naomba ushauri, mimi ni kijana miaka 28 mke wangu umri huo pia. tumeanza kuishi pamoja 2012 baada ya kumpa Mimba. sasa mwenzangu ni jeuri Kiasi na ana wivu sana na sim zangu. Shida kila wakati ataka tuachane, kwasasa anadai ndugu zangu hawampendi na pili mimi ninawasiliana na wanawake sana. Anataka tuachane tuna watoto 2, nimekua nikimuomba aachane na hayo mawazo kwa mda Sasa. Naomba wenye uzoefu nshauri nifanyeje?
...wewe Unampenda?
una sababu zipi zinazokufanya usimuache?
ni kweli unafanya hayo maswala na ana ushahidi wa usaliti wako?
Kama ni hivo badirika na ufanye kile anachokitaka yaani husiwasiliane na wanawake hovyo pia kama unaishi na ndugu jaribu kuwa mbali nao ili muwe na amani ktk ndoa yenu!
Pole sana kiongozi!
Mkubalie ndio dawa yake. Kadiri anavyokuambia muachane then ukambembeleza ndio ataendelea kukusumbua maana anajua huwezi kukubali na anatumia hio kama silaha/fimbo yake. Na atakuwa keshakujulia unampenda sana na hutaki muachane kwa sababu ya watoto wenu na jina lako pia.
We nenda tu jioni mwambie ''Mke wangu nimekaa nimetafakari naona bora tuachane kama unavyotaka. ukitaka watoto nenda nao au niachie tu'' usiongeze neno nenda kafanye mambo yako mengine....uwe siriazi kweli kweli then uone reaction yake. Sentensi zake tatu za kwanza zishike vizuri...Ndipo ukweli ulipo kama anataka kweli au anatishia.
Nina Jamaa alizaa na dada mmoja, kukawa kuna kitu wametofautiana.. yule binti akamwambia ''njoo chukua takataka yako'' akimaanisha mtoto. jamaa kwa hasira kaenda.. unafikiri binti alikubali? hakutaka kumuachia. akadai lazima nipajue kwenu kwana nione nani atakaa na mwanangu.. jamaa kampeleka, kufika oooh siwezi muacha mwanangu... ''mnajua uchungu wa mwanangu nyie'' then ngoma ikaisha bila bila.
Yawezekana nawe anakuchezea tu akili.. maana mara nyingi huwa hawamaanishi wakisemacho na wakimaanishacho huwa hawakisemi. Mtaalamu Mr Rocky plz leta hekima zako hapa.
Tafadhali kama unamsaliti.... NAKUOMBA kWAROHO MOJA UACHE. WANAO NA FAMILIA YAKO INAKUHITAJI SANA KULIKO UNAVYOJUA.
Asante sana I will do that one day. hata wiki hii alikomaa kuondoka nimemwomba abaki tulee watoto
tumeanza kuishi pamoja 2012 baada ya kumpa Mimba.
Anataka tuachane tuna watoto 2
Hii story mkuu Tized mbona ina utata
wameanza kukaa pamoja 2012 na wana watoto wawili!!!!?????
Na pili je unampenda au anakupenda
Na kama anakupenda au mnapendana je umetulia
Nini kilimfanyaa aanze kupekua simu zako maana kuna wasi wasi ambao ameupata na akaanza kupekua simu zako
Kingine maisha ni yenu wawili ndugu kuingilia mapenzi yenu au mke kudai ndugu zako hawampendi inaingiliana vipi na maisha yenu. Kwani hao ndugu walikuwepo wakati mnaanza mapenzi yenu
naomba ushauri, mimi ni kijana miaka 28 mke wangu umri huo pia. tumeanza kuishi pamoja 2012 baada ya kumpa Mimba. sasa mwenzangu ni jeuri Kiasi na ana wivu sana na sim zangu. Shida kila wakati ataka tuachane, kwasasa anadai ndugu zangu hawampendi na pili mimi ninawasiliana na wanawake sana. Anataka tuachane tuna watoto 2, nimekua nikimuomba aachane na hayo mawazo kwa mda Sasa. Naomba wenye uzoefu nshauri nifanyeje?
Aisee! Mimba ya kwanza 2012,,2014 mna watoto 2,hakika lazma atake muachane,utamuua na mimba za mfululizo.
wakwanza kazaliwa 2011 wapili 2014. Mimi nilimpenda tangu nlipo muona sjui kuhusu yeye. khs ndugu si Kweli kua wanaingilia yeye tu ndo ahisi huvyo
Mapenzi nikusikilizana nikuelewana na kuheshimiana,sasa kama yeye ameonyesha ishara ya kukushiba huna raha ya nyumba
yako kisa nini? akisema tena nataka talaka mwambie lete nikuandikie uone sura yake itakavyo mbadilika,atakushutumu unawanawake tele sujui nini usiwe na mda wakubishana nae baada ya hapo kua na Mamuzi yakiume asikuchokoe roho maisha yenyewe mafupi haya...