yasingefika hapa.

Mkwe kaapa kunifunga, kunibambikia kesi. Nimerudi juzi kati, nikakuta walivunja nyumba na kuchukua kila kitu hadi ndala za chooni, labda walidhani ntawafata tena. Mwanamke kapangishiwa na baba mkwe kwa fenicha zangu.

Ndo hivyo sasa polisi nina RB, je ni salama nibaki hapahapa Dar nianze maisha upya under hidden identity au nivuke boda? Nipe mchango wa mawazo, kunikosoa hakutanisaidia maana sikuomba yanipate haya majanga.
wewe unashida tena mm nisingekuweza hata kwa dakika 15 ..

kwanza una gubu...sana nadhani ndo chanzo cha yoote hahaha halafu inaelekea ni mnyanyasaji mlevi tena yule wa wa kuchefua .....
 
Ulipata tatizo dogo sana ila ukatumia akili ya kipuuzi sana kudeal nalo ndio maana linakuwa kubwa kila kukicha. Utaharibu future yako kwasababu ya mambo ya kipuuzi na kukosa busara na ustaarabu wa kawaida.

Duc in Altum
 
Kwa nilivyo muelewa ni sindano za kuzuia mimba

Ila mama alikosa mzuka kutokana na kutumia vdonge hvyo akawa anataka ajarbu njia nyingneya kuzuia mimba ndo aka opt sindano

Ila mzee kaomba usiku tendo mama anasema yupo blid (wifi kachoka natabia za mume na pili vdonge vna mkosesha hamu)
Ila huyu kaka etu alisahau vyote kichwa cha chin kilipo anza kufanya kaz
Yeah anaonekana katili sana kumpa mwanamke konde zito kisa amekataa dah! ni wazi mapenzi zero, mana tabia ya mapenzi hata kama huna hamu ukimpata mtu akakuhamasisha vizuri hata kama hutampa leo basi japo siku ya pili, inaelekea huyu anagegeda kama kuku anarukia tu, kumpa 3000 ya sindano sio maandalizi tosha yakumgegeda kiasi ufanye una haki yakumdunda.
 
kumbe ndo mana siku hizi watu hawataki kuoa
yaan nimeshangaa ukitaka PAPUCHI ya mkeo mpk uanze kujaza form ya maombi tangu mchana ama sivyo utaisikia kwa jirani
inaonesha wewe jeuri mkeo ana adabu mixer kusudi BABAMKWE mtu mzima hovyo na huyo askari ni POLICE KIDORE ndo maana mmetukanana weee mpka simu zimeisha charge
km ni mkeo wa ndoa huna budi kurudi na kuomba msamaha ili yaishe maisha yaendelee
lkn sijajuq hiyo ndoa ni ya KIKRSTO au ya KIISLAMU
 
Wanajamvi, maoni yenu tafadhali:

Mchana nilimtaarifu mke wangu kuwa usiku nitahitaji huduma, akadai kuwa vidonge siku hizi vinamkosesha hamu ya kula n.k. hivyo akachome sindano, nikampa hela na akaenda hospitali.

Jioni tukakwaluzana kwa swala la hausigeli kuchelewa kurudi nyumbani baada ya kutumwa. Hali hiyo ilizua taharuki baada ya mke wangu kumuuliza binti yuko wapi na hatoi majibu, basi tukalala hatuongei.

Usiku mimi nikataka penzi, ile kumwamsha akadai yuko period, nikamwambia basi nipe hela niliyokupa ukachomee sindano maana ulinidanganya, akadai hela hana. Nilijiskia hasira kwasababu ameniongopea kuhusu pesa yangu, lakini pia anataka kucontrol mambo ya chumbani…hivyo nilimshushia ngumi moja ya kichwa, akaamka kama amewehuka, makelele kibao kasha akakimbilia kwa mpangaji jirani, ni bibi.

Ilikuwa saa 7 usiku, biba akaja kunisihi na mke akaingia ndani huku akikusanya nguo zake akidai anaondoka akalale sebuleni, aliendelea na kauli chafu nikamshushia ngumi ingine matata, akakaa kimya, akalala sebuleni.

Kulipokucha, kumbe alishaondoka alfajiri pamoja na Smartphone yangu na ufunguo wa nyumba, ukweni ni mtaa wa 3. Nikaenda kwao kwa niaba ya kuchukua simu na ufungua lakini baba mkwe akanisukumia nje kama mbwa. Nilighadhabika, pia simu ilikuwa na appointment muhimu kuliko kito chochote kwa siku hiyo. Nikaenda kupiga viroba kadhaa, nikanunua panga jipya na kuwarudia. Aisee, mama mkwe alivyotaharuki nilicheka sana kimoyomoyo lakini lengo ilikuwa kuwapiga mkwara wanipe simu yangu.

Baba mkwe akaninyemelea kwa nyuma na kuninyakua panga, nikawa nimeishiwa ujanja, nikajondokea zangu. Nilirudi nyumbani nikachoma nguo zote mke wangu hadi mafuta ya kujipaka, yaani kila kitu chake nikapiga petrol.

Jioni nikaletewa barua ya wito wa Polisi ati niende kesho asubuhi nasubiriwa vinginevyo ntafikishwa mahakamani, mimi kulipokucha nikabadili kitasa (maana aliondoka na ), nikabeba begi la nguo na kusepa. Baadae nikaanza kutukanana nao kwa simu; mkwe, mke, polisi na wote wanaomsapoti huyu mke niliyemtaraki kwa staili hiyo, nikabadili na namba na simu.

Sasa, yupi mwenye makosa? Ingawa najua laity ningevumilia kunyimwa penzi usiku ule, yasingefika hapa, pia ningeamua kutoifata simu yangu, yasingefika hapa. Pia na yeye angekubali kutekeleza wajibu wake chumbani (ikumbukwe nimemuandaa tangu mchana), yasingefika hapa. Na angekuwa mtiifu na kutonijibu kuntu jioni ile kuhusu hausigeli, yasingefika hapa.

Mkwe kaapa kunifunga, kunibambikia kesi. Nimerudi juzi kati, nikakuta walivunja nyumba na kuchukua kila kitu hadi ndala za chooni, labda walidhani ntawafata tena. Mwanamke kapangishiwa na baba mkwe kwa fenicha zangu.

Ndo hivyo sasa polisi nina RB, je ni salama nibaki hapahapa Dar nianze maisha upya under hidden identity au nivuke boda? Nipe mchango wa mawazo, kunikosoa hakutanisaidia maana sikuomba yanipate haya majanga.
Nimekuona wa hovyo sana, na wewe ni kiongozi wa familia?!
 
Umejibu kwa hisia kali..ha ha ha ha
hahahaha kwa maelezo ya huyu mleta mada haaaaaaaaaaaaaaa tungeshatoana ngeu saa nyingii anaelekea ana matatizo akiamua halali home akiamuahatoi hela ya kula tena ni yule anayeweza kumvua mkewe nguo mtaani bila haya
 
hapo ushaharibu ishu ya kufanya ni kutafuta wazee wastaarabu waende kwa mkwe ingawa sio rahisi kueleweka lakini kwa muda wanaweza wakaafikiana,au kama vip tumia plan B nenda direct polic hiyo ni ndoa jishushe nna uhakika yataisha kuna watu wanafanyiana vitendo vya hatari na yanaisha huyo mkwe asikutishe kama kufungana rahisi hivyo magereza yangekua kama maduka kwa uwingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom