Sultan Ali Baba
Mwanamke mmoja wa Uganda amemkimbia mume wake kutokana na mahitaji makubwa ya tendo la ndoa!
Tukio hilo limewashangaza watu wengi Uganda baada ya Ruth Nakyune kumkimbia mume wake alietajwa kwa jina la Sultan Ali Baba.
Ugomvi wa wawili hao umefikishwa katika kituo cha Polisi cha Bulenga ambako mama huyo alimuomba mume wake waachane kutokana na kushindwa kumudu mahitaji ya mume wake.
"Naomba kzachana na ndoa hii kwa kuwa mahitaji ya tendo la ndoa yamekuwa makubwa na ya mara kwa mara" mama huyo alitoa kauli hiyo ktk kituo hicho cha Polisi.
Mama huyo alisema hawezi kuvumilia hali hiyo kwa kuwa anapomwambia hawezi kufanya hivo ugomvi mkubwa hutokea.
Kwa upande wake Sultan alisema mke wake alikuwa akimdanganya na anashindwa kueleza ukweli kwamba ameshindwa kukidhi mahitaji yake.
Rafiki wa sultan alisema ni kweli mama huyo alikimbia nyumbani kutokana na mume wake kuwa na mahitaji makubwa na alifafanua kuwa wake zake wawili wa zamani walimkimbia kutokana na dozi kuwa kubwa.
Baada ya mazungumzo marefu Sultan alimuomba mke wake arejee nyumbani kwa ajili ya kuwatunza watoto, lakini mama alikataa.
Mwananchi, Dec 18, 2014, pg 32.