Mke huyu ni balaa jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke huyu ni balaa jamani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 21, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mimi ni kama mkimbizi nyumbani kwangu. Kabla ya kuoa, nyumbani kwangu kulikuwa ndio kimbilio baada ya mihaingaiko yangu ya kutwa nzima, lakini tangu nimuoe mke wangu huyu ambaye nimedumu naye kwa miaka mitano sasa, nimejikuta nikiwa ni mkimbizi kwenye nyumba yangu mwenyewe. Ndivyo alivyoanza simulizi yake rafiki yangu huyu maarufu kwa jina la Udandala.

  Mke wangu ni mama wa nyumbani na ili tusaidiane katika kuyakabili maisha, niliamua kumfungulia duka ili aweze kujiajiri. Cha kushangaza, pato halionekani na biashara haiongezeki, kila nikimdadisi sababu ya biashara kuzorota wakati nilimpa mtaji wa kutosha, yeye hukimbilia kuwalaumu majirani wanaoishi jirani na lilipo duka lake kuwa ni washirikina. Mke wangu huyu anapenda sana kutumia muda wake mwingi kunichunguza niko wapi, nafanya nini, na kwa nini, mpaka nakereka kwa kweli. Nikiacha simu mezani, ataichukuwa na kuibofyabofya na kusoma meseji zote na kupekua phonebook ilikuchunguzaina namba gani zenye jina la jinsia ya kike na kuzikariri (ni mzuri wa kukariri namba usipime) na kuwapigia kwa minajili ya kuwaanzishia ugomvi, wakati mwingine hutumia njia za ki-intelijensia ili kujua wanapokaa au wanapofanya kazi na akishajua huwafuata huko huko na kulianzisha.

  Nikienda naye matembezini, kila msichana tutakayepishana naye atamtoa kasoro, na kama ni kwenye Mghahawa au Bar basi atawatoa kasoro wahudumu wote watakaotuhudumia. Kama msichana yeyote anatokea kuniangalia ndiyo inakuwa balaa, maana ugomvi utaanzia hapo kwa maswali ya ajabu-ajabu kama, ‘kwa nini yule msichana anakuangalia sana?' Mimi nakosa jibu, kwa sababu siwezi kujua sababu ya mtu mwingine kuniangalia. Kwa tabia hiyo, mara nyingi tunajikuta tukiwa na malumbano yasiyoisha, badala ya kujadili juu ya maisha yetu na familia yetu au namna ya kuongeza kipato katika familia. Kwa upande wa kipato ninachopata hata hakitoshi kuweka akiba maana mwenzangu bajeti zake ni za juu sana. Hata kama kila kitu kipo ndani lakini matumizi yetu yanafikia kiasi cha elfu 20 kwa mlo wa siku. Ingawa tupo sita ndani ya nyumba, yaani mimi, yeye, msichana wa kazi, mdogo wake na mke wangu (ambaye ameajiriwa hivi karibuni na hajaanza kujitegemea) na watoto wetu wawili wa miaka 7 na miaka 5, lakini mimi na mdogo wake hatuli pale nyumbani mchana kwa sababu tunaenda kazini. Hivi kweli nyumba zote zenye kipato cha kawaida inakuwa hivyo? Kama nikisafiri kikazi na kumuachia laki mbili, hata kama nitakaa kwa siku tano tu, nikirudi nnitaambiwa hela zimeisha na alikuwa anakopa dukani kwake, na hilo deni nitatakiwa kulilipa.

  Anapenda watoto waende shule zenye kuibuka kama uyoga kwa kufuata uzuri wa majengo na zenye majina ya saint... Mtakatifu... English Medium... Academic School bila hata kuangalia pato letu kama linakidhi hayo matumizi. Kwa mfano huyu mwenetu wa kwanza kwa miaka miwili tu ameshamhamisha shule takriban tatu akisingizia kuwa walimu hawajui kufundisha, ha uhamisho huo mara zote unanighrimu, lakini mwenzangu wala hajali.
  Kitu kingine anachonikera zaidi ni kunilinganisha na watu au ndugu anaowafahamu... ‘Ona mwenzako fulani amejenga nyumba kubwa kama nini.' au 'Ona fulani amenunua GX100 mpya kabisa tena kaagiza Japan, lakini wewe umezubaa tu.' Wakati yeye ananilinganisha, lakini tangu nimfungulie hiyo biashara hajawahi hata siku moja kuchangia chochote pale nyumbani zaidi ya kunitaka nimuongeze mtaji kila mwenzi.

