Mke huyu ni balaa jamani!

@mtambuzi
Unajua unapoteza mapato na hizi story zako
Ungana na Shigongo kwenye riwaya au anzisha viarida vya stori fupi fupi hata ukiuza sh.2000 utapata faida kubwa.

Acha masihara bana................. Unajua wewe ni mtu mzima sasa, au huzioni hizo mvi zako kichwani?
 
Pole yake sana....It seems mke wake anashindwa kutambua majukumu yake kama mwanamke ndani ya nyumba,ndio maana anakuwa limbukeni wa kupenda vitu vikubwa bila kuangalia hali yake jamaa kiuchumi. Na jamaa so far mapenzi yashashuka maana mpaka wazo la kuacha limeingia kichwani....Kama atashindwa kuyatatua mwenyewe ayapeleke kanisani.. Ila asipoangalia mkewe atazidi kumrudisha nyuma kimaendeleo kila siku..na ikitokea amefukuzwa kazi..baaaaaasi,mke ndo bye-bye tena.
 
Hebu wana JF fungukeni hapa, nimshauri nini huyu mwenzetu mbaye ndoa yake inaonekana kumuelemea?

Mbona pole zake!
Sasa tukifunguka si ndio rafiki yako atajinyonga maana ataona kapata laana!
Ila cha kuuliza - kwani alimpatia wapi huyo mke? Hakumchunguza kujua hulka zake?
Sitaki kuamini huyo mdada/mmama amekuja kubadilika ghafla.Kama kabadilika ghafla, ni kwanini?
 
  1. hiyo tabia ameianza katika hiyo miaka mitano yote au ni karibuni??
  2. yeye na mkewe mahusiano yao yakoje (wanaweza kukaa na kuongea?)
 
Si ana biashara bwana, haina haja kuumizana vichwa..Chukua watoto peleka boarding, alaf home kila mtu ajitegemee kwa mahitaji, kuanzia misoc n evrthn! OVER...

Safi sana....ila anaweza anza kuuza kitumbua chake akisingizia humtunzi
 
Mbona pole zake!
Sasa tukifunguka si ndio rafiki yako atajinyonga maana ataona kapata laana!
Ila cha kuuliza - kwani alimpatia wapi huyo mke? Hakumchunguza kujua hulka zake?
Sitaki kuamini huyo mdada/mmama amekuja kubadilika ghafla.Kama kabadilika ghafla, ni kwanini?

Anadai mabadiliko yalianza taratibu mwendo kama kinyonga, na ghafla graph ikapanda....................
Nimeeleza wazi kwamba alimpa mimba kiwa form four na ndipo akalazimishwa kumuoa na baab wa binti.
 
Anadai mabadiliko yalianza taratibu mwendo kama kinyonga, na ghafla graph ikapanda....................
Nimeeleza wazi kwamba alimpa mimba kiwa form four na ndipo akalazimishwa kumuoa na baab wa binti.

mkuu hapo ndipo tatizo lilipoanza kwani naamini mwanamke amejiweka kwenye nafasi ya kutokufanywa lolote na inawezekana ameshajielewa ni kiasi gani mapenzi aliyonayo kwa mwenzake.. kingine ile dhana ya kwamba ndoa ililazimishwa kutokana na ujauzito nalo linachangia ..

kifupi ndoa inapokuwa na sababu ya tatu katika kufungwa huwa inakuwa ni tatizo tayari
 
@mtambuzi
Unajua unapoteza mapato na hizi story zako
Ungana na Shigongo kwenye riwaya au anzisha viarida vya stori fupi fupi hata ukiuza sh.2000 utapata faida kubwa.

Kwa taarifa yako Mtambunzi ni level nyingine,nakuomba usimlinganishe na udaku wa akina Shigongo,maarifa aliyonayo huyu mtu yanatosha kabisa kurekebisha matatizo ya familia hiyo....kinachohitajika ni huyu mleta mada kuonyesha ushirikiano.
 
Huo ni msalaba, ukubali kama ni msalaba wako kisha ubebe kwa akili, utafanikiwa kuuona hauna uzito.

Usikate tamaa wala usijione mnyonge kwake, jipe ujasiri na uwe muda tulivu na kuongea naye kuhusu furaha ya maisha yenu ya ndoa na malengo yenu ya baadae. Wakati wa maongezi jitahidi kuwa mvumilivu maana anaweza kukujibu hovyo kwa kuwa ndio tabia yake, jitahidi sana kumuelimisha na kumuonyesh nia yako ni kupenda muishi kwa raha kwa kusaidiana kutokana na mnachopata.

Inawezekana huyo mkeo ni mgumu kuelewa hali halisi ya ugumu wa maisha. Pengine hata hilo duka hajui kwa nini ulimfungulia wala hajui umuhimu wake na hajui nini wajibu wake kama mwanamke ndani ya nyumba. Inawezekana ulimjengea maisha ya kukutegemea na kwamba wewe unaweza kila kitu na yeye hana lolote la kufanya zaidi ya kujiona ni malkia mwenye bahati kuliko wengine!
 
mkuu hapo ndipo tatizo lilipoanza kwani naamini mwanamke amejiweka kwenye nafasi ya kutokufanywa lolote na inawezekana ameshajielewa ni kiasi gani mapenzi aliyonayo kwa mwenzake.. kingine ile dhana ya kwamba ndoa ililazimishwa kutokana na ujauzito nalo linachangia ..

kifupi ndoa inapokuwa na sababu ya tatu katika kufungwa huwa inakuwa ni tatizo tayari

Kumbeeee eh!........... nishapata pa kuanzia sasa.......................
 
Story ndefu ila inasikitisha. Pole sana ila hapo ilipofikia ni pagumu. Kaza moyo ufanye maamuzi magumu
 
Kumbeeee eh!........... nishapata pa kuanzia sasa.......................

pia hata mwanaume inawezekana alipata athari kisaikologia na alikuwa anaamini si chaguo lake na inawezekana pia akawa ndo chanzo cha tatizo .. pia anaweza kuwa amepata mtu (mwanamke) mwingine kwake anaamini ndo chaguo lake hivyo kapata sehemu cha kulinganishia , na kwa kuwa alikuwa tayari anaamini si chaguo lake hivyo amejikuta anatunza madhara badili ya kurekebisha..
 
duu kweli pole cna ila mi cjaolewa ila nahisi kama na ww umezidi upole cna
hebu jaribu kuwa ukali kidogo na umweleze hali halisi ya maisha
jaribu kununua kila ki2 muhumu ndani ya nyumba ila hela ya ma2mizi uache kidogo
na pia hebu jaribu kuupuuzia wakati mwngne
ikishindika jaribu kumtishia kumuacha na utoweke kama wiki ivi kama anakupenda ajajirudi mwenywe
kwanz amekujua ww ni unamuogopaa ndo maan anaketasa pole cna baba yangu
 
pia hata mwanaume inawezekana alipata athari kisaikologia na alikuwa anaamini si chaguo lake na inawezekana pia akawa ndo chanzo cha tatizo .. pia anaweza kuwa amepata mtu (mwanamke) mwingine kwake anaamini ndo chaguo lake hivyo kapata sehemu cha kulinganishia , na kwa kuwa alikuwa tayari anaamini si chaguo lake hivyo amejikuta anatunza madhara badili ya kurekebisha..

Nilimuuliza kama ana udhaifu gani ambao mkewe huwa anaulalamikia mara kwa mara, yeye akadai kuwa yeye ni chakaramu sana na anapenda sana kujichanganya na watu wa rika zote, wake kwa waume kitu ambacho mkewe hapendi na kinamkera........... Ni kweli, jamaa anayo tabia hiyo kwa kuwa mimi ni rafiki yangu wa muda mrefu, namfahamu kitabia. sina uhakika kuhusu kuisaliti ndoa yake kwa sababu siko karibu naye saaana kama zamani kabla hajaoa.

Kuna wakati anadai mkewe alimwambia waziwazi kuwa anajisikia hayuko salama katika ndoa yake kutokana na tabia yake ya uchakaramu na kujichanganya na watu wakiwemo wanawake na wanaume...................na yeye anadai hawezi kuiacha tabia hiyo kwa sababu ameshazoea kucheka na watu bila ubaguzi.
 
  • Thanks
Reactions: BPM
Wanazuoni wa Kujamiiana (Sociologists) wanasema kwamba if you tell others about your problem; 1/3 WILL ignore, 1/3 will lough at you and 1/3 have many more problems unlike yours...mimi hapa itabidi nipite tu........
 
du nimechoka,
huyu mke wake kimeo haswa
cha msingi asiwe anampa tena hela za matumizi anunue kila kitu aache hapo na ambane mkewe ampe aultimutum kila mwezi alete hela fulani kuchagia pale nyumbani na afanye stock cheking ktk hiyo business aangalie hela zinaenda wapi
akiwa anasafiri asimpe hata sent,na watoto yeye mwenyewe amue wasome wapi sasa kwani yy ndio kichwa cha nymba
uhuru alompa mkewe ameuharibu inabidi awe dikteta sasa ili ndoa iendelee.
 
kwakuwa ni mkirsitu pita katika duka la vitabu pale posta mpya kanisa katoriki ulizia kitabu kimeandikwa ndoa yangu kitakusaidia sana pengine kupata ushauri mnzuri zaidi wakumueleza wengi tunakutana na matatizo kama haya na makosa ni yetu tokea tunaanza uhusiano matokeo yake tunapata galama kubwa mbele ya safari na hii huanza mnapokuwa mmezaa watoto
 
Hata mimi hilo tatizo la upole wa mume nimeliona, jamaa ni mpole sana na ana muogopa mkewe kupita kiasi, kwa kifupi naweza kusema ameshikwa hasa.................
Sasa ikiwa huyu bwana yuko hivyo, anaonesha amekuwa sikio la kufa.
Si ajabu hata ukimshauri ataenda kumwambia mkewe kuwa Mtambuzi ameniambia hivi na vile. Hayo mengine yote anayodai "eti kwao mkewe hakuna wa kumkalisha chini, mama ameshindwa na watoto aliozaa mwenyewe", ni visingizio tu vya kuhalalisha upole wake. Atendelea kukulalamikia kwa sababu yamemfika shingoni, lakini nina wasiwasi yeye mwenyewe anamwogopa mkewake.

Kama ana ubavu, mwambie anatakiwa kutawala hapo nyumbani kwa mkono wa chuma mpaka mambo yataporejea katika hali ya kuvumilika.

Talaka sio busara, lakini kama ufumbuzi wa mwisho talaka inaruhusiwa pale ambapo ndoa inakuwa karaha badala ya raha. Kwa ufupi kazi ipo!
 
Umeona eh! Mimi nilijaribu kumwambia kuwa kila jambo linatakiwa kuwa kwa kiasi, hata upole una kiasi chake................. nilimshauri awe mkali japo kidogo na kuwa msemaji mkuu wa nyumba yake................. Alikubali, lakini nina wasiwasi sana na kukubali kwake, hakuonekana kuwa serious..................
 
Back
Top Bottom