Haya nyie watoto wa kike
huku someni hii..
Mwanamke mmoja wa Uganda amemkimbia mume wake kutokana na mahitaji
makubwa ya tendo la ndoa. Tukio hilo limewashangaza watu wengi wa Uganda
baa ya Ruth Nakyeyune kumkimbia mume wake alietajwa kuwa ni Sultan Ali
Baba.
Ugomvi wa wawili hao umefikishwa katika kituo cha polisi cha Bulenga
ambako mama huyo alimuomba mume wake waachane kutokana na kushindwa
kumudu mahitaji ya mume wake. Naomba kuachana na ndoa hii kwa kuwa
mahitaji ya tendo la ndoa yamekuwa makubwa na ya mara kwa mara mama
huyo alitoa kauli hiyo katika kituo hicho cha polisi.
Mama huyo alisema hawezi kuendelea kuvumilia hali hiyo kwa kuwa
anapomwambiwa hawezi kufanya hivyo ugomvi mkubwa hutokea kati ya wawili
hao. Nakyeyune alisema inapotokea anaumwa au hajisikii kufanya tendo
hilo, Sultan anabadilika na kukataa kuzungumza nae kwa siku kadhaa.
Kwa upande wake Sultan alisema mke wake amekuwa akimdanganya na
anashindwa kueleza ukweli kwamba ameshindwa kukidhi mahitaji yake. Mara
nyingi amekukwa akiomba msamaha na wakati mwingine amekuwa akitishia
kujiua wakati ninapohitaji huduma alisema Sultan.
Alisema yeye ni mume mwema kwa kuwa hanywi pombe kama walivyo wanaume
wengine na anashangaa kwa nini mke wake anashindwa kumtosheleza licha ya
kuwa na sifa hiyo.
Sultan alisema anashangaa kwa nini mke wake aliamua kuwaacha wazazi
wake na kuamua kuolewa na yeye huku akijua hana uwezo wa kutekeleza
jukumu hilo ipasavyo.
Rafiki wa Sultan alisema ni kweli mama huyo alikimbia nyumbani kutokana
na mume wake kuwa na mahitaji makubwa na alifafanua kwamba wake zake
wawili wa zamani walimkimbia kutokana na dozi kuwa kubwa. Maneno
yote anayozungumza huyo mama ni tuhuma za kawaida, lakini ukweli ni
kwamba anamuogopa mume wake. Na si malalamiko ya kwanza kwani amekuwa
akilalamika mara kwa mara alisema rafiki huyo.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu, Sultan alimuomba mke wake arejee
nyumbani kwa ajili ya kuwatunza watoto, lakini mama alikataa.