  Anashindwa na huyu mdogo wake tunayeishi naye, ni binti mdogo kabisa, lakini kila akipata mshahara anachangia kwa kununua mahitaji ya pale nyumbani, ingawa huwa sipendi afanye hivyo. Huyu mke wangu hajawahi kuwanunulia watoto hata leso au soksi lakini kazi yake ni kunilaumu kila uchao. Kama nikimuhoji kwamba yeye anachangia nini katika familia ananikata kalma na kudai kwamba yeye ni mwanamke na hapaswi kufanya hivyo. Anaenda mbali zaidi na kudai kwamba hata vitabu vya dini vinasema, mwanaume atakula kwa jasho lake na mwanamke atazaa kwa uchungu, ambapo tayari alishatekeleza jukumu lake la kunizalia kwa uchungu watoto wawili, na sasa ni jukumu langu kuhakikisha familia inapata mkate wa kila siku, yeye haimhusu. Kinachonishangaza, yeye anawaita wanawake wengine wasiiolewa kuwa ni Malaya, machangudoa, wachuna buzi, eti ni wawindaji wa waume za watu, ila yeye ni mke mwema kwa mumewe, Hivi waume za watu ndio wakuteswa kwenye ndoa zao wenyewe!? Hivi mapenzi ya kweli ni yapi katika ndoa? Hebu niambie Mzee Mtambuzi, hivi kweli naweza kujivunia ndoa hii yenye mashaka makubwa kiasi hiki?

  Hebu wana JF fungukeni hapa, nimshauri nini huyu mwenzetu mbaye ndoa yake inaonekana kumuelemea?
   
 2. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  me sijui kwa kweli ngoja wa2 wakushauri.................... naona kabeba tatizo moja balaa.
  huruma bure jaman. mpe pole saxa hayuko ndoan bali matatizoni mmh ndoa ndoano haswaaa.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,698
  Trophy Points: 280
  Low self esteem is what is troubling her....................a good husband helps his wife knowing the sources of her gaffes.................not running away like a coward.....................cha kumshauri ni kuwa atambue ana tatizo la kutojiamini na ndiyo maana hutumia muda mwingi kusagia wenzie akifikiri kwa kufanya hivyo basi yeye ataonekana bora kumbe kila kashfa itokayo mdomoni kwake inapima yeye mwenye ni mtu wa namna gani.........
   
 4. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah aisee pole sana, huyo ni mke wa ndoa?
  Dawa ni kumminyia bajeti tu wala usiumize kichwa,piga mahesabu uone sh ngapi inatosha kwa siku then mwachie,KUWA KAUZU ZAIDI YA DAGAA otherwise itakula kwako, hata akilalamika we tulia ila ukimwendekeza atakutesa,haya maisha yanatakiwa kwenda kwa step, ukiwa nyuma kimaendeleo sisi tutakushangaa wewe, after all mwanamke hapaswi kukucontrol hata siku moja, be a GENTLEMAN aisee na hii kitu ilitakiwa uimalize kimyakimya home, atanyooka tu ila kwa kuwa ameona atakachohitaji unamfanyia kwanini asiendelee???? Chukua nafasi yako ya UBABA WA NYUMBA and everythnng will be good.
  Regards*
  b-52
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Duh inapofikia hali kama hiyo ndo huwa nachoka na maisha ya ndoa. Inabidi wamrudie mungu, wawe karibu na mungu katika maisha yao, lakini pia rafiki yako inabidi ajitahidi kufahamu matumizi halisi ya nyumbani ili aweze kuanza taratibu kudhibiti "Flow of money".
  Rafiki yako pia ajaribu kuelewa mwenye kuijenga hiyo familia ni yeye, na mwenye kuibomoa ni yeye. Hivyo ni juu yake kuamua kukaa na kumueleza mke wake hali halisi ya mienendo ya familia yao na kipi alichokuwa anakitegemea wakati wanaoana. Mara nyingi matatizo kama haya yanatokeaga kwa wanawake wasiojiamini kutokana na kukosa elimu ya kiwango angalau cha sekondary.
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi mkuu, binafsi nilikuwa na dhamira ya kutaka kupata nafasi ya kuzungumza na mke wa huyu jamaa pia ili niweze kumsaidia kuliona tatizo alilo nalo, lakini huyu bwana anadai kuwa mkewe ni mkali kama pilipili na kama akijua kuwa amekwenda kutafuta ushauri nje, litazuka balaa na atashutumiwa kwa kutoa siri za ndani, yeye alikuwa anatafuta namna ya kumuacha, lakini anawaonea huruma watoto wake na pia anahisi jambo hilo litamgharimu. nashindwa kukubaliana naye juu ya kumuacha mkewe, naninachotaka ni kujaribu kutafuta namna ya kuwashirkisha hata ndugu wa mkewe kutatua tatizo hilo, lakini hilo nalo anadai ni jambo lisilowezekana, kwani mkewe hata kwao hakuna anayeweza kumkalisha chini. baba mkwe alifariki siku nyingi, na mama mkwe hana kauli wa watoto aliowazaa mwenyewe............... Shughuli ni pevu
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Bi mkubwa wako anaonekana ni mtu mwenye wivu wa kupindukia pia ni mtu mwenye tamaa. Ni vzr kukaa naye na kumulewesha apunguze wivu na kufocus kwenye maisha ikiwemo mradi wa duka uliomfungulia. Unapokutana naye kwa kumuonya hakikisha unamueleza kwa busara, upole na upendo mwingi. Usitumie jazba, utaharibu.

  Too much of anythig is harmful. Wivu ukizidi inakuwa ni kero, na ukikaa kimya ataona kuwa anayoyafanya ni mazuri. Samaki mkunje angali mbichi, akikauka atavunjika.

  Pole ...
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa Bwana Udandala, walifunga ndoa na mkewe kanisani kanisani................ nadhani ni M-lutheran
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,698
  Trophy Points: 280
  kukimbia matatizo siyo suluhishi hata huko anakutaka kwenda atakutana nayo jawabu hapo ni kukabiliana.........sidhani wewe kuingilia kati ni jawabu........nionavyo umpe mbinu jamaa yako za kulitatua tatizo hilo...................huo ni mtihani ambao Mwenyezi Mungu kampa..............akiushinda atafaidi matunda ya ndoa yake akishindwa basi karaha zisizo na ukomo zamsubiria.......
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  huyo mwanamke ni mbinafsi, mchoyo na mwenye tabia mbaya.... hivi kabla hajaamua kumuoa hakuyaona yote hayo?

  huyo mwanaume asimame kama mwanaume, awe mkali maana mkewe ni kauzu, awe na misimamo na aweke taratibu na sheria kwenye nyumba yake
  1.acha kumtoa out, ataatalalamika sana atasema sana lakini acha kama miezi sita hivi
  2. kama una kimtaji biashara fanya mwenyewe usimtegemee mkeo kwa shughuli yoyote ya maendelea
  3.endelea kumuelimisha kadri uwezavyo, inawezekana wewe ni mpole na mkeo keshakujua au umeilea hali hiyo ni vyema ila mwelimishe na akoseapo kuwa mkali kidogo
  4.shule: akihamisha mtoto shule this time mwambie agharamie mwenyewe wewe huna hela, na kama mna akaunti ya pamoja hamisha fedha zote kwenye akaunti yako binafsi, ingawa inauma mwache mtoto akae nyumbani hata mwezi mzima ataona uchungu na kuacha kitendo hicho.

  sijui mkeo ni limbukeni au mfujaji. in short hajali, hakujali wewe wala familia, usimuhusishe sana kwenye maendeleo na akikwambia fulani ana vx mwambie aende kwa huyo mwenye vx akamuoe. punguza upole mkeo huyo ni kauzu kauzu kauzu mbinafsi na mfujaji inabidi uwe imara ili nyumba isonge mbele, usimuendekeze sana
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni maoni mazuri, lakini mke wa huyu bwana ni form four na ana cheti cha compyuta pia............
   
 12. arnolds

  arnolds Senior Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Si ana biashara bwana, haina haja kuumizana vichwa..Chukua watoto peleka boarding, alaf home kila mtu ajitegemee kwa mahitaji, kuanzia misoc n evrthn! OVER...
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280

  Hata mimi hilo tatizo la upole wa mume nimeliona, jamaa ni mpole sana na ana muogopa mkewe kupita kiasi, kwa kifupi naweza kusema ameshikwa hasa................. Alinidokeza kuwa alimpa mimba huyo binti yeye akiwa chuoni na binti akiwa form four, mdingi akamshikia bango amuoe au sivyo atamfunga, mzee alikuwa ni bosi fulani serikalini, jamaa akanywea akajichukulia mke na kuishi naye kinyumba kwa miaka miwili ndipo wakafunga ndoa................. labda lile jinamizi la kulazimuishwa kumuoa binti linamuandama na huenda anatishwa kila akitaka kuchukua hatua.
   
 14. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hapo kaka umenena aisee
  Hakuna kuumiza kichwa hapo abiria chunga mzigo wako
   
 15. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Jamaa kashikwa sana na atateseka sana kwa staili hii
   
 16. A

  Aine JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mwambie huyo mwanamke anione
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280

  ingawa sishauri watu kuachana lakini saa nyingine kero zikizidi hebu akae mbali kidogo, angalau wiki mbili tatu atafakari maisha yake.
  unapotoka kwenye mihangaiko unatarajia urudi nyumbani ukapata faraja na si kero, unatarajia ukabembelzwe na si kutusiwa na kulinganishwa na wanaume wengine, maana sijui kama watoto wanapata malezi yenye maadili mema hapo.......
  mfano kipindi hiki cha likizo anaweza peleka watoto kwa bibi mwenyewe akaenda mkoa hata wiki 2 atulize mawazo atafakari ushauri anaopewa apange mikakati ya kuufanyia kazi, arudi nyumbani. na abadilike sasa, ajenge nyumba yenye principles, asimame kama mwanaume

   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  @mtambuzi
  Unajua unapoteza mapato na hizi story zako
  Ungana na Shigongo kwenye riwaya au anzisha viarida vya stori fupi fupi hata ukiuza sh.2000 utapata faida kubwa.
   
 19. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,
  Dah!mie sina ndoa na hapa naomba niwe msomaji tu,
  But ila kwa aina ya huyo mwanamke mwenzetu kumrudisha kwenye mstari wala haihitaji busara,
  Hapo huyo jamaa avae uso wa mbuzi km hawajuan afanye alichoandika Arnolds hapo juu basi.
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana kwa ushuri wako mzuri, tatizo la huyu bwana ambalo naliona ni kwamba alimpa nafasi kubwa sana mkewe mpaka akamtawala vya kutosha, mimi sipingi mke kumtawala mume hususana kwa maswala ya nnyumbani kwa sababu wanwake ni wazurin kwenye idara hiyo, lakini pale mke anapovuka mipaka na kutumia uhuru huo vibaya, mume anatakiwa kushtuka na kupunguza madaraka mapema sana.............. Pale mke anapofanya atakavyo na mume ukabaki kuwa mtu wa kuumia ndani kwa ndani bila kukemea, hapo ndipo tatizo linapokuwa kubwa na kuleta rabsha kama hizi zinazomkabili huyu rafiki yangu...................


  Ni kweli, ni ngumu san kumshauri mtu amuache mkewe au mumewe, lakini kuna wakti ushuri huo haunabudi uchukue nafasi pale hali inapokuwa ngumu kama hivi............... Kma ulivyosema, hivi ni malezi gani ambayo wanwapa watoto? hapo panatengenezwa bomu lingine la watoto wasio na nidhamu na watukutu kupindukia. Wakati mwingine ni vyema kucukua maamuzi magumu pale hali inapoonekana kutotengemaa........................................

  lakini Je Ukristo unasemaje kuhusu kutengana au talaka?
   
Loading...