Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka 30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka 30

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jakubumba, Nov 9, 2011.

 1. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa Kibaoni mjini hapa, amewavunja mbavu wasikilizaji wa kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ipembe, baada ya kumjibu Hakimu kuwa kijana aliyemfikisha mahakamani hapo si mwanawe bali mumewe.

  Katika kesi hiyo, mwanamke huyo Asha Abdallah anamshitaki mumewe, Kiemi Itambu (30), kwa kumwibia Sh 30,000 alizokuwa ameficha chini ya godoro.

  Wawili hao wakiwa kizimbani jana, Hakimu Hosea Mkude alimwuliza mke: “Kwa nini wewe bibi unaolewa na kijana ambaye ana umri wa mwanao, huoni aibu?

  Asha alijibu: “Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu.”

  Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha’ hakimu: “Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?”

  Majibu hayo yalisababisha watu waliojazana kwenye chumba hicho cha Mahakama, washindwe kujizuia na kuangua vicheko.

  Ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa Kiemi alitenda kosa hilo Novemba 3, saa mbili asubuhi Kibaoni mjini hapa.

  Asha alidai mahakamani hapo kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kumwibia Sh 100, 200 na 500, lakini safari hii alivuka mpaka kwa kuiba Sh 30,000 ndiyo maana akaamua kumfikisha mahakamani.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje baada ya kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya kutoa Sh 50,000 hadi Novemba 15 kesi hiyo itakapotajwa.

  source. Habari leo
   
 2. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Umedesa, huoni mwenzio keshatoa hii habari? Hebu angalia post ya Fidel80.
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni! No comments
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  mods ziunganisheni hizi sredi zimejirudia
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mabibi wa leo wanawafundisha nini watoto na wajukuu wao kama hali yenyewe ndo ivo mtu anajinadi bila wasiwasi
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  "Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu."
  eh! makubwa haya mie napita njia tu!!!!!
   
 7. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hizi kesi nyingine ni noma??? Mwanaume angekuwa na umri wa miaka 60 na mwanamke 30, mwanaume angebambikiwa na kesi ya kubaka, uongo au kweli????
   
Loading...