Mke analalamika house girl mchawi!

Mke analalamika house girl mchawi!

NATA.......ninayaheshimu mawazo yako sana mdogo wangu. Ninapenda unavyoainisha mambo.

Pamoja na kuwa mama anaweza akawa alijisahau kimajukumu (na hata kihaiba-ya wajibu wake kama mke, mpenzi wa huyo mume) bado kutembea na msichana wa kazi ni makosa hakujustify kwa baba kuwa na mahusiano na dada wa kazi. Sijui kwa nini wanaume huwa hawahangaiki sana na resque solutions than escaping ones..................... kama mkeo kajisahau si mnajadiliana na kukumbushana?? kwa nini ukae kimya kisha umchape mwenzio na fimboya ndani kama hiyo??

Mimi nilishasema kuwa mwanaume anayegeukia kwa msichana wa kazi/shemeji yake au rafiki wa mkewe kwa jina la kutafuta refuge ya mapenzi ni weak......... anatake advantage ya hao wanawake wenzangu... Kama ni kidume kilichodhulumiwa haki yake ya ndoa au whatever haki basi atafute mwanamke wa nje, mbali kabisa na sio hao.

Unakataa afu mwisho unakubali mwenyewe huyo wa mbali ni mwanamke pia na mara nyingi huwa ni alie karibu ndo atakupindua chunguza vizuri wanaume wengi ikitokea huchukua karibu either kazini ama nyumbani wengine hukimbilia ulevi ambao ni hatari pia.
 
Last edited by a moderator:
Kuna ndugu yangu mmoja alikwenda kwao kujifungua, na kabla ya kwenda kwao mimba yake ilikuwa inamsumbua. Msichana aliopoona mama mwenye nyumba kaondoka. Akawa huru mpaka picha za mama mwenye nyumba zikatolewa ukutani akaweka za kwake. Je kilichofanyika kilikuwa sahihi? Mama mwenye nyumba baada ya kukuta hali hiyo alichukua jukumu la kumfukuza msichana ndani ya muda mfupi.


Hivyo watu hawa siyo wa kuamini sana ndani ya nyumba zetu.
 
Hili ni suala la kuanguka kiimani..nadhani huyo jamaa ameweka mafundisho ya dini kando, na kuamua kusema lolote liwe,,,haiji akilini mtu aache familia yake iteketee kwa ajili ya mwanamke mwingine,,,lazima kuna tatizo kubwa sana tena lililodumu kwa muda mrefu.
Namshauri huyo mke adumu katika kumuomba mungu.
 
Back
Top Bottom