Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka (30) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka (30)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngongo, Nov 9, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]MWANAMKE mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa Kibaoni mjini hapa, amewavunja mbavu wasikilizaji wa kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ipembe, baada ya kumjibu Hakimu kuwa kijana aliyemfikisha mahakamani hapo si mwanawe bali mumewe.

  Katika kesi hiyo, mwanamke huyo Asha Abdallah anamshitaki mumewe, Kiemi Itambu (30), kwa kumwibia Sh 30,000 alizokuwa ameficha chini ya godoro.

  Wawili hao wakiwa kizimbani jana, Hakimu Hosea Mkude alimwuliza mke: “Kwa nini wewe bibi unaolewa na kijana ambaye ana umri wa mwanao, huoni aibu?

  Asha alijibu: “Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu.”

  Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha’ hakimu: “Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?”

  Majibu hayo yalisababisha watu waliojazana kwenye chumba hicho cha Mahakama, washindwe kujizuia na kuangua vicheko.

  Ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa Kiemi alitenda kosa hilo Novemba 3, saa mbili asubuhi Kibaoni mjini hapa.

  Asha alidai mahakamani hapo kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kumwibia Sh 100, 200 na 500, lakini safari hii alivuka mpaka kwa kuiba Sh 30,000 ndiyo maana akaamua kumfikisha mahakamani.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje baada ya kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya kutoa Sh 50,000 hadi Novemba 15 kesi hiyo itakapotajwa.

  My take.

  Hii ni hatari kubwa vipi hakuna sheria ya kulinda vijana dhidi ya ubakaji bila kujali jinsia.Sheria ya ubakaji inapendelea wanawake kwanini wanaume tusianadamane kupinga unyanyasaji wa aina hii kibibi kizee miaka 60 kuolewa na kijana wa miaka 30 ni uzalilishaji mkubwa.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni! No comments
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  ah akiisahapevuka tu ni mkubwa huyo; anabaki kuwa mtoto ndani ya familia yenu!
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hili lipost mbona likodublicated??!
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Twende mbele turudi nyuma maneno ya Bibie AshaDii si huyu wa JF yana ukweli ndani yake.

  Asha alijibu: "Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu."

  Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha' hakimu: "Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?"
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Kama kuna thread nyingine Mod waziunganishe hakuna kosa hata wewe ukikutana na uzi mzito kama huu lazima utapenda kuwashirikisha wenzako.

   
 7. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ma-love hayo, hayana macho
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Ndiyo ushangae unaweza kuta mama wa huyu kijana ana miaka 47.

   
 9. Chimps

  Chimps JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 571
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 80
  kama wazee wenzake wameishiwa nguvu, na yeye bado mwili unadai mambo atafanyaje???
  Si jambo la ajabu maana kuna wanaume wazee wa miaka kama 60 wanatoka na vibinti vya miaka 20
  muhimu kama wamependana acha wale raha
   
 10. ram

  ram JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,203
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Mwacheni bibi , kwa raha zake babuweee, sasa kesi ikiisha sijui wataendelea kuwa mume na mke?
   
 11. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Yaelekea JF sasa imeshaanza kuishiwa na mada
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Unapendelea mada za aina gani !.

   
Loading...