Rafiki yangu analalamika....,
Ndoa yake na mkewe haina muda mrefu sana , wote wana toka katika familia ya kikristu wa dhehebu la Kiroma na ndipo walipofungia ndoa yao.
Mungu kawajalia watoto na kazi nzuri pia.
Kwa takriban miezi saba sasa, Mkewe ambaye anaelimu na kazi nzuri amekuwa akisali katika moja ya haya makanisa ya "upendo/upako". Alianza kidogo kidogo kwa kuhamasishwa na wenzake sasa amebobea kuliko hata "mama mchungaji", imefikia kiasi cha kuwa kama amerogwa na "neno", kila siku anachelewa kurejea nyumbani toka kazini na mume akimuuliza anamjibu alikuwa kanisani...na akirudi nyumbani ni mapambio tu kwenda mbele,
Kwa siku za jumamosi na jumapili, inakuwa kama mama hayupo kabisa nyumbani na huwaacha watoto na msichana wa kazi akidai yeye yupo kanisani kuiombea familia yake.
Rafiki yangu anasema amejaribu kumsihi sana mkewe amunguze hiyo kasi ya kanisani ili pengine aangalie familia na asiache muda mwingi wa majukumu yake unachukulia na msichana wa kazi. Lakini sasa mke imefikia mahala anasema hawezi kamwe kuacha kanisani hata sekunde moja na ni heri aachike kuliko kupoteza ufalme wa mbingu...na anamweleza mumewe kuwa akizidi kumkera kwa hili la kushinda kanisani itabidi akaombe maombi maalumu ya kufunga kwa ajili yake kwani anaona yeye sasa ni kama ibilisi.....
Hivi hali inapofikia hivi, tunajenga au tunabomoa??...
Nakumbuka hata wakati Kakobe anapamba moto miaka ya 1996-1998 ndoa nyingi zililegalega kama si kuvunjika kabisa, akina mama wengi walichagua kuishi kanisani kwa Kakobe kuliko kushinda na family zao home. Huo mama Ajue kabisa kwamba ndoa ni mungu aliiweka saa anakiuka kiapo chake mwenyewe? anatenda dhambi bila yeye kujijua, nadhani bado mapepo hayajamtoka vizuri anahitaji KUPUNGWA kwa sala na maombi
Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi; bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu: - 1Wakorintho 1:18 Ndivyo biblia inavyosema - ndio maana wengine hawaoni umuhimu wa kuabudu au kusikia neno la Mungu au kumsifu Mungu au kuomba katika nyumba ya Ibada (Kanisani) kwa muda mrefu - siku nzima au hata mkesha (usiku kucha); Kwao kukesha kwenye pombe, clubs, kukesha kuangalia mipira, TVs etc ni sawa ila Kanisani wanaona ni upuuzi
Pia katika Biblia imeandikwa: "LAKINI NATAKA MSIWE NA MASUMBUFU. YEYE ASIYEOA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA BWANA AMPENDEZEJE BWANA; BALI ALIYEOA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII, JINSI ATAKAVYOMPENDEZA
MKEWE. KADHALKA ...................... YEYE ALIYEOLEWA HUJISHUGHULISHA JINSI YA KUMPENDEZA MUMEWE" 1Wakorintho 7: 32-35.
Kifupi ni kuwa watu wengi (Wanaume/Wanawake) wamekuja kumjua Bwana Yesu baada ya kufunga ndoa - (NA JINSI ILIVYO RAHA KUMPATA YESU MAISHANI) wanatamani kuwa na Yesu na kufanya mambo ya Yesu 24 hrs. ili hali wana familia - kwa kweli inabidi tu wabalance -
inabidi MWANAMKE AJIPANGE - TENGENEZA CHAKULA, SAFISHA NYUMBA, HAKIKISHA MAMBO YA NYUMBANI KWAKO YAKO SAWA - KISHA NENDA ZAKO KANISANI HALAFU MWOMBEE SANA MUMEO ILI AKUELEWE KWANI KUPITIA WEWE ANATAKASWA (Bible inasema hivyo)
Wana JF - onjeni muone YESU alivyo mwema ........... kuliko pombe, sigara, uzinzi, mipira, ufisadi, umbea etc. - na Karibuni anarudi tena - sio dini wala dhehebu - ni YESU
Ifike FAMILIA ZISHINDE KANISA (BABA, MAMA NA WATOTO INCLUSIVE) ili wote siku moja TUISHI MILELE NA BWANA

kweli, mara mia, bora washinde kanisani, kuliko wale wanaoshinda bar, kwenye madanguro wakidangura na wanaume wengine, kuliko wale wanaokula supu na mguu wa mbuzi baa wakati watoto wanakula wali au ugali na housegirl. nakwambia, kati ya vitu vyema huyo mama amechagua, ni kukimbilia kwa Yesu,na huyo jamaa ashukuru Mungu tu, kwasababu akimharasi sana huyo mama akarudi nyuma, ataenda kumpata bar anakunywa na wanaume wengine, hapo tena atarudi hapa aje kualamika mke wake kaacha kanisa sasa amekuwa mlevi na mzinzi. asisumbue akili zetu hapa, hili ni jambo la kushukuru wala si kulalamika.
kwa habari ya huyu mama, siamini kama haachi chochote kwaajili ya watoto kama inavyoongelewa hapa, hakuna mchungaji anayeweza kuwaruhusu washirika wake kufanya kitu kama hicho, kwanza hiyo ingekuwa dhambi, na ni kosa la jinai kwa kutokuwapa watoto wako haki za msingi. kwa mama mwenye uchungu wa labour, hawezi kuwatelekeza watoto wake hivyo. hapa huyu jamaa kinachomuuma si mama kutohudumia watoto, ni huyu mama kwenda makanisa ya kilokole. sasa endelea kumharas, atakaporudi nyuma akaenda kunywa mipombe akarudi chakali akakupiga na vibao ndo utakuja tena hapa kutusumbua na maswali yako. huu ni ushauri wa bure, yakikupata usiseme nilikuwa na mdomo mbaya.
Hii kitu ni ngumu sana... Kuna ndugu yangu ana-experience the same thing. Mke wake halali nyumbani anasema anaenda kwenye mikesha. Hajui watoto wamekula nini au wamelala vp, kibaya zaidi hata huyo HG hana, anategemea mtoto wake wa miaka 10 ndio amuhudumie baba yake. Hivi hapa mwanaume akiamua kuoa mke mwingine anaweza kulaumiwa??
hili nalo neno!Jamani sie binadamuhatutabiriki.Kama angekuwa anacheat kwa uzinzi nje ya ndoa angeonekana shetani.anakwenda kanisani bado anamuona mbaya badala ya kumshukuru Mungu.Uliposema for better for worse ni pamoja na situation kama hizi.akae chini na mkewe wazungumze na aaribu kumuelewa na kumuonyesha upendo zaidi.Atabalance muda vizuri ili upande wowote usiathirike.
NB.asimkataze kwenda kanisani,baada ya kitambo akikomaa kiroho atakuwa mke bora sana na hata yeye atapata baraka na ulinzi wa Mungu kupitia mkewe.
Kama huyu Mama ana hausigeli ameula wa chuya. Kama hana, ajiandae kusoma namba kwani watamdaka mumewe huko uraiani. Anamtia mumewe majaribuni - atachoka kusihi....
Heri akakae kanisani kuliko baa. Kuna waume wengi wanachelewa sana kurudi nyumbani wanarudi wamelewa watoto wamewasahau, hao ndio wabaya zaidi.
Heri akakae kanisani kuliko baa. Kuna waume wengi wanachelewa sana kurudi nyumbani wanarudi wamelewa watoto wamewasahau, hao ndio wabaya zaidi.
FL 1 inawezekana huko kanisani ni chakula cha mchungaji ndo maana anachelewa sana kurudi hm,kwa hiyo jamaa(mme) anaambulia mapambio tu.
hilo nalo tulifikrie