Waambie pendaneni, msinyimane π
Chanzo kikubwa cha mchepuko na nyumba ndogo ni kunyimana π
Lakini, miongoni mwa sababu za kukaribisha ndani ya ndoa, maradhi ya fedheha kama vile UTI sugu, gono, kaswende na hata UKIMWI ni kunyimana π
Lakini, pia chanzo cha yatima na watoto wa mitaani, single mothers na single fathers walio hai na afya zao kabisa, ni kunyimana π
Ni vizuri kuketi chini kwa upendo na upole, kubainisha kasoro, tofauti na ukweli wa hali hiyo na hatimaye kusawazishana na kusameheana π
Mpendane, msichokozane! Amani ya bwana iwe ndani yenu. Tendo ni Baraka yake Mungu, amewakirimia katika kushirikiana nae katika kazi ya uumbaji.
Haifai kuchoka, kuwa mvivu au kukataa bila sababu yoyote ya msingi kushiriki kazi ya uumbaji. Kumbuka Mungu yuko katikati yenu katika kazi hiyo, peaneni kwa upendo bila hiyana, msinyimane tafadhali π