Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,694
- 1,772
kumbe inatakiwa akae miaka mingapi ndio apate ujauzito mwingine? lakini mbona ashapona kabisa?miaka miwili? mbona bado bado. ingekuwa alizaa njia ya kawaida sawa..
mimi simlazimishi ila ninachomwambia ni ukweli mtupu na yeye anadai bado sana kupata mimba, ifanyeje? kwani huo muda wa miaka miwili hawezi kupata ujauzito mwingine?ulimuuliza sababu kwanini ataka hivyo akasema je ? Au wewe unataka kulazimisha hata huongei naye unadhani hizi ni zama za mwanaume kuamua tu?
mh! mgumu kumesa lakini!Hukutushirikisha wakati unampa mimba ya kwanza so endelea exparte hivohivo!pia kabla hujatafta nyumba ndogo fikiria ungekuwa ndo wewe umefanyiwa upasua afu jamaa anakupa mimba baada ya miaka miwili tu???hapo huja tuambia ameacha kunyonyesha lini??au ndo broila???vuta subira kaka mpe miaka mingine miwili so far anakupa unyumba haina taabu
Punguza Jazba, kaa naye chini na muulize yeye angependa kubeba mimba mtoto wenu akiwa na umri gani then hapo anaweza kukueleza na kukupa sababu za maamuzi yake. Huwezi kujua labda kuna tatizo la kiafya linalomfanya aone uzito kubeba mimba ...Mimi namshangaa huyu mke wangu! nimezaa naye mtoto mmoja ila alijifungua kwa njia ya upasuaji miaka miwili iliyopita. kwa sasa mtoto keshakuwa mkubwa maana ana umri wa miaka miwili na mimi nilitaka nimpe mimba nyingine ili azae halafu ndio tupange mipango mingine ya maisha.
Cha kushangaza sasa ni kuwa kila ikifika muda wa yeye kupata mimba hukwepa sana ikiwemo kutaka tutumie zana ili asipate mimba. Nishamwambia tupate mtoto mwingine ili tupumzike kabisa ili mwili wake upate nguvu aruie hali yake ya usichana lakini hataki kunielewa ati anataka tuzae mtoto mwingne baada ya miaka mitano! huku si kutaka kunifanya nikatafute nyumba ndogo ya kuzaa nayo ili niweze kujiongezea familia?
Au mwanamke anapojifungua kwa oparesheni inatakiwa akae miaka mingapi ndio apate ujauzito mwingine!
Kwa kweli nashindwa kumuelewa huyu mwanamke